Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Hapa nitaelezea Sababu za msingi zinazosababisha majengo yanayofanana kujengwa kwa gharama tofauti.

Tuzungumzie mchoro wa nyumba ya vyumba vitatu vya Kulala kimoja kati ya hivyo ni master bedroom, sitting room, dining, kitchen ,public toilet na store.
Mchoro aliununua ndugu anaitwa Juma, baada ya Juma kununua Alitoa copy akawapa majirani zake wawili Hasani na John.

Hawa wote walijengewa na fundi mmoja ambae ni mimi. Lkn Kila mtu kutumia gharama tofauti kusimamisha boma.

SABABU ZA MSINGI ZA KUFANYA GHARAMA ZA UJENZI ZITOFAUTIANE :

1. location
2. Uimara
3.land type. (slop au tambalale)
4.soil type
5.nyakati.

HAPA NITAZUNGUMZIA UIMARA
Msingi wa nyumba imara utajengwa Kama ifuatavyo.
. Utachimbwa kwenda chini urefu WA mita moja au zaidi.
. Utaanza na zege yenye ratio nzuri kabla ya kujenga tofali
.Utajengwa kwa tofali imara
.Utawekewa Beam yenye kusukwa nondo na ratio nzuri
.Utamwagiliwa maji ya kutosha.
ILI HAYA YOTE YAFANYIKE LAZIMA UMPATE FUNDI MZURI.

Juma aliomba nyumba yake nimjengee kwa viwango hivyo, ndio maana nilitumia tofali nyingi,cement nyingi, nondo nyingi, mchanga mwingi, kokoto nyingi, ring za kutosha, maji mengi nk. Ktk kujenga msingi.

John alisema uwezo wake mdogo , yeye alihitaji tuchimbe futi moja kwenda chini baada ya hapo tujenge tofali, hakuishia hapo pia alisema tusiweke Beam.

Kilichotekea ni utofauti wa Tshs zaidi ya million nne kati ya hiyo misingi miwili.

Kiufupi Juma alitumia 6mil
John Tshs 2.8mil
Hasani Tshs 4mil.

Kilichotofautisha ni uimara WA kujenga msingi. Hawa wote ni majirani.

Mpaka tunamaliza boma Juma alitumia 18m
John 7m
Hasani 12m.
Nyumba zote hizi zikipigwa rangi vizuri hutoweza kujua madhaifu ya awali mpaka pale utakapoanza kuona nyufa (expansion joint)

Hoja yangu hapa ni kwamba unapotokea mjadala wa gharama za ujenzi LAZIMA tuzingatie vitu mhimu vinavyosababisha gharama kuwa kubwa au ndogo.

Ushauri.
1.Tusipende kukimbilia kununua nyumba wakati hujui ilijengwa kwa viwango vipi.
2.Jenga nyumba imara ogopa vya Bei cheee
3.Nyumba kuijenga si lelemama, ili kumudu anza mdogomdogo. Ukiwa na 5m anza hata msingi.

Ukihitaji fundi, usisite kunitafuta, Hakina utaenjoy service yangu.
0655173113


UPDATES
tuendelee na mjadala wetu. Hapo awali tulijadili jinsi namna gani uimara wa nyumba unavyoathiri gharama za ujenzi. Leo tujadili namna location inavyoathiri gharama za ujenzi.

NAMNA LOCATION INAVYOSABABISHA GHARAMA ZA UJENZI KUWA TOFAUTI.

Mungu aliumba ardhi ktk mionekano tofauti. Kuna tambalale, milima na mabonde.
Ujenzi ktk Eneo tambalale unagharama nafuu kulinganisha na Eneo lenye slope . Lakini pia ujenzi wa Eneo tambalale lililoko Chanika mkoni DSM Unaweza kuwa na gharama tofauti na ujenzi wa Eneo tambalale lililoko msasani mkoani DSM. Hivyo hivyo ujenzi wa DSM unagharama kubwa kuliko ujenzi wa Mbeya.

SABABU ZA KUTOFAUTISHA GHARAMA KATI YA ENEO TAMBALALE NA LENYE SLOP.

sanasana hapa kimbembe huwa ktk kujenga msingi wa nyumba.

Msingi uliotumia tofali 1500 katika eneo tambalale, msingi huohuo ukitaka kuujenga ktk eneo lenye slope unaweza kutumia tofali 2300 au zaidi kulingana na ukali wa slope.
Tukumbuke kwamba Kwa kadri tofali zinavyoongezeka ndivyo na material mengine yanavyozidi kuongezeka kitu ambacho hupelekea kuongezeka kwa gharama za fundi. Si ajabu kumalizia 10mil ktk msingi wa nyumba ya Vyumba vitatu ktk Eneo LA slope.

Hivyo basi kama hutaki kutumia gharama kubwa kwenye ujenzi epuka kununua viwanja vilivyo na slope.

Jambo lingine linaloathiri ktk location ni upatikanaji wa material.
Mfano mtu anaejenga mbezi beach atanunua tani 18 Za mchanga zaidi ya 450.000 Tshs wakati mtu wa Chanika atanunua Kwa 220,000tshs.

Pia boma utakalojenga kwa 8mil Mbeya, DSM utalijenga Kwa zaidi ya 15mil. Sababu Mbeya tofali ni cheap, labour ni cheap nk.

Kwa ujenzi imara na wakisasa tutafutane 0655173113
Sijakuelewa ,NYUFA(expansion joint.)
-una maana gani??
 
Sijakuelewa ,NYUFA(expansion joint.)
-una maana gani??
Nyufa ni Cracks kama kawaida, expansion joint ni uwazi unaowekwa wakati wa ujenzi kwa ajili ya kuzuia nyufa za kawaida au kuruhusu mtanuko na mbonyeo kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, pia kuzuia nyufa kutokana na mdidimio(settlement)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, elezea ujengaji wa msingi kwa kutumia steps. Maeneo mengi hasa yenye miinuko mafundi wanaweka steps kwenye foundation, hilo hufanya idadi ya matofali ipungue sana, maana kwa eneo kama Kimara hadi Mbezi, Malamba huko maeneo mengi ni ya miinuko.

1. Je, ujenzi wa steps kwenye miinuko una madhara gani katika uimara wa nyumba?

2. Wakati wa kumwaga ground beam, sijawahi kuona fundi akifanya kupima level ya beam, kwa maana ya upande mmoja kuwa sawa na mwingine, hii husababisha beam isiwe level na mwisho nyumba ikatitia kidogo lazima nyufa ndogondogo zitokee. Kwa nini hamfanyi kupima level ili kuwe na ulinganifu kwenye beam?
Unaweza pata level kwa kutumia mpira wa maji (water level method).mafundi wengi wanaharibu kazi zao kwa kutojua njiia hii rahisi.
 
Mleta mada nakupongeza kwa kuipenda kazi yako. Ila nakuomba pia uwe unatumia ushauri wa wataalamu wa ujenzi. Namaanisha uchote maarifa kwa Architects, Engineer na Quantity Surveyor. Mie nimesoma ujenzi na nimepitia maelezo yako naona kama hayajajitosheleza pengine ni kutokana na ufahamu wa kitaalamu. Kwa mfano, nyumba sio lazima iwe na ground beam, kuna sababu hupelekea iwepo au isiwepo.kwa hiyo wakati mwingine mnaongezea gharama za ujenzi zisizokuwa za lazima kwa kigezo/kauli mbiu ya nyumba imara

Sent using Jamii Forums mobile app
Anahitaji kozi za ujenzi atakuwa vizuri zaidi.vitu kama leveling na kutumia theodolite (kwaajili ya setting )zitaongenza ujuzi wako sana .usiogope bei kuna mpaka used kwenye amazon na e-bay.but mtafute elimu zaidi utatisha sana
 
Unaweza pata level kwa kutumia mpira wa maji (water level method).mafundi wengi wanaharibu kazi zao kwa kutojua njiia hii rahisi.
Hii kitu naona mafundi wameshaachana nayo mda sana, niliona jamaa mmoja akifitisha geti ndio alikuwa anatumia sana kuweka level, na ni very precise!!!
 
Hii kitu naona mafundi wameshaachana nayo mda sana, niliona jamaa mmoja akifitisha geti ndio alikuwa anatumia sana kuweka level, na ni very precise!!!
Mkuu ukikosa darubini basi itabidi utumie pipe level. Huwezi Jenga nyumba bila kuilevel. Siamini kwamba kuna fundi anaeweza fanya upuuzi huo.
 
Anahitaji kozi za ujenzi atakuwa vizuri zaidi.vitu kama leveling na kutumia theodolite (kwaajili ya setting )zitaongenza ujuzi wako sana .usiogope bei kuna mpaka used kwenye amazon na e-bay.but mtafute elimu zaidi utatisha sana
👏👏👏 si unajua elimu haina mwisho Mkuu. Ila darubini tunatumia sana.
 
👏👏👏 si unajua elimu haina mwisho Mkuu. Ila darubini tunatumia sana.
safi sana mafundi wengi hawataki kujiongeza,ukimwambia weka timanzi anakwambia timanzi ni kwa wanafunzi.but naona utafika mbali kwani watu wanawaepuka big contractors sabababu ya gharama,wewe ukiujua udhaifu huo utakimbia kazi.kila la kheri!!!!
 
Back
Top Bottom