Haya maboss zangu naona uzi ulianza vizuri ila kama ukaanza kutoka nje ya rengo. Sote tupo hapa kuelimishana. Hatutafuti washindi.
Ila Natumai wote mpo poa.
Mim kijana mwenzenu natokea Katavi mpanda. Na ni mkulima wa zao la korosho kwa miaka miwili sasa.
Kwa kifupi nilichopitia kwenye kilimo hiki kinatia moyo kwa kweli, miche inakua vizuri haina shida sana, ukiipa huduma kidogo ina respond vizuri sana. Kwa ufupi
Shamba nilinunua eka nyingi tuu. Kwa eka moja nilinunua kwa 100,000 kufyeka na kuzoa 100,000 kuchimba mashimo 30 bei 5000 (watu wa day) kupanda 30 bei 5000 (watu wa day). Na kila baada ya miezi 6 ni kufanya usafi, kupiga dawa na kuweka mbolea basi, kwa sasa nipo mwaka wa pili wa kupanda. Mungu akinijalia naweza nikavuna mwaka huu. Maana nilipanda mwaka jan 2020.
Kiukwelu nimepata epxerience kubwa sana kwa upande wangu na nimejifunza mengi mpaka sasa. Ila maswali yangu ni machache, hasa kipindi hiki ninachoelekea kwenye mavuno.
SWALI.
1. Huku kwetu Katavi ni wageni wa hichi kilimo wengi wetu tumeanza miaka ya hivi karibuni, kwa nyinyi mlioko huko mtwara hua mnafanya nini zaidi kwenye upande wa soko? Na kuna mahala mmekuwa mnaongelea kuhusu minada hiyo minada inakuaje? Je ipo uko uko Mtwara au inafanyika online? Ni physical kama ile ya nguo ama inakuaje? Na mtu anawezaje kushiliki? Hasa wa nje ya mtwara.
2. Halafu pia kwa upande wa kilimo ni vitu gani hasa mkulima anapaswa kufanya inapokaribia muda wa miche kutoa maua na matunda? Je kuna mbolea ya kuweka? na ni ipi?? Vipi kuhusu sumu za kupulizia ni zipi?
3. Swali la mwisho. Je ni muhimu miche kupruniwa matawi ya chini na kubakisha matawi ya juu. Je hii ina faida na hasara gani?
Hongera na karibu sana kwenye kilimo cha korosho..hakika ni uthubutu mkubwa..naomba nikujibu maswali yako kama ifuatavyo.
1.Minada ya ununuzi wa korosho huendeshwa na vyama vikuu vya ushirika kwa huku Mtwara na masasi kinaitwa MAMCU vito vingi kulingana eneo..lindi..tandahimba..pwani kote huko vipo..ndani ya hivyo vyama vikuu kunakua na vyama vidogo vidogo ambavyo vinapatikana kwenye kata ama kijiji husika ambapo wanachama wake ni wakulima wa kijiji au kata husika.
Hivyo kipindi cha mavuno kikianza wakulima huvuna korosho na kuzipeleka kwenya maghala ya vyama vyao husika katika kijiji..hupimisha wingi wa kilo kisha hupewa risiti ambapo mfumo huu unaitwa stakabadhi ghalani.
Kisha chama kikuu cha ushirika kushirikiana na Bodi ya korosho huitisha mnada ili kununua korosho zote katika wilaya ambapo hicho chama kinafanya kazi.
Hivyo matajiri huja..na bei elekezi hua imapangwa na bodi ya korosho kwa mwaka husika hivyo wa nunuzi hawatakiwi kushuka chini ya bei husika bali kupanda..hivyo hushindana kila mmoja kwa bei yake na idadi ya kilo atatakazo nunua..hivyo bei ya juu kupatikana huletwa mbele ya wanachama/wakulima wakiridhia ndio inakua bei ya mnada wa kwanza wasipo ridhia mnada unafanyika kipindi kingine tena...kama bei imekubaliwa na mkulima basi mnunuzi/wanunuzi wote wananunulia kwa bei hiyo.
Mzigo wa korosho utachukuliwa..kisha malipo huanza kufanyika kupitia akaunti ya mkulima husika..maranyingi ndani ya mwezi malipo hufanyika.
Pia kumbuka minada hufanyika kila baada ya wiki..na bei hushuka au kupanda kulingana na uhitaji wa korosho.
2.Kuelekea mavuno shamba huwa linasafishwa kuondoa nyasi na takataka..kisha kipindi cha kuchipua maua..kunakua na upuliziaji wa dawa hususani dawa ya sulful na booster..ili kuondoa ukungu/fungus ambao hathiri majana na kupukutisha maua..upuliziaji hufanyika zaidi ya mara 4 inategemea na hali ya hewa pia hali ya magonjwa katika shamba husika.
3.Inashauriwa kuprun miti ya mikorosho tangu ikiwa midogo ili kuondoa maotea ya pembeni..kwani mti ukiwa mkubwa huinama na kugika chini..pruni kila mwaka hadi mti ukiwa na miaka mi3.
Ni hayo tu kwa leo kama una mengine karibu tushauriane..natumaini kuna mengi wadau wataongezea..kila la kheri.
#MaendeleoHayanaChama