Fahamu makosa makubwa matano ya mwanzo ya kisiasa ya Rais Samia ambayo yanamgharimu sasa

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Kwenye siasa kila maamuzi yanazaa matokeo na matokeo yanaweza kuwa chanya au hasi. Hapa chini nitaweka baadhi ya matukio ya kimaamuzi yaliyofanyika kimakosa na Rais Samia mwanzoni mwa utawala wake na yanamgharimu vibaya kwa sasa.

1. Kurithi baraza la mawaziri la Magufuli. Mbali na kuwa lilikuwa ni kosa la kikatiba pia lilikuwa ni kosa la kisiasa. Ule ulikuwa ni udhaifu mkubwa wa Samia kisiasa. Wanasiasa wale wale, leo ndio wanatumika kumzunguka na kunyemelea kiti chake.

2. Kumtengenezea Mbowe kesi ya ugaidi ili kuzima mjadala wa Katiba Mpya. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa la kisiasa. Pasipo sababu ya msingi Samia aliamua kujitengenezea uadui na wapinzani wa CCM. Japokuwa Samia alikuja kuifuta ile kesi baadaye sana lakini itachukua muda mrefu sana kuirudisha hiyo imani.

3. Kuanza mapema wazi wazi harakati za urais 2025 kwa mwamvuli wa kijinsia. Siasa za kuukumbatia uanamke ni sumu inayochukiwa vibaya sana na jamii yenye mtizamo wa mfumo dume na wanawake wanaoamini mwanamke hafai kuwaongoza au kuwatawala. Bila kujua, ghafla wanaume na wanawake wengi wanamchukia rais Samia kwa mtizamo huo.

4. Kuwarudisha haraka serikalini na ndani ya CCM watu waliofukuzwa (kwa haki au chuki) na Magufuli au wanasiasa waandamizi waliokuwepo katika serikali au CCM kipindi cha Kikwete. Watu kama Kinana, January Makamba, Nape etc. Watu wengi wenye mtizamo chanya kuhusu Magufuli wanamuoa Samia kama mtu aliyekuja kuzika yote mema ya Magufuli ili kuyafufua yote mabaya ya Kikwete.

5. Kuwapooza au kuwakumbatia baadhi ya watu wasioweza kufaa kabisa katika utawala wake. Kundi kama la Covid 19, Sukuma gang (Bashiru, Pole Pole) lilipaswa liwe ni hadithi iliyosahaulika ndani ya wiki mbili tu toka Samia aingie madarakani. Uwepo wa hao watu bungeni, serikalini au ndani ya CCM ni kujiharibia kisiasa.

Bado Rais Samia hajachelewa sana, anaweza kurekebisha baadhi ya mambo sasa na baadhi ya mambo kwenda sawia kwa sehemu.
 
Rais ajaye alishatabiriwa na Nabii TB Joshua

Anapiga Jalamba pale kwa Wananchi Jangwani
 
Una upungufu wa akili ama mgonjwa wa alikili
 
Kosa kubwa analofanya ni kukosa uwezo, hana uwezo ndio maana hayo mengine yote hawezi.
 
Mie nadhani baraza angelirithi japo nusu tuu, wengine angewapiga chini.
Makamba, Nepi, Mhagama, Madelu, Rizmoko, Katambi fyekelea mbali.
 
Siasa za kuukumbatia uanamke ni sumu inayochukiwa vibaya sana na jamii yenye mtizamo wa mfumo dume na wanawake wanaoamini mwanamke hafai kuwaongoza au kuwatawala.
 
Sukuma gang ndo kitu gani wewe mpumbavu?

Mtawachukia wasukuma na watani zao kisa waliwatoa malinda, nyanoko.
 
Bado Rais Samia hajachelewa sana, anaweza kurekebisha baadhi ya mambo sasa na baadhi ya mambo kwenda sawia kwa sehemu.
Emu tuanze na hili, unahisi anaweza kulirekebisha kwa mda gan?

Siasa za kuukumbatia uanamke ni sumu inayochukiwa vibaya sana na jamii yenye mtizamo wa mfumo dume na wanawake wanaoamini mwanamke hafai kuwaongoza au kuwatawala.
 
Mkuu

Hii orodha na ziada ya hapo hakuna ambacgo hakuambiwa mama yetupendwa.

Lakini umesahau jambo moja hapo. Kutozihakiki taarifa anazopelekewa na wasaidizi wake.

Pia kupuuzia kupima ushauri anaopewa na wateule wake....

Na pia kuamini kuwa Watanzania ni wajinga milele.

Kumshauri mama muda huu ni kujipotezea muda. Amechagua njia anayoiona ni sahihi tumuache aendelee kusonga mbele.

Tusisahau kumpigia vigelegele kila aendapo maana anaamini kwenye tabasamu la usoni.
 
Kwenye siasa kila maamuzi yanazaa matokeo na matokeo yanaweza kuwa chanya au hasi. Hapa chini nitaweka baadhi ya matukio ya kimaamuzi yaliyofanyika kimakosa na Rais Samia mwanzoni mwa utawala wake na yanamgharimu vibaya kwa sasa.

1. Kurithi baraza la mawaziri la Magufuli. Mbali na kuwa lilikuwa ni kosa la kikatiba pia lilikuwa ni kosa la kisiasa. Ule ulikuwa ni udhaifu mkubwa wa Samia kisiasa. Wanasiasa wale wale, leo ndio wanatumika kumzunguka na kunyemelea kiti chake.

2. Kumtengenezea Mbowe kesi ya ugaidi ili kuzima mjadala wa Katiba Mpya. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa la kisiasa. Pasipo sababu ya msingi Samia aliamua kujitengenezea uadui na wapinzani wa CCM. Japokuwa Samia alikuja kuifuta ile kesi baadaye sana lakini itachukua muda mrefu sana kuirudisha hiyo imani.

3. Kuanza mapema wazi wazi harakati za urais 2025 kwa mwamvuli wa kijinsia. Siasa za kuukumbatia uanamke ni sumu inayochukiwa vibaya sana na jamii yenye mtizamo wa mfumo dume na wanawake wanaoamini mwanamke hafai kuwaongoza au kuwatawala. Bila kujua, ghafla wanaume na wanawake wengi wanamchukia rais Samia kwa mtizamo huo.

4. Kuwarudisha haraka serikalini na ndani ya CCM watu waliofukuzwa (kwa haki au chuki) na Magufuli au wanasiasa waandamizi waliokuwepo katika serikali au CCM kipindi cha Kikwete. Watu kama Kinana, January Makamba, Nape etc. Watu wengi wenye mtizamo chanya kuhusu Magufuli wanamuoa Samia kama mtu aliyekuja kuzika yote mema ya Magufuli ili kuyafufua yote mabaya ya Kikwete.

5. Kuwapooza au kuwakumbatia baadhi ya watu wasioweza kufaa kabisa katika utawala wake. Kundi kama la Covid 19, Sukuma gang (Bashiru, Pole Pole) lilipaswa liwe ni hadithi iliyosahaulika ndani ya wiki mbili tu toka Samia aingie madarakani. Uwepo wa hao watu bungeni, serikalini au ndani ya CCM ni kujiharibia kisiasa.

Bado Rais Samia hajachelewa sana, anaweza kurekebisha baadhi ya mambo sasa na baadhi ya mambo kwenda sawia kwa sehemu.
Nachallenge andiko lako: 1. Sioni tatizo Mhe. Rais kuendelea na baraza la mawaziri ambalo alifanya nalo kazi akiwa VP. 2. Ushahidi wa Mbowe kufunguliwa kesi kisa Katiba haupo, maana uchunguzi ulianza kabla hajawa Rais. 3. Mhe. Rais anapozungumzia gender equality anazungumzia Global Agenda (Gender equality goal No.5, ktk Sustainable Development Goals). 5. Siyo sahihi kueneza ukabila na hicho mnachokiita Sukuma gang ni sumu mbaya. 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom