Habari zenu wajariamali wenzangu.Juzi nilibandika uzi humu wa'Kesho naenda kumbelea shamba langu la milkfish,' Niliahidi kuwapa updates zote nitakapofika site kesho naenda kutembelea shamba langu la mikorosho
Jana nilifika mchana nilipofika tu nikaenda shambi kuangalia mazingira/shamba. Leo kulipokucha tu tulianza safari ya shamba na vijana wangu.
Safari shambani
Shambani mambo sio mabaya mikorosho imeshatoa mauwa na mingine imeshatoa tegu
Mambo mazuri kama unavyoona
Shughuli za leo shambani zilikuwa ni kupuliza dawa na kusafisha shamba ili kuweka mazingira vizuri kwa kusubiria mazao yaanguke.
Historia fupi ya Shamba.
Shamba nilinunuwa mwaka juzi.Shamba lina ukubwa wa ekari mbili lina jumla ya mikorosho 100.Nilianza kulihudia mwaka 2016 kwa kukata mikorosho 40 ya zamani/iliyozeeka na kupanda ya kisasa.Rasmi mwaka jana nilianza kulima kwa maandalizi ya msimu unaokuja.Kwa kuwa nilitumia gharama nyingi sana sikuweza kulihudimia vizuri shamba langu.
Nilitumia jumla ya shilingi 2k kuliandaa.Msimu ulipoanza nilipata jumla ya kg2000 ambayo kwa mwaka jana bei ya @kg1=3500 Hivyo.
2000×3500=7000,000/ nashukuru Mungu mwaka jana mambo yalikuwa mazuri kidogo.Niliweza kutengeneza faida nzuri sana.Mwaka huu nimeongeza bajeti ya shamba kwani wanasema,"The higher the risk the higher the demand".
Nashukuru Mungu mradi wa shamba umenifungulia njia katika ujariamali hadi sasa nimefanikiwa kuwekeza katika maeneo mawili.
Baada ya shughuli kupumzika muhimu
NB Mimi ni mwajiriwa serikalini hivyo changamoto ni nyingi katika kuendesha shughuli hizi za shamba
Karibuni