Muwe mnafuatilia mambo kabla ya kutuhumu watu. Je, mnaamini watu wote walio Segerea kwa Money Laundering ni kweli wametakatisha pesa?
Nendeni Kigamboni Kisarawe 2 karibu na kiwanda cha Maji (Afya) muone mabanda makubwa sana ya kufugia Kuku tena yapo 14 na mlima wa Mbolea ya kuku. Walikua wanafuga Kuku mpaka laki 2 kwa mpigo kutokana na pesa za wawekezaji. Nenda kaulize hata majirani kama hakukua na mradi wa ufugaji uliokua ukiendelea. UPATU unatokea wapi hapo?
Huyo Wankyo Simon ndio kiboko ya kesi za Money laundering. Wanatafuta tu sababu ya kutaifisha hizo Bilioni17 za wananchi.
Kama kweli huu ni Upatu, mbona kuna miradi mingine kama hio mitatu nayoifahamu bado inaendelea na watu wanawekeza huko?
CHEMA - Unawekeza hela kisha baada ya miezi mitano unarudishiwa 60% ya pesa ulowekeza
WEKU - Picha inajieleza
JATU - Hawa wana wanachama zaidi ya 2000 na viongozi wa Serikali hadi Waziri Manyanya kashahudhuria mikutano yao. Unawekeza 1/3, wanakukopesha 2/3 na kukulimia Mahindi, Maharage, Mpunga n.k na baada ya mavuno wanakurudishia 1/3 yako plus faida yote ya mauzo ya mavuno yatokanayo na 3/3 ya mtaji.
Acheni ushamba, kilimo kina faida kikifanywa kitaalamu. Huyo Tariq wa Mr Kuku amesoma SUA na aliajiri maafisa Kilimo waliokua full time pale Shambani. Anachukua pesa yako na kuizungusha kwa faida mara NNE kabla ya kukurudishia 70% ya faida. Broiler anakuzwa kwa mwezi MMOJA tu na kuuzwa, maajabu yako wapi hapo?
Hii ni dhulma tu, hamna maelezo tofauti.
Hio Bilioni 17 imewatoa watu fulani mate.