Fahamu tafsiri sahihi ya kosa la uhaini na adhabu yake usije ukasema watu wanaonewa

Fahamu tafsiri sahihi ya kosa la uhaini na adhabu yake usije ukasema watu wanaonewa

Huo siyo ushahdi wa kushawishi au kuchochea; hapo walikuwa wanatoa maoni yao kuhusu jinsi ya kusonga mbele. Hawajakusanya watu wakawashawishi na kuwachochea. Polisi wangekuwa makini, wanagesubiri watuhumiwa hao wakusanye watu waanzae kuwashawishi. Na elewa kushahwishi na kuchochea siyo sentensi moja tu, ni process kama kutongoza; unamwambia mtu afanye jambo haelewi au hataki, unarudia tena na tena hadi anakubali.
 
Mkuu kichuguu unahaki ya kutoa maoni na kila mtu anayo. Mwalimu Nyerere alitoa maoni kuwa haoni na halizishwi na sababu za kuiuza NBC ila hakufikia hatua ya kusema wala kwambia watu waandamane ili kuiondoa serikali. Mwalimu huo uwezo alikuwa nao na watu wangeandamana. Mwisho wa siku leo tuna NBC tena inadhamini ligi ya mpira na tuna NMB iko mpaka kwenu.
Nyinyi leteni siasa hawa watu watafungwa na hamtawaona mitaani kama serikali ikiaamua kuishi kwa kutumia sheria.
Huna hoja kwahiyo una maanisha viongozi wanalindana?
 
Uhaini ni kosa la jinai analofanya mtu dhidi nchi yake na mtu anyefanya kosa hili anajulikana kama msaliti.Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini. kifungu 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote akifanya haya atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini:
  1. kujaribu kumuua Rais,
  2. kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano,
  3. kusababisha,
  4. kuwezesha,
  5. kuchochea,
  6. kushawishi,
  7. kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais
  8. kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali,
  9. kupindua serikiali iliyo madarakani,
  10. kutishia serikali, bunge au mahakama.
Kwa watu wenye akili timamu dr Slaa, Wakili Mwambukusi, na mtukanaji mkuu wa seriakli Mdude Nyangali hawawezi kuwa wamekwepa amri hizi kumi za uhaini
Mungu akubariki uishi siku nyingi ili uyaone mengi
 
Ndiyo unavyojidanganya, kwenye jinai nia tu inakufunga. Kwenye uhalisia rejea kesi ya akina Kadego wakati wa Nyerere, kwani hata walimgusa, walikamatwa kama kuku wakala mvua za kutosha. kwa kukuongezea kule kanisani watu husali hivi
UNGAMO LA DHAMBI.

Nakuungamia Mungu Mwenyezi; nanyi ndugu zangu, kwani nimekosa mno
  1. kwa mawazo,
  2. kwa maneno,
  3. kwa vitendo, na
  4. kwa kutotimiza wajibu.

Nimekosa mimi, nimekosa mimi, nimekosa sana. Ndio maana nakuomba Maria mwenye heri, Bikira daima, Malaika na watakatifu wote, nanyi ndugu zangu, niombeeni kwa Bwana Mungu wetu.
Kati ya hayo mambo manne Slaa, Mwambukusi na Mdude wametimiza 1,2, na 4 sijui wanaponea wapi
kwenye jinai ni vitu 2 tu ndugu yangu- mens rea and actus reus - hebu dadavua hizo kwanza tuone kama watafungwa. Vnginevyo ni hearsay tu...
 
Ni vigumu kuprove kuwa walishawishi au walichochea; wao walikuwa wanatoa maoni yao.

Iwapo kila anayeongelea makosa ya serikali atachukuliwa kuwa anachochea au anashwawishi basi maana ya demokrasi inakuwa imekwishai kwa kuondoa kipengele kinachomruhus raia kwenda popote au kusema lolote mradi havunji shreia. Kwa sababu kukosoa serikali itakuwa ni uvunjanji wa sheria.

Ninachomhurumia Dr. Slaa ni kwa vile aliwahi kuwa Padre wa kikatoliki. Kwenye utawala kama huu, yeye ataonekana mgalatia anayeleta vurugu na ni lazima anyamazishwe kwa njia zozote hata ziwe haramu.
N i jambo ambalo limegeuzwa kuwa la kidini kwa vile linahusisha waarabu ambao wana uhusiano wa karibu sana na dini ya kiongozi wa nchi.
Uko sahihi kuna watu wanapinga udini ila asilimia 70% ya watu wao ni wadini kwa asili.
 
kwenye jinai ni vitu 2 tu ndugu yangu- mens rea and actus reus - hebu dadavua hizo kwanza tuone kama watafungwa. Vnginevyo ni hearsay tu...
Mkuu wewe unadhani walitunga sheria hiyo ni wajinga -subiri uone.
 
Mdude kwa kweli serikali ilale naye tu matusi yalizidi, aliona ana haki ya uzalendo kuliko uzalendo wenyewe. Wacha aliwe kichwa.

Hao wengine serikali iwafikirie

NB: Kabla hujaamua tetea kitu fikiria kuhusu familia yako kwanza, usiwatetee wasiojielewa
 
Uhaini ni kosa la jinai analofanya mtu dhidi nchi yake na mtu anyefanya kosa hili anajulikana kama msaliti.Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania, mtu akifanya yafuatayo huhesabiwa kama amefanya kosa la jinai la uhaini. kifungu 39 ( 1 ) cha kanuni za adhabu kinasema kuwa mtu yeyote ambaye yumo ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote akifanya haya atakuwa ametenda kosa la jinai ambalo ni kosa la uhaini:
  1. kujaribu kumuua Rais,
  2. kuanzisha vita dhidi ya Jamhuri ya Muungano,
  3. kusababisha,
  4. kuwezesha,
  5. kuchochea,
  6. kushawishi,
  7. kushauri kuhusu kifo, kumlemaza, kumzuia, kufungwa kwa Rais
  8. kumwondolea Rais heshima na jina la mkuu wa nchi, amiri jeshi mkuu, au kiongozi wa serikali,
  9. kupindua serikiali iliyo madarakani,
  10. kutishia serikali, bunge au mahakama.
Kwa watu wenye akili timamu dr Slaa, Wakili Mwambukusi, na mtukanaji mkuu wa seriakli Mdude Nyangali hawawezi kuwa wamekwepa amri hizi kumi za uhaini
Namba 8 inamuhusu Nape pamoja na Kinana waliosema rais ni mshamba na amechanganyikiwa
 
Rushwa ya DP World isitutenganishe Watanzania ni wamoja.
Tufanyeni mijadala tufanyeni makongamano tufanyeni siasa lakini tuwe wajanja sio tushawishi Nchi hii iwe na Lawlessness.

Kila mtu ana kisasi fulani na mwenzake sasa bila polisi si tutamalizana
 
wenyewe.Sheria haisemi mtu akitamka maneno ya kuchochea mapinduzi dhidi ya Rais maana yake anakuwa ametenda kosa
Screenshot_20230816_173725_Adobe Acrobat.jpg
 
Back
Top Bottom