Fahamu tofauti kati ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha

Fahamu tofauti kati ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2021
Posts
600
Reaction score
1,843
Eid ul-Fitr maana yake ni "sikukuu ya kumaliza mfungo" na kutumiwa kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Siku hii huwa ni siku rasmi ya mapumziko katika mataifa mengi yenye waumini wengi wa Kiislamu. Hata hivyo idadi ya siku za mapumziko huwa tofauti katika nchi mbalimbali.

Waislamu huanza sherehe hizi kwa kukusanyika kwa maombi ya kila mwaka ambayo hufanyika muda mfupi baada ya macheo.

Ni kawaida kuwaona Waislamu wakikusanyika katika misikiti na viwanja vya wazi kwa maoni ya pamoja.

Kabla ya ibada hiyo, huwa wanatoa sadaka kwa maskini (huitwa Zakat) ambayo ni moja ya nguzo kuu katika dini ya Kiislamu.

Ni kawaida kwa miji mikuu mataifa ya Kiislamu kupambwa sana na sherehe kubwa kuandaliwa, watoto kununuliwa nguo mpya na kupewa zawadi mbalimbali.

Siku hii huadhimishwa baada ya kuonekana kwa mwezi wa Shawwal.

Eid al-Adha ndiyo sikukuu kuu zaidi ya kidini miongoni mwa Waislamu kote duniani na pia huwa ni siku ya mapumziko mataifa mengi yenye Waislamu.

Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu ya kutoa kafara/kuchinja" kwa Kiarabu na hutumiwa kukumbuka wakati nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ismael alivyoamriwa na Allah, lakini akapewa kondoo na Mungu amtoe kafara badala yake.

Sikukuu ya Eid ul-Adha huadhimishwa kuanzia siku ya 10 tangu kuonekana kwa mwezi wa Dhu al-Hijjah.

Ibada ya Hajj kwenda Mecca huanza siku mbili kabla ya Eid al-Adha na tarehe yake huthibitishwa baada ya kuoenakana kwa mwezi huo wa Dhu al-Hijjah.

Eid al-Adha ina majina mbalimbali katika mataifa ya Kiislamu

Waislamu pia huvalia mavazi yao mazuri na ya kupendeza siku hii na huenda msikitini kwa maombi.
Baadhi humchinja ng'ombe, mbuzi au kondoo kukumbuka kitendo cha imani cha nabii Ibrahimu.
Hula chakula chenye nyama na huwapa jamaa, majirani na maskini nyama ya mnyama waliyemchinja.

Eid Mubarak kwa Kiarabu maana yake ni "sherehe au sikukuu njema au yenye Baraka".

Ni salamu za kawaida wakati wa sikukuu za Eid.

eid-al-adha-mubarak-template-design-fec47ba1698e837a4b3f71856d462158_screen.jpg
 
Nikuulize kidogo, kawaida mwezi ni mmoja kwa muonekano, lakini kwenu mmeutofautisha kuna mwezi wa Eid - ul - Fitr na mwezi wa Eid - al - Adha, unaweza kuniambia ni wakati gani mnapoutofautisha kusema mwezi wa Eid - ul -Fitr umeisha sasa unaingia mwezi wa Eid - al - Adha?
 
ni Ishmael au Isaka?
Ni Isack, Ishmael alikuwa ni Yule Mtoto wa Ibrahim kutoka Kwa house girl Kwa MJIBU wa biblia, Ila Kwa kuwa hivi ni vitabu viwili tofauti basi huenda kitabu pendwa kinaelezea hivo
 
Ni mkristo ila andiko lako nimelifurahia

Nb.Licha ya kuwa mm ni beberu msinichinje eid ul adha hii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] (just joking)
Tunashukuru ndugu yetu, karibu sana upate ubwabwa na kitoweo
 
Waislamu na Wakristu wameibiana notes kwenye hiyo stori ya Ibrahimu kutaka kumtoa mwanae kafara alfu Mungu akampa kondoo
Ishmael kwa Kiarabu ni: ( إسماعيل, Ismaeyl) ndiye mtu anayejulikana katika dini ya Kiyahudi, Ukristo, na Uislam kama mwana wa Abraham au (Ibrahim), aliyezaliwa na Hagar (Hajar).
Katika Uislam, Ismail anachukuliwa kama nabii wa MUNGU na pia ni babu kwa mtume Muhammad (s.a.w) . Pia alihusishwa na ujenzi wa Kaaba huko mjini Makka.
 
Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu ya kutoa kafara/kuchinja" kwa Kiarabu na hutumiwa kukumbuka wakati nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ismael alivyoamriwa na Allah, lakini akapewa kondoo na Mungu amtoe kafara badala yake.
Msaada:
  1. Watoto wa Ibrahim walikuwa ni nani na nani
  2. Yupi kati yao alikuwa mkubwa
 
Ni Isack, Ishmael alikuwa ni Yule Mtoto wa Ibrahim kutoka Kwa house girl Kwa MJIBU wa biblia, Ila Kwa kuwa hivi ni vitabu viwili tofauti basi huenda kitabu pendwa kinaelezea hivo
Hicho kisa kizima cha Ibrahimu kutaka kumchinja mtoto wake sijawahi kukisoma popote kwenye Quran, labda kwenye biblia na hadithi za mtume.
 
Nikuulize kidogo, kawaida mwezi ni mmoja kwa muonekano, lakini kwenu mmeutofautisha kuna mwezi wa Eid - ul - Fitr na mwezi wa Eid - al - Adha, unaweza kuniambia ni wakati gani mnapoutofautisha kusema mwezi wa Eid - ul -Fitr umeisha sasa unaingia mwezi wa Eid - al - Adha?
Ahsante ndugu muulizaji na kwa faida ya wengine. Sisi waisilamu tuna miezi yetu ya kiisilamu ambayo ni miezi 12, miezi hii kwa lugha ya kiswahili tunaidadavua kama wa Mfungo.

Eidil-Fitir
(siku kuu ya kula) hii ni siku kuu baada ya kumaliza funga ya swaum katika Mwezi wa Ramadhan ambao kwa kiswahili mwezi wa Ramadhani huitwa mfungo 12. Ramadhan ndio jina la mwezi wa 9 wa kiisilamu, kwa kiswahili ni mfungo 12. Mwezi huo wa Ramadhan, ni lazima waisilamu wafunge mwezi mzima, na wakimaliza kufunga wanasheherekea siku kuu ya kula inaitwa EIDIL - FITR.
Ramadhan = september = mwezi wa 9 = mfungo 12 kwa kiswahili

Eidil- Adh-ha ambayo pia huitwa Eidil-Hajj (Siku kuu ya kuchinja au Siku kuu ya Hija). Hii ni siku kuu ambayo hupatikana kwenye mwezi wa 12 wa kiisilau unaoitwa DHUL-HIJA ambao kwa kiswahili ni mfungo 3. Katika mwezi huu ndio mwezi ambao waisilamu wanatakiwa waende kuhijji Makka (kutufu madhambi), huu ndio mwezi wa 12 yaani mwisho wa mwaka wa kiisilamu, kwa hivyo kwa tukio la wao kwenda kuhijji na kumaliza hijja ndio inatakiwa kusheherekea na ndio maana ikaitwa EIDIL-HAJJ (Siku kuu ya hija). Lakini pia tarehe kama hizo kuna tukio kubwa lilitokea, ambapo Ibrahim alimriwa amchinje Ismail, na kafara yake akachinjwa mnyama. Kwa tukio hilo ndio ikaitwa pia Eidi ya kuchinja yaani (Eidil-Adh-ha).
Dhul-hija = December = mwezi wa 12 = mfungo 3 kwa kiswahili.

Hapa chini nimekuwekea orodha ya miezi ya kiisilamu kama utapenda kuisoma

Mwezi wa 1 unaitwa MUHARAMU = Kwa kiswahili ni Mfungo 4
Mwezi wa 2 unaitwa SWAFAR = Kwa kiswahili ni Mfungo 5
Mwezi wa 3 unaitwa RABIUL-AWAL = Kwa kiswahili ni Mfungo 6

Mwezi wa 4 unaitwa RABIUL-AKHIR = Kwa kiswahili ni Mfungo 7
Mwezi wa 5 unaittwa JAMADIL-AWAL = Kwa kiswahili ni Mfungo 8
Mwezi wa 6 unaitwa JAMADIL-THANI =Kwa kiswahili ni Mfungo 9

Mwezi wa 7 unaitwa RAJABU = Kwa kiswahili ni Mfungo 10
Mwezi wa 8 unaitwa SHAABAN = Kwa kiswahili ni Mfungo 11
Mwezi wa 9 unaitwa RAMADHAN = Kwa kiswahili ni Mfungo 12

Mwezi wa 10 unaitwa SHAUWAL = Kwa kiswahili ni Mfungo Mosi
Mwezi wa 11 unaitwa DHUL-KADA = Kwa kiswahili ni Mfungo pili
Mwezi wa 12 unaitwa DHUL-HIJA = Kwa kiswahili ni Mfungo tatu
 
Msaada:
  1. Watoto wa Ibrahim walikuwa ni nani na nani
  2. Yupi kati yao alikuwa mkubwa
Maisha mazima ya Ibrahimu yametajwa kwa kina kwenye Biblia, kwenye Quran hayako kamili wala bayana, yameguswa guswa.

Kwa rejea za Biblia, mtoto mkubwa wa Ibrahimu alikuwa ni Ishmaili, lakini alikuwa ni mtoto wa mchepuko wake (house girl wake). Mtoto halali wa ndoa alikuwa Isaka, huyo ndio alizaa na mkewe, kimiujiza fulani na ndio alihaidiwa kuwa mrithi wa baraka kuu za uzao wake.
 
Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu ya kutoa kafara/kuchinja" kwa Kiarabu na hutumiwa kukumbuka wakati nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ismael alivyoamriwa na Allah, lakini akapewa kondoo na Mungu amtoe kafara badala yake.
Maisha mazima ya Ibrahimu yametajwa kwa kina kwenye Biblia, kwenye Quran hayako kamili wala bayana, yameguswa guswa.

Kwa rejea za Biblia, mtoto mkubwa wa Ibrahimu alikuwa ni Ishmaili, lakini alikuwa ni mtoto wa mchepuko wake (house girl wake). Mtoto halali wa ndoa alikuwa Isaka, huyo ndio alizaa na mkewe, kimiujiza fulani na ndio alihaidiwa kuwa mrithi wa baraka kuu za uzao wake.
Hapa ndipo pananichanganya
  1. Ismael
  2. Ishmaili
  3. Isaka
alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ismael
Mtoto halali wa ndoa alikuwa Isaka,

Hawa kwenye biblia wametajwa kana nani na nani
 
Eid al-Adha ndiyo sikukuu kuu zaidi ya kidini miongoni mwa Waislamu kote duniani na pia huwa ni siku ya mapumziko mataifa mengi yenye Waislamu.

Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu ya kutoa kafara/kuchinja" kwa Kiarabu na hutumiwa kukumbuka wakati nabii Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ismael alivyoamriwa na Allah, lakini akapewa kondoo na Mungu amtoe kafara badala yake.

Mtoto wa kwanza ni Isma'eyl (Ishmael)
Mtoto wa pili ni Is-ḥaaq (Isaac)
Kwahiyo tumwombe mleta mada aweke record sawa, amepotosha
 
Back
Top Bottom