Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Utapeli wake uko wapi?

Ana mwaka wa tatu akiendesha mradi wake kwa mfumo huohuo, je ana rekodi ya kumtapeli mtu yeyote?

Uwekezaji ni lazika uwe wa kampuni za soda, beer au na bank? Kwamba uwezekaji kwenye ufugaji sio sahihi?

Je, kampuni kubwa ambazo watu wanawekeza huwa hazifilisiki?

Huyu bwana angehukumiwa kwa matumizi ya pesa za wawekezaji na sio kuweka general comments kwamba ni tapeli bila kueleza utapeli wake. Mbona hii mifumo inafanyika hata kwenye vikundi vyetu (formal na informal). Tunachangishana pesa na kuwekeza kwenye kilimo na miradi mingine kisha tunagawana faida.

Je, pesa anayokusanya anaiwekeza kwenye miradi inayohusiana na kuku au hakuna biashara yoyote ya Kuku na anafanya PONZI SCHEME?

Huyu bwana hayuko Ulaya, yuko Kigamboni na ana ofisi plus mashamba ya kuku, YENYE KUKU. Kabla hujaharibu biashara na miradi ya watu mtandaoni uende kwaza ukajiridhishe. GNLD na FOREVER LIVING nao walitukanwa sana kwamba wanafanya utapeli lakini mpaka leo wapo wanapiga mzigo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii bei ni bei elekezi kwa mikuku yote hiyo isiyowika.
Hakuna cha competitive price hapo.
Labda angekuwa anauza 4,500.
 
Hoja kama hizi utawadanganya nazo hao wajinga wajinga wanaowaletea ninyi fedha zao na siyo mimi! Maisha yangekuwa rahisi namna hii mnayodanganya hii dunia isingekuwa na maskini. Ni suala la muda tu lakini ukweli utajulikana na wajinga wanaowapa fedha zao watabaki wanalia na kuomboleza.
 
Tumia akili, usiwe mjinga.
Jifunze, elewa ndio ukosoe. Tatizo lenu wajuaji wa JF huwa mnakimbilia kukosoa kabla hata ya kuelewa. Ni ujinga!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia akili, usiwe mjinga.
Jifunze, elewa ndio ukosoe. Tatizo lenu wajuaji wa JF huwa mnakimbilia kukosoa kabla hata ya kuelewa. Ni ujinga!

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea kinyume. Hapa unaniambie niwe mjinga ili unitapeli. Nimekumbia mtawapata hao hao wajinga wapenda vya mtelemko lakini siyo mimi. Mnakotaka kulalia ndiko nilikoamkia. Nina uhakika wa 100% ni suala la muda tu lakini watu mtaliza watu. Nimekuwa karibu na wafugaji kuku wa grade ya juu na wenye mtaji mkubwa kuliko huu mnaotapeli watu na sijaona mfugaji analipata faida kama hii mnayoahidi hapa.
 
na wanaoingiza hela kwa kununua hisa za makampuni makubwa km amazon na Facebook wanaingiza hela wakiwa wanafanyeje?

Mkuu umeelewa mfumo wa Mr Kuku lakini...!!?? Ni weka hela,, upate Hela. No any calculation, No any risk... Yaani Mfano ukiweka Laki na Nusu lazima upate Laki tatu. haijalishi biashara itaenda vipi...

Hakuna investiment isiyokuwa na Risk Mkuu,,,
Thank me later
 
Nimegundua kitu very simple logic...
Kwa kawaida Broilers wanakuwa kwa wiki 5 ambazo ni sawa na siku 35, sasa unaambiwa wekeza halafu unalipwa baada ya siku 180, Je simple mathematics katika 180 kuna 35 ngapi? Regardless ya cost atakayotumia katika kuwafuga, kuwatunza broilers hakosi faida nono .... Submitting.
 
Hii logic inaweza kuwa sawa ama isiwe sawa je hawa kukua anawauza kwenye soko gani na je umeshaajiuliza yeye atapata wapi pesa za kuwalipa watu endapo lets say watu ml5 wakiamua kujiunga kwa kila siku let say watu laki mbili mbili ataweza kupata wapi iyo pesa ya kuwalipa double times hawa watu laki mbili lets wote hawa laki mbili mbili kila mmoja amewekeza may be ml2 mbili mbili je unajua ni sh ngap jamaa atatakiwa kuwa nayo kwa kila siku ili awalipe hawa watu? Je ni kweli hii kampuni inauwezo wa kufanya production yenye uwezo wa kutengeneza iyo pesa per day na bado yeye akabaki na faida plus production cost nayo ikabaki alafu akalipa hawa watu kila siku?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Zinafilisika stock markets uje kuwa kuku!

Hakuna uwekezaji audio na risk. The higher the risk the higher the return.

Kama umeamua kiwekeza popote na chochote jua uwezekano wa kupata na kukosa ni 50/50.

Ni kwamba kwenye kuwekeza kuna 50% chance ya kupata faida na 50% chance ya kupata hasara.
 
Poleni sana mliopata majanga, mpaka serikali inaingilia kati kuna namna
 
Kwa kweli ukubwa wa faida anaounadi ndio unaostua
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Utapeli unafanisha ni stock markets? You are kidding me! Tusitaniane ndugu. Nasema hivi: Huo mradi wa kuku ni utapeli kwa asilimia zote na hakuna namna utafanikiwa. Narudia tena: Ni utapeli na hakuna namna yoyote kuwa utafanikiwa. Waibieni hao hao mazezeta wapenda mteremko lakini watu wenye akili zao hamuwapati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…