Fahamu zaidi kuhusu kinga ya Ukimwi iitwayo PEP

Fahamu zaidi kuhusu kinga ya Ukimwi iitwayo PEP

Ulipima ukakutwa una maambukizi ndo ukaenda kutumia hizo dawa au ulitumia dawa kwa hisia tu?.
 
Hii habari isikie tu isikukute, sidhani kama kuna mtu atatumia hizi dawa akawa salama na akarudia kufanya ngono uzembe, ni mateso yasiyomithilika, mwezi ni mdogo sana kama unadaiwa lakini ukitumia hizi dawa mwezi ni Kama mwaka, kuna mtu anatarajia kwenda kupima kesho baada ya kumaliza dozi.
 
Ulipima ukakutwa una maambukizi ndo ukaenda kutumia hizo dawa au ulitumia dawa kwa hisia tu?.
Nilitembea na huyo mwanamke kisha tukaenda kupima,ndio akagundulika kuwa ana HIV positive, mm nilikuwa negative, nikaenda Angaza nikapima SKU hiyhiyo ndipo nilipopewa dawa hizo!
 
Hii habari isikie tu isikukute, sidhani kama kuna mtu akatumia hizi dawa akawa salama na akarudia kufanya ngono uzembe, ni mateso yasiyomithilika, mwezi ni mdogo sana kama unadaiwa lakini ukitumia hizi dawa mwezi ni Kama mwaka, kuna mtu anatarajia kwenda kupima kesho baada ya kumaliza dozi.
We acha Tuy! Hizo dawa zinakera mnoo! Zina ndoto za ajabu, njaa inakuuma kama nguruwe na bado ukimeza zina harufu mbaya mno! Mavidonge menyewe n makubwa mno! Aisee n mateso kwa kweli!

ILA NGONO UZEMBE TUACHENI JAMANI!ZINA GHARAMA MNO
 
Hahaaa nimependa hapo, "safari yangu ya kutafta mtoto nje ya ndoa nimeifunga rasmi"
Unajuwa unaweza ukawa hujaandikiwa kupata mtoto Bas kufoc foc nako n kubaya! Its better to stay calm! Nitafanya mpango wa kuwa natembelea vituo vya Watoto yatima ili kumaliza kiu yangu ya Watoto, ila siyo kuzaa nje tena
 
Mtoto muhm ,kukosa na risasi kwenye uwanja wa vita hakugairishi mapambano
 
We acha Tuy! Hizo dawa zinakera mnoo! Zina ndoto za ajabu, njaa inakuuma kama nguruwe na bado ukimeza zina harufu mbaya mno! Mavidonge menyewe n makubwa mno! Aisee n mateso kwa kweli!

ILA NGONO UZEMBE TUACHENI JAMANI!ZINA GHARAMA MNO
Hebu tupia kapicha tuzione mkuu!!
 
HAKIKA MKUU MSHUKURU MUNGU ,,ULITAKA KURUKA JIVU NAKUKANYAGA MOTO

MUNGU AMEKUONYESHA ILO NA SASA KUA MAKINI.

Siku ingime mpimishe au kondomu
 
View attachment 688059

Kama View attachment 688061

Habari zenu wanaJF,

Mwezi mmoja uliopita nilileta uzi kuhusiana na kutembea na binti mwenye VVU,

Lengo kuu la kutembea na huyo binti ilikuwa ni tamaa ya kutaka kupata mtoto hata nje ya ndoa kwani mke wangu hana uwezo wa kupata ujauzito! Nimeishi nae toka 2010 lakini mpaka sasa hajawahi kupata ujauzito.

Tulienda hospital zifuatazo kutaka kupata tiba na suluhisho lakini imeshindikana. Saint Gasper Itigi, Upendo hospital (Dodoma), Agha Khan (Dodoma), General hospital (Dodoma), CF (Mwanza), Kamanga (Mwanza), Sekuture (Mwanza), Bugando (Mwanza) kwa Dkt Mwaka ( mtaalamu wa tiba mbadala- Ilala Bungoni)

Huko kote sio tu alikuwa anapatiwa peke ake matibabu, lah hasha hata mimi nilikuwa napimwa sperm analysis, nakuonekana niko poa.

Kisa cha mke wangu kutopata ujauzito ndio kilichonipelekea kutoka nje ya ndoa.

Mara baada ya kutembea na huyu mdada niliamua kwenda kumpima ili tuanze rasmi safari ya kutafuta mtoto tukiwa tunajiamini sote.

Tulipoenda maabara, huyu binti aligundulika kuwa +, sikuamini, nikamchukua kwenda maabara nyingine, majibu yalikuwa yale yale tu yaani she was HIV positive.

Immediately nikaamua kwenda Angaza, nikapewa hizo (PEP) nikaambiwa nizitumie mwezi mzima kisha nipime tena baada ya kumaliza hiyo dozi.

Kiukweli dawa hizi zinamaudhi sana mwanzoni, ndoto za ajabu, njaa kuumua kupita kiasi na kichefuchefu.

Doz hiyo nimemaliza juzi, so nilikuwa najishauri kwenda kupima huku moyo mwingine ukisita lakini nikaamua bora niende tu liwalo na liwe, maana hakuna kitachobadilika kama nitakuwa nimeathirika ni bora nijijue mapema tu! Basi bwana, nikaenda maabara, nimepimwa na kukutwa mzima (negative), hakika sikuamini ilibidi nimwelezee huyo aliyenipima situation ilivyokuwa, akasema hiyo inawezekana ukatembea na mwenye HIV kama kutakuwa na maandilizi ya kutosha na kusitokee mchubuko basi ni nadra zana kuambukizwa kwa mtu aliye negative.

Napenda kumshukuru mungu kwa kuniepusha na hili janga, na safari yangu ya kutafuta mtoto nje ya ndoa, nimeifuta rasmi.

Najua nawachosha lakini hiyo ndio hali halisi.

Hapa chini ni kopo la hizo dawa na majibu yangu, Mara baada ya kupima Leo.

Onyo! UKIMWI HAUJARIBIWI!KONDOM NI MUHIMU SANA!
Futa rasmi mkuu,usirudie tena,naona sasa umeona wanaoupata hali inavyokuwa...
 
Wasiwasi wako tu,
endelea kutafuta mtoto
ukimwi hata kama upo sio tishio kivile,una miaka 28,ukiupata leo utaanza kuchoka miaka 30 ijayo,si tayari hata kama sio ukimwi safari ya kwenda mbinguni huwa ishaanza.

Huyo uliempima sijui yuko positive,anaweza kuku outlive ndo ubaki unashangaa.
 
Nilitembea na huyo mwanamke kisha tukaenda kupima,ndio akagundulika kuwa ana HIV positive, mm nilikuwa negative, nikaenda Angaza nikapima SKU hiyhiyo ndipo nilipopewa dawa hizo!
Kama unahitaji mtoto njoo Uganda , upandikize kwa technology inayoitwa IVF, manii yanatolewa na kupandikizwa kwenye kizazi cha mkeo na anabeba mwanao
 
Kama unahitaji mtoto njoo Uganda , upandikize kwa technology inayoitwa IVF, manii yanatolewa na kupandikizwa kwenye kizazi cha mkeo na anabeba mwanao
Hata Muhimbili nadhani hiyo technology IPO, specialist mmoja kutoka kamanga hospital àliniambia! Ila sijafikiria kutumia iyo
 
Wasiwasi wako tu,
endelea kutafuta mtoto
ukimwi hata kama upo sio tishio kivile,una miaka 28,ukiupata leo utaanza kuchoka miaka 30 ijayo,si tayari hata kama sio ukimwi safari ya kwenda mbinguni huwa ishaanza.

Huyo uliempima sijui yuko positive,anaweza kuku outlive ndo ubaki unashangaa.
We Tania tu!
 
Back
Top Bottom