Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Fahamu kuhusu vibali vya ujenzi, umuhimu wake na namna ya kuvipata

Waambie unajenga ofisi ya CCM, watakuruhusu mara moja.
 
Labda urasimu kipindi cha nyuma lakini asaivi ukifuata njia sahihi utakipata kwa haraka zaidi
Shilingi ngapi kupata kibali cha nyumba ya kuishi mbona haujasema?
Au ndo umeacha ili kuweka mwanya wa rushwa watu wakija kuomba?
 
Si kweli kwamba tunapenda short cut. Shida ni ugumu wa upatikanaji wa huduma. Huo mlolongo si mfupi, kuna miezi ya nenda rudi na karaha hapo. Si ajabu aliyeandaa utaratibu hajawaandaa wahudumu. Matokeo yake ni usumbufu.
manispaa za miji na majiji kuna miungu watu, mbaya zaidi kila mmoja anataka kitu kidogo hii nchi ni corrupt sana
 
Usituite watanzania wajinga hapo ulipo ukifuatiliwa Elimu na Uraia wako unaweza kufa kwa pressure vilevile
Hahaha samahani lakini mkuu
nimesema hivyo kwa sababu unaona mtu anafanya kivingine ukimleta kwenye uhalisia anajifanya anajua sasa ndo ivyo. Kuna mama alijenga maeneo ya mkondo wa maji sasa amemaliza ujenzi naja kumuambia hapa hapafai na namuonyesha na kalavati la maji ndo anapata presha.

hii nchi bana inanifurahishaga sana ila basi ni bora tufiche taaluma zetu ila wanaichi bana wanachosha aisehhh mpaka nakuwa emotional

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kiwanja hakina hati ( hakijapimwa) taratibu zikoje?
 
Kuukamirisha huo mchakato mpaka kuanza ujenzi, mtu unakuwa ushapigwa pesa ambayo huenda ikaringana na gharama za ujenzi wa nyumba mpya

_ where ever you are remember me_
kuukamirisha##kuukamilisha, ikalingana##ikaringana.

Jamii ya fesibuku imevamia huku jamvini.

Hahahaha!!
 
Habarini wote wadau wa JF natumai mpo poa.

Dhumuni langu ni kuomba kufahamishwa vigezo na masharti ya kupata kibali cha ujenzi Wilaya ya Kigamboni, maana mimi ni mgeni kabisa kwenye masuala haya sasa naambiwa sasa hivi hakuna kujenga kiholela mpaka fundi mwenyewe akanikatalia akasema nifuate kibali la sivyo wanakuja kuwadaka mafundi unapigwa faini ya kutosha.

Wadau wenye kujua hili anipe muongozo kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaa ukiendekeza miradi ya wala rushwa hutakuja jenga kamwe. Kama unajenga ghorafa hapo sawa. Lakini kama unajenga squatter lakini pako planned na unatambuliwa na Serikali ya Mtaa kuwa mmiliki wa hicho kiwanja na barabara za mtaa zipo ili ujue uelekeo wa nyumba itakaaje anza kujenga. Kama mafundi wanakuletea kauzibe nipe hiyo kazi nikujengee na team yangu hakuna kulemba!
 
Eti "mpaka fundi mwenyewe akanikatalia akasema nifate kibali la sivo wanakuja kuwadaka mafundi unapigwa fain ya kutosha"

Huyo ni fundi au? Mafundi chao ni kukabidhiwa fungu na kupiga kazi hayo mambo ya kibali cha ujenzi atajua bosi.
 
Back
Top Bottom