Utapeli wake uko wapi?
Ana mwaka wa tatu akiendesha mradi wake kwa mfumo huohuo, je ana rekodi ya kumtapeli mtu yeyote?
Uwekezaji ni lazika uwe wa kampuni za soda, beer au na bank? Kwamba uwezekaji kwenye ufugaji sio sahihi?
Je, kampuni kubwa ambazo watu wanawekeza huwa hazifilisiki?
Huyu bwana angehukumiwa kwa matumizi ya pesa za wawekezaji na sio kuweka general comments kwamba ni tapeli bila kueleza utapeli wake. Mbona hii mifumo inafanyika hata kwenye vikundi vyetu (formal na informal). Tunachangishana pesa na kuwekeza kwenye kilimo na miradi mingine kisha tunagawana faida.
Je, pesa anayokusanya anaiwekeza kwenye miradi inayohusiana na kuku au hakuna biashara yoyote ya Kuku na anafanya PONZI SCHEME?
Huyu bwana hayuko Ulaya, yuko Kigamboni na ana ofisi plus mashamba ya kuku, YENYE KUKU. Kabla hujaharibu biashara na miradi ya watu mtandaoni uende kwaza ukajiridhishe. GNLD na FOREVER LIVING nao walitukanwa sana kwamba wanafanya utapeli lakini mpaka leo wapo wanapiga mzigo.
Sent using
Jamii Forums mobile app