Fahamu vitu vinavyotofautisha gharama za ujenzi kwenye majengo yenye kufanana mchoro

Mkuu interlocking blocks ndiyo zikoje ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Interlocking ata mimi nimezifikiria maana ata cost ya kupaka rangi unaiondoa ila naonaga kama zinapooza sana kimwonekano. Hivi huwezi mtu uka mix baadhi ya kuta zikawa interlocking na nyengine ziwe blocks za kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu interlocking blocks ndiyo zikoje ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hizi ni aina ya tofali zinatengenezwa kwa kuchanganya soil and cement,ziko katika muundo unaozipa uwezo wa kuvaana(interlock) hivyo upangaji wake wakati wa ujenzi utumia mortar(cement and cement) bila kiathiri uimara wa joint zake.

Zimetumika maeneo mengi kwa mfano katika ujenzi wa nyumba za makazi na shule.Pia unaweza zitumia katika ujenzi wa ghorofa inayoshikiliwa na nguzo& beam za zege.

Uzoefu umethibitisha kuwa zinagunguza gharama za ujenzi kwa kiasi kikubwa.Angalia picha hizo kwa muonekano wake katika ujenzi


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kuuliza uwiano wa rangi na maji ktk uchanganyaji wa gympsum kwa ajili ya skimming ya ukuta

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Kipindi gani kinafaa kuchimba msingi wa nyumba, Msimu wa Mvua au Kiangazi?
 
Kipindi chochote kinafaa, cha msingi nikufahamu tabia za udongo
Sawa sawa. Kuna ile dhana kwamba msimu wa mvua hasa masika sio kipindi kizuri cha kuchimba msingi wa Nyumba. Nadhani ni mafundi tuu wanakuwa wanakwepa kuchota maji kwenye msingi endapo utajaa maji. Ile kimtazamo ni muda mzuri maana hutahitaji kumwaga maji na pia cement itakauka taratibu na kuwa imara zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kutofautiana na wewe kidogo ktk suala la kusema kwamba mafundi wote ni wazembe kwa upande wa kuset vyoo&wiring,mimi fundi wangu alimwaga zege vyooni na bafuni ila akabakiza nafasi za kuweka vyoo na kitolea maji machafu bafuni alipokuja mtaalam wa choo baada ya kuviweka akamalizia yeye kuziba pengo la zege lililobaki.

Wiring na mfumo wa maji machafu ya jikoni hakuna namna utafanya ili usitindue kuta shida itakuja pale unapookota mafundi uchwara mtaani wanakuja wanatindua kuta wanalaza mabomba na wire kisha wasizizibe na mchanga ili kumrahisishia fundi plaster kufanya kazi yake kwa ufanisi hapa lazima utaona wote wanafanana akili ila siyo hivyo.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…