Ahsante ndugu muulizaji na kwa faida ya wengine. Sisi waisilamu tuna miezi yetu ya kiisilamu ambayo ni miezi 12, miezi hii kwa lugha ya kiswahili tunaidadavua kama wa Mfungo.
Eidil-Fitir (siku kuu ya kula) hii ni siku kuu baada ya kumaliza funga ya swaum katika Mwezi wa Ramadhan ambao kwa kiswahili mwezi wa Ramadhani huitwa mfungo 12. Ramadhan ndio jina la mwezi wa 9 wa kiisilamu, kwa kiswahili ni mfungo 12. Mwezi huo wa Ramadhan, ni lazima waisilamu wafunge mwezi mzima, na wakimaliza kufunga wanasheherekea siku kuu ya kula inaitwa EIDIL - FITR.
Ramadhan = september = mwezi wa 9 = mfungo 12 kwa kiswahili
Eidil- Adh-ha ambayo pia huitwa Eidil-Hajj (Siku kuu ya kuchinja au Siku kuu ya Hija). Hii ni siku kuu ambayo hupatikana kwenye mwezi wa 12 wa kiisilau unaoitwa DHUL-HIJA ambao kwa kiswahili ni mfungo 3. Katika mwezi huu ndio mwezi ambao waisilamu wanatakiwa waende kuhijji Makka (kutufu madhambi), huu ndio mwezi wa 12 yaani mwisho wa mwaka wa kiisilamu, kwa hivyo kwa tukio la wao kwenda kuhijji na kumaliza hijja ndio inatakiwa kusheherekea na ndio maana ikaitwa EIDIL-HAJJ (Siku kuu ya hija). Lakini pia tarehe kama hizo kuna tukio kubwa lilitokea, ambapo Ibrahim alimriwa amchinje Ismail, na kafara yake akachinjwa mnyama. Kwa tukio hilo ndio ikaitwa pia Eidi ya kuchinja yaani (Eidil-Adh-ha).
Dhul-hija = December = mwezi wa 12 = mfungo 3 kwa kiswahili.
Hapa chini nimekuwekea orodha ya miezi ya kiisilamu kama utapenda kuisoma
Mwezi wa 1 unaitwa MUHARAMU = Kwa kiswahili ni Mfungo 4
Mwezi wa 2 unaitwa SWAFAR = Kwa kiswahili ni Mfungo 5
Mwezi wa 3 unaitwa RABIUL-AWAL = Kwa kiswahili ni Mfungo 6
Mwezi wa 4 unaitwa RABIUL-AKHIR = Kwa kiswahili ni Mfungo 7
Mwezi wa 5 unaittwa JAMADIL-AWAL = Kwa kiswahili ni Mfungo 8
Mwezi wa 6 unaitwa JAMADIL-THANI =Kwa kiswahili ni Mfungo 9
Mwezi wa 7 unaitwa RAJABU = Kwa kiswahili ni Mfungo 10
Mwezi wa 8 unaitwa SHAABAN = Kwa kiswahili ni Mfungo 11
Mwezi wa 9 unaitwa RAMADHAN = Kwa kiswahili ni Mfungo 12
Mwezi wa 10 unaitwa SHAUWAL = Kwa kiswahili ni Mfungo Mosi
Mwezi wa 11 unaitwa DHUL-KADA = Kwa kiswahili ni Mfungo pili
Mwezi wa 12 unaitwa DHUL-HIJA = Kwa kiswahili ni Mfungo tatu
Hayo masuala ya mfungo 3 na mfungo 6 ni mambo ya kipuuzi ambayo tunatakiwa tuachane nayo, Tuache kuipeleka dini kimazoea