Al Watani
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 21,237
- 31,811
Mkuu interlocking blocks ndiyo zikoje ?Hongera kwa elimu uliyoitoa kuhusiana na baadhi ya mambo ya msingi kuhusu ujenzi.Asilimia kubwa ya watu wanaogopa kuanza ujenzi moja ya sababu ikiwa ni kukosa uelewa kuhusu mchakato mzima wa ujenzi.
Mbali ya elimu ya darasani,elimu itokanayo na uzoefu kazini ni muhimu sana jambo ninaloliona kwako. Japo baadhi wameonekana kukushambulia ila kwa mtazamo wangu uzoefu ulionao ni muhimu sana hasa hasa katika fani ya ujenzi.
Ushauri wangu kwako ni kuendelea kujielimisha kwani kutokana ukuaji wa teknolojia zipo mbinu mpya za ujenzi zenye kupunguza gharama za ujenzi.
Ushauri wangu kwa wanaotarajia kujenga na wataalam wa ujenzi, wasifanye mambo kwa mazoea kwani zipo style nyingi za ujenzi zenye kutumia gharama ndogo kwa mfano matumizi ya interlocking block,semi prefabricated slab(hii ni aina mpya ya ujenzi wa slab(jamvi) yenye kutumia nondo kidogo na zege kidogo bila kuathiri ubora).
Pia ningependa kushauri wengi wetu tujenge tabia ya kuwatumia watalaamu katika hatua za mwanzo kabla ya kuanza ujenzi. Tumia wataalam kupata ushauri na wakuandalie ramani kulingana na mahitaji yako kwani hii inaweza kukusaidia kupunguza gharama zinazoweza kujitokeza baadae.
Mwisho kabisa kwako fundi naomba unieleweshe tiles nzuri zenye ubora ni zipi? Bei yake ikoje? Na katika box moja zinakuwa tiles ngapi na size gani?
Ahsante.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app