Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

Naona jamaa wamemtia nyavuni tayari
 
Hili liwe fundisho tuache umero wa kupenda pesa za kufanyiwa kqzi
 
Muwe mnafuatilia mambo kabla ya kutuhumu watu. Je, mnaamini watu wote walio Segerea kwa Money Laundering ni kweli wametakatisha pesa?

Nendeni Kigamboni Kisarawe 2 karibu na kiwanda cha Maji (Afya) muone mabanda makubwa sana ya kufugia Kuku tena yapo 14 na mlima wa Mbolea ya kuku. Walikua wanafuga Kuku mpaka laki 2 kwa mpigo kutokana na pesa za wawekezaji. Nenda kaulize hata majirani kama hakukua na mradi wa ufugaji uliokua ukiendelea. UPATU unatokea wapi hapo?

Huyo Wankyo Simon ndio kiboko ya kesi za Money laundering. Wanatafuta tu sababu ya kutaifisha hizo Bilioni17 za wananchi.

Kama kweli huu ni Upatu, mbona kuna miradi mingine kama hio mitatu nayoifahamu bado inaendelea na watu wanawekeza huko?

CHEMA - Unawekeza hela kisha baada ya miezi mitano unarudishiwa 60% ya pesa ulowekeza

WEKU - Picha inajieleza

JATU - Hawa wana wanachama zaidi ya 2000 na viongozi wa Serikali hadi Waziri Manyanya kashahudhuria mikutano yao. Unawekeza 1/3, wanakukopesha 2/3 na kukulimia Mahindi, Maharage, Mpunga n.k na baada ya mavuno wanakurudishia 1/3 yako plus faida yote ya mauzo ya mavuno yatokanayo na 3/3 ya mtaji.

Acheni ushamba, kilimo kina faida kikifanywa kitaalamu. Huyo Tariq wa Mr Kuku amesoma SUA na aliajiri maafisa Kilimo waliokua full time pale Shambani. Anachukua pesa yako na kuizungusha kwa faida mara NNE kabla ya kukurudishia 70% ya faida. Broiler anakuzwa kwa mwezi MMOJA tu na kuuzwa, maajabu yako wapi hapo?

Hii ni dhulma tu, hamna maelezo tofauti.

Hio Bilioni 17 imewatoa watu fulani mate.
 
Kuna Jamaa Yangu Nilimwambia Ni Kekundu
 
Kweli ukiwa mjanja umaskini unaaga mwaka tu ebu fikiria 17B chap tu ya wapenda vitonga
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Anasema Kila Siku Tanzania Ni Tajiri

Billions 17 Haraka
 
Na imekuwa kama ulivyonena! Heheh ...wanakolalia ndiko ulikoamkia...lo bravo mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…