Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

kweli kabisa mkuu nimepita ukanda wa bagamoyo nimeona namna mikorosho ilivyostawi na kubeba korosho nyingi ilihali haina matunzo kabisa ya kusafishiwa kutifuliwa wala haijawahi kupuliziwa dawa kwa ujumla zinakubali sana ukanda wote wa pwani

HABARI,
"zegebovu1,

Huo ukanda wote ndio Ukanda wa korosho ukiweza kupata heka 10 ukazitunza vema wewe ni tajiri ukipata zaidi ndio inakuwa habari njema zaidi.

Sisi tunalalamika sana mambo ya ajira na mambo mengine ila hii aridhi ya bure tunayoiacha nyasi zinakuwa tukiitumia vema ni utajiri tosha huo ndio msaada pekee Serikali inayotupa kwamba tuna ardhi na upatikanaji wake ni mwepesi nenda nchi kama Rwanda utapata jibu.Endelea kufanya upembuzi Tafuta eneo ukipata kubwa zaidi itakuwa vema.

Ukipata nijulushe nikutumie video ya kufundisha jinsi ya kubebesha mikorosho unaweza kubebesha wewe mwenye ukapunguza gharama.

LUMUMBA
 
Mkuu, ubarikiwe sana naku PM sasa hivi tuongee mambo yenye tija.
 
Mkuu Lumumba, naomba kuuliza. Je, hii niche ambayo serikali inagawa bure inakuwa imebebeshwa? Na je, inamazao mazuri? Tumehamashishwa kulima korosho mwaka huu ila wasiwasi ni ubora wa mbegu.
 
Mkuu Lumumba, naomba kuuliza, Je hii niche ambayo serikali inagawa bure inakuwa imebebeshwa? Na Je inamazao mazuri? Tumehamashishwa kulima korosho mwaka huu ila wasiwasi ni ubora wa mbegu.

HABARI,
"Shark's Style,

Hongera ndugu kwa kuwa na kasi ya kuulizia kuhusu Korosho Ninafarijika sana Naomba niwe muwazi kwani ni fulsa Kubwa ambayo ipo kwetu sasa Lazima watanzania tuichangamkie.

Hii miche ya inayotolewa na Serikali mingi Haikubebeshwa miche ya kubebeshwa inakazi kubwa sana kama ipo ya idadi kubwa ni vigumu Serikali kubebesha miche zaidi ya millioni 10 na kuigawa kwa wananchi.

Hii miche ni ya mbegu ambazo zimefanyiwa utafiti na wataalamu wetu wenyewe kule Naliendele kituo cha utafiti wa mazao Na ujue TANZANIA ni kati ya nchi zinazoongoza kuwa na zaidi ya aina ya mbegu 50 bora Duniani.

Hii miche ni mizuri sana na inaanza kuzaa mapema kwa kuwa si kama ile ya kienyeji hii ni miche iliyoboreshwa hata kwenye swala la magojwa instahimili sana.

Nakushauri usitegemee hii ya Kugawa ya Serikali kwani mingi inakwenda vijijini wewe kama unashamba tayari funga safari nenda Naliendele kule utapatiwa mbegu pamoja na mafunzo ya kutosha ya kuandaa mbegu mpaka kwenda kupanda shambani.Utachelewa sana ukisubiri ile ya kugawa pia ya kugawa ina idadi uataambiwa kila kaya miche 100 wakati wewe unataka miche 5000.

MAWASILIANO YA KITUO CHA UTAFITI NALIENDELE

Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com

http://www.erails.net/TZ/nari-naliendele/ari-naliendele/


LUMUMBA
 
Je korosho haiwezi kustawi kanda ya ziwa?

HABARI,
"Mzila nkende,
Samahani sana sikuliona hili swali lako Naomba niseme hivi zaidi ya asilimia 75 ya eneo lote la Tanzania zao la korosho linakubali nimetoa mfano mdogo sana kama mikoa ya dodoma na singida ambayo ndio mikoa kame Tanzania korosho inakubali kanda ya ziwa mikorosho inakubali usiwe na shaka.

LUMUMBA
 
Hii Miti 120 inakaaje au kueneaje kwenye Heka moja kaka?mYaani umbali kutoka mti hadi mti ni upi?
Na kutoka mstari hadi mstari ni umbali gani?
 
Naliendele wanauza hii Miche kwa kiasi gani?
 
Kaka ngoja na mimi nijiandae by mwaka kesho nianze iki kilimo cha korosho
 
Hii Miti 120 inakaaje au kueneaje kwenye Heka moja kaka??
Yaani umbali kutoka mti hadi mti ni upi??
Na kutoka mstari hadi mstari ni umbali gani??

HABARI,
"Shark,
Ok safi kwa swali zuri,Nikujulishe kitu kimoja mimea mingi ya kupandikizwa hua haiwi mikubwa sana kwakuwa tayari uzao wake ukokaribu yani inajitambua kwamba tayari imeshakuwa mikubwa,Ni kama ukuaji wa mtoto binadamu anavyozidi kukua ndio kasi ya ukuaji inavyopungua tofauti na mtoto.

Sasa kwakuwa hii miti inaanza kutao mavuno ndani ya miaka 2-3 kwakuwa umetoa kwenye kikonyo yenyewe inajielekeza kwenye kutoa mazao na sio kukua tena kwa hilo ukuaji wake ni taratibu wakati inatoa mazao.

Sasa tukirudi kwenye swali lako ni kwamba heka ina 70 kwa 70 na Kwenye upandani upana wa mstari na mstari ni mita 7
na upana wa mti na mti ni mita 5-6 na kwa Heka hapo utapata jibu na kwa mpangilio huo unaweza kukaa kwa zaidi ya miaka 15 kwa mpangilio huo.

LUMUMBA
 
Ahsante kwa elimu mkuu
 


HABARI,
Pia kwa huo mpangilio wa upana kati ya mstari na mstari mti na mti Kule Dodoma wilaya ya mpwapwa gereza la pale wanashamba lenye mikorosho ya miaka kumi kwa mwaka mikorosho ile inatoa mpaka kilo 30 kwa mkorosho mmoja na ina miaka kumi tu ukiangalia mti hauna unapana hata wa mita 2.5 ila ikifikia zaidi ya mika 25 kama imeanza kubanana unaweza kupunguza mkorosho mmoja kati ya mitatu ila unakuwa tayari umeshapata mavuno zaidi ya mika 20 kwa mkorosho utakao utao ili kupata nafasi.

Pia kwa kutumia mikorosho hiyo unaweza kuandaa mwenyewe miche mingine ya kubebesha kwa kutumia vikonyo kutoka kwenye mikorosho hiyohiyo ukaongeza idadi ya miti,

LUMUMBA
 
Mkuu lumumba Shukrani sana kwa somo lako nimelielewa vizuri, Naihitaji hiyo video ya jinsi ya kubebesha miche nitaipataje mkuu? Je, unaweza kunitumia PM, kama kwenye jukwaa hili inashindikana?
 
Mkuu lumumba Shukrani sana kwa somo lako nimelielewa vizuri, Naihitaji hiyo video ya jinsi ya kubebesha miche nitaipataje mkuu? je unaweza kunitumia PM, kama kwenye jukwaa hili inashindikana?


HABARI,

"kimpupu,
Ok Hongera na Asante kwa kuelewa soma,Nivumilie kidogo kabla ya saa kumi jioni leo nitapost video 2 au zaidi hapa zinazoonyesha jinsi ya kubebesha mikorosho(cashew grafting method).

LUMUMBA
 
Mkuu lumumba Shukrani sana kwa somo lako nimelielewa vizuri, Naihitaji hiyo video ya jinsi ya kubebesha miche nitaipataje mkuu? je unaweza kunitumia PM, kama kwenye jukwaa hili inashindikana?


HABARI,
Kwanza niwapongeze wadau wote mnaofatilia Kilimo cha korosho.
"Thesis, kimpupu, "Mshuza2,, SUKAH, Gu Jike , ankai, Shark , Mndengereko One ,Na wengine

Nime Post video 4 zinazoonyesha jinsi ya kubebesha miche ya mikorosho (grafting).Ukiangalia kwa vitendo inatosha,Kama una swali niulize.





LUMUMBA
 
Asante sana kwa elimu hiyo broo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…