Fahamu tofauti kati ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha


Hayo masuala ya mfungo 3 na mfungo 6 ni mambo ya kipuuzi ambayo tunatakiwa tuachane nayo, Tuache kuipeleka dini kimazoea
 
Asante, nimesoma nakuelewa, nikuongeze swali dogo, nimeona mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa 9 na ndio pekee huwa mnafunga, sasa kwanini na hii miezi mingine nayo mmeipa majina ya "mfungo" wakati huwa hamfungi?
 
Kwenye Biblia Isaka ndo alitakiwa kutolewa kafara alf kwenye Quran Ishmael ndo alitakiwa kutolewa sadaka

Kila mtu anavutia upande wake
 
Asante, nimesoma nakuelewa, nikuongeze swali dogo, nimeona mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa 9 na ndio pekee huwa mnafunga, sasa kwanini na hii miezi mingine nayo mmeipa majina ya "mfungo" wakati huwa hamfungi?
Kabla ya yote itambulike kuwa mwezi mtukufu wa Ramadhani na ambao ndio mwezi maarufu zaidi kwa walio wengi ni mwezi wa tisa(9) katika mpangilio wa miezi 12 ya kiislam.
Lakini kutokana na taratibu za kimila na kitamaduni kwa kuwa mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa mfungo basi ilizoeleka kuiita miezi mingine ya kiislam kwa kuipa namba ya kuwa ni mwezi wa ngapi kufungua baada ya mwezi wa mfungo ambao ni Ramadhani, hivyo mwezi wa kwanza kufungua baada ya Ramadhani ambao ni Shawwal uliitwa mfunguo mosi au "Mfungo mosi" , mwezi wa pili kufungua tokea kuisha kwa Ramadhani ambao ni Dhulqaa'dah nao uliitwa mfunguo pili au "Mfungo pili" nakuendelea kama inavyooneshwa hapa chini

9.Ramadhani (mwezi wa mfungo)
10.Shawwal (Mfungo mosi)
11.Dhulqaa'dah (Mfungo pili)
12.Dhul-Hijjah (Mfungo tatu)
1.Muharram (Mfungo nne)
2.Swafar (Mfungo tano)
3.Rabiiu'l awwal (Mfungo sita)

Hivyo kwa maana hiyo hata Rabiiu' thaani ungeweza kuitwa "mfungo saba" na Rajab ungeweza kuitwa mfungo au "mfunguo 10" kwa kuwa ni mwezi wa 10 tokea kufungua Ramadhani iliyopita na Shaaban kuitwa kama mfungo au "mfunguo 11" kwa kuwa ni mwezi wa 11 tokea kufungua Ramadhani iliyopita.
 
Vipi Mtume wetu Muhammad (s.a.w) atacopy na kupaste ilihali alikuwa hajui kusoma wala kuandika, hiyo nayo ni miujiza iliyo tukuka
 
Kwanini mwezi wa Ramadhan mnauita mwezi wa haki,miezi mingine siyo ya kutenda haki?

Kwanini wakati wa mwezi wa Ramadhan misikiti inajaa lakini sasa hivi ni mitupu?
Je,ni sahihi kuacha dhambi mwezi wa Ramadhan na kuendelea kutenda dhambi miezi mingine?
 
Ungelikuwa haupo kwa ajili ya chuki ningelikujuza zaidi, lakini kwakuwa umejawa chuki, fitina na hasadi haufai hata kuwa mkristo, kwasababu wakristo hawako namna hiyo. Angalia wenzako wanavyojadiliana kwenye comment
 
Ahsante, uisilamu unahimiza kutenda haki na kusimamia haki, hivyo swala la kutenda haki halifungamani na mwezi bali ni muongozo wa dini kwa aujumla. Kwa hivyo ambaye hatendi haki katika miezi mingine huyo bado hajaufahamu uisilamu na bado imani yake ina ukakasi. Swala la kutenda haki halifungamani na mwezi bali ni mfumo mzima wa maisha ya mwanaadamu anatakiwa kuishi kwenye haki.

Misikiti inajaa mwezi huu mtukufu wa ramadhan kwasababu ni mwezi wenye fadhila nyingi, ni mwezi wenye rehema nyingi na pia ni mwezi ambao Mwenyezi MUNGU huacha wazi milango ya toba kwa ajili ya watu kuomba msamaha kutokana na madhambi yao, ndio maana watu wengi hujaa misikitini. Lakini kwa ujumla mwenye kuendelea kutenda dhambi baada ya Ramadhan huyo anachukuliwa kama mtu mwenye kumfanyia mzaha Mwenyezi MUNGU. Hata katika miezi mingine haipaswi muisilamu kutenda madhambi.
 
Asante, nimesoma nakuelewa, nikuongeze swali dogo, nimeona mwezi wa Ramadhan ni mwezi wa 9 na ndio pekee huwa mnafunga, sasa kwanini na hii miezi mingine nayo mmeipa majina ya "mfungo" wakati huwa hamfungi?

hilo neon mfungo halina mahusiano ya dini, ni mazoea ya waswahili tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…