Fahamu tofauti kati ya mizigo(luggage) na kifurushi (parcel) ukisafiri na SGR

Tanzania Railways Corp

Govt Institution
Joined
Mar 23, 2018
Posts
292
Reaction score
690
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa ufafanuzi wa aina gani ya mizigo abiria anayoruhusiwa kusafiri nayo katika mabehewa ya abiria ya SGR.

Akitolea ufafanuzi huo Aprili 12, 2025 katika stesheni ya Magufuli Jijini Dar es Salaam, meneja wa Treni za abiria wa TRC Bw. Ringo Mboma, amebanaisha kuwa mizigo (Luggage) inayoruhusiwa ni mizigo yenye ulazima kwa abiria awapo safarini mfano begi la nguo na kompyuta mpakato yenye uzito unaokubalika kulingana na daraja husika ambazo ni kilo 20 kwa daraja la uchumi na kilo 30 kwa daraja la kifalme ((Royal) na biashara.

Aidha Bw. Mboma ameeleza kuwa kwa sasa TRC kupitia treni za SGR haisafirishi vifurushi (Parcels) kwani treni za abiria hazina behewa maalumu la kusafirishia vifurushi.

Katika hatua nyingine bwana Mboma, ameeleza kuwa TRC imeshapokea mabehewa ya mizigo ya SGR na hivi karibuni itaanza kutoa huduma za usafirishaji wa vifurushi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
 
Attachments

  • dac95085-21e5-4d61-b0cb-6bd8fbcfa173.jpeg
    dac95085-21e5-4d61-b0cb-6bd8fbcfa173.jpeg
    120.2 KB · Views: 50
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa ufafanuzi wa aina gani ya mizigo abiria anayoruhusiwa kusafiri nayo katika mabehewa ya abiria ya SGR.

Akitolea ufafanuzi huo Aprili 12, 2025 katika stesheni ya Magufuli Jijini Dar es Salaam, meneja wa Treni za abiria wa TRC Bw. Ringo Mboma, amebanaisha kuwa mizigo (Luggage) inayoruhusiwa ni mizigo yenye ulazima kwa abiria awapo safarini mfano begi la nguo na kompyuta mpakato yenye uzito unaokubalika kulingana na daraja husika ambazo ni kilo 20 kwa daraja la uchumi na kilo 30 kwa daraja la kifalme ((Royal) na biashara.

Aidha Bw. Mboma ameeleza kuwa kwa sasa TRC kupitia treni za SGR haisafirishi vifurushi (Parcels) kwani treni za abiria hazina behewa maalumu la kusafirishia vifurushi.

Katika hatua nyingine bwana Mboma, ameeleza kuwa TRC imeshapokea mabehewa ya mizigo ya SGR na hivi karibuni itaanza kutoa huduma za usafirishaji wa vifurushi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.
Naombeni kazi ya kufagia kwenye mabehewa, naweza kuokota pesa Tanzania Railways Corp
 
Back
Top Bottom