Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Niongezee tu hata kupaka rangi nyumba yako unahitaji kibali vinginevyo faini! Usifanye shughuri yoyote ya badiliko bila kibali.
Niliweke sawa hili;

kupaka rangi nalo linatokana na wilaya kama hapa Tanzania nadhani ni wilaya mbili ambazo unatakiwa uchukue kibali ni wilaya ya Ilala na Manispaa ya dodoma
 
Tutakupa elimu bure ili ukafuatilie mwenyew labda kukusaidia tutakupatia watu waliopo katika wilaya husika wakusaidie kwa haraka zaidi mana tunafahamiana kutokana na mwingiliano wa kazi zetu

Asante sana mkuu. Nitakutafuta soon kwa upande wa manispaa ya kinondoni. Blessed.
 
Kwa Kitendo cha kubomoa jengo kisa mtu ajafuata utaratibu wa permit ni ukorofi,yawapasa kwenda kulitazama jengo na kama linakizi vigezo kuwe na faini ya kutofuata taratibu.kama halina vigezo ndio libomolewe.
 
Ingefaa process zote zicost hiyo 150000
Lakini kunahitajika hadi sign za msanifu majengo mtaalamu wa ramani cheti sijui cha nn
Malipo ya kila mwaka ya kiwanja
Mpaka uje kuitoa hiyo 150000 utakuta umetumia zaidi ya milion
Kibali ukiwa na 150000 kwa wilaya kama ubungo unakipata haraka tu kikubwa uwe na michoro iliyochorwa na wataalamu
 
Niliweke sawa hili;
kupaka rangi nalo linatokana na wilaya kama hapa Tanzania nadhani ni wilaya mbili ambazo unatakiwa uchukue kibali ni wilaya ya Ilala na Manispaa ya dodoma
Unachoongelea ni utekelezaji tu, Service Levy au ukitaka Kodi ya Maendeleo ipo miaka mingi na wengi walikuwa hawatozwi wakaisahau, sasa imekumbukwa na baadhi wameanza kutozwa, wanaishangaa wanadhani ni kodi mpya kumbe sivyo; Wilaya zote za Dar vibali hivyo vinahitajika kwani sheria na kanuni za Jiji ni moja.
 
Nikitaka kupimiwa kiwanja changu gharama yake inakuwaje gharama zenu?
 
Ahsante sana kwa muongozo...

Vinasumbua sana kupatikana hivyo... unaweza anza kujenga mpaka unamaliza bado hakijatoka... haswa nyumba za makazi...


Cc: mahondaw
 
Ingefaa process zote zicost hiyo 150000
Lakini kunahitajika hadi sign za msanifu majengo mtaalamu wa ramani cheti sijui cha nn
Malipo ya kila mwaka ya kiwanja
Mpaka uje kuitoa hiyo 150000 utakuta umetumia zaidi ya milion
Uoga wako mkuu lakini ukitaka kwa hela hiyo unachukua vizur tu
 
Nikitaka kupimiwa kiwanja changu gharama yake inakuwaje gharama zenu?
Inatakiwa tufike site tuangalie eneo then tukupe mahesabu yote na ushauri pia then siku hizi ukitaka kupunguza gharama mnaweza mkakaa kikao na majiran zako then mkachanga gharama mana peke yako naweza kukuambia mpaka kumaliza mchakato 5M lakin mkiwa wengi mnashare.....Mana sheria ya asaivi natengeneza ramani ya mpango mji sio peke yako bali na watu wa pembeni wataingia kivyovyote vile sasa kupunguza gharama washilikishe
 
5m????
Mh aya
 
Huku mtaani kwa sasa kuna hii changamoto ya kuandikiwa maandishi haya kwenye kuta za nyumba nyingi zinazoendekea kujengwa.

"SIMAMISHA UJENZI, FIKA OFISI YA ARDHI NA VIBALI VYAKO".

Yasemekana ni kutokana na kujenga bila kibali cha ujenzi. Tatizo ni kwamba utaratibu wa kupata hicho kibali una konakona nyingi sana na upigaji ndani yake.

Kupata ramani tu ya architect sio chini ya 100,000/=
Hapo bado kulipia kibali chenyewe
Bado injinia anayeipitisha hajaomba chochote

Kwa kifupi masikini tunaojenga kwa kuungaunga, hizi konakona ndiyo zinatuumiza zaidi. Mnatumia mbinu mbadala ipi kukabiliana na hili kwa mnaojenga maeneo ya mjini?
 
Sisi wa huku vijijini ni kuporomosha tu vibanda bila tatizo lolote lile.
 
Hilo suala huwa linanishangaza sana. Kuna kero nyingi sana mitaani ikiwa ni pamoja na ubovu wa barabara za mitaani, miundombinu mibovu hasa ya uondoshaji maji taka na yale ya mvua.

Kero nyigi hazishughulikiwi kwa wakati kwasababu utaambiwa watendaji wachache, rasilimali fedha hakuna,au tatizo halijulikani kwenye ngazi ya Wilaya na urasimu mwiiingi.

Lakini jaribu kufanya kitu cha maendeleo kama ujenzi wa makazi biashara au anzisha mradi wa kuingiza pesa. Mamlaka zote zinazoitwa za "udhibiti" zitakuja siku hiyohiyo kila mtu akiwa na madai yake na yote yanahitaji uyalipie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…