View attachment 688059
Kama
View attachment 688061
Habari zenu wanaJF,
Mwezi mmoja uliopita nilileta uzi kuhusiana na kutembea na binti mwenye VVU,
Lengo kuu la kutembea na huyo binti ilikuwa ni tamaa ya kutaka kupata mtoto hata nje ya ndoa kwani mke wangu hana uwezo wa kupata ujauzito! Nimeishi nae toka 2010 lakini mpaka sasa hajawahi kupata ujauzito.
Tulienda hospital zifuatazo kutaka kupata tiba na suluhisho lakini imeshindikana. Saint Gasper Itigi, Upendo hospital (Dodoma), Agha Khan (Dodoma), General hospital (Dodoma), CF (Mwanza), Kamanga (Mwanza), Sekuture (Mwanza), Bugando (Mwanza) kwa Dkt Mwaka ( mtaalamu wa tiba mbadala- Ilala Bungoni)
Huko kote sio tu alikuwa anapatiwa peke ake matibabu, lah hasha hata mimi nilikuwa napimwa sperm analysis, nakuonekana niko poa.
Kisa cha mke wangu kutopata ujauzito ndio kilichonipelekea kutoka nje ya ndoa.
Mara baada ya kutembea na huyu mdada niliamua kwenda kumpima ili tuanze rasmi safari ya kutafuta mtoto tukiwa tunajiamini sote.
Tulipoenda maabara, huyu binti aligundulika kuwa +, sikuamini, nikamchukua kwenda maabara nyingine, majibu yalikuwa yale yale tu yaani she was HIV positive.
Immediately nikaamua kwenda Angaza, nikapewa hizo (PEP) nikaambiwa nizitumie mwezi mzima kisha nipime tena baada ya kumaliza hiyo dozi.
Kiukweli dawa hizi zinamaudhi sana mwanzoni, ndoto za ajabu, njaa kuumua kupita kiasi na kichefuchefu.
Doz hiyo nimemaliza juzi, so nilikuwa najishauri kwenda kupima huku moyo mwingine ukisita lakini nikaamua bora niende tu liwalo na liwe, maana hakuna kitachobadilika kama nitakuwa nimeathirika ni bora nijijue mapema tu! Basi bwana, nikaenda maabara, nimepimwa na kukutwa mzima (negative), hakika sikuamini ilibidi nimwelezee huyo aliyenipima situation ilivyokuwa, akasema hiyo inawezekana ukatembea na mwenye HIV kama kutakuwa na maandilizi ya kutosha na kusitokee mchubuko basi ni nadra zana kuambukizwa kwa mtu aliye negative.
Napenda kumshukuru mungu kwa kuniepusha na hili janga, na safari yangu ya kutafuta mtoto nje ya ndoa, nimeifuta rasmi.
Najua nawachosha lakini hiyo ndio hali halisi.
Hapa chini ni kopo la hizo dawa na majibu yangu, Mara baada ya kupima Leo.
Onyo! UKIMWI HAUJARIBIWI!KONDOM NI MUHIMU SANA!