SoC01 Faida atakayopata kijana baada ya kuoa

Stories of Change - 2021 Competition

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Pamoja na uwepo wa utitiri wa ndoa sasa lakini bado katika ulimwengu wa sasa kuna vijana wanaogopa kuoa.

Kwanza kijana acha uoga kila kijana akiamua anaweza kuoa na kumudu familia hata kama ana kipato kidogo tu. Nina miaka miwili ndani ya ndoa na hizi ni faida nilizopata.

MATUMIZI BORA YA FEDHA.
Kabla sijaoa ni rahisi sana kutumia pesa bila mpangilio mzuri, unaweza kwenda baa ukagawa 🍻 na ofa mbalimbali,kula kula hovyo sababu nyumbani hakuna chakula lakini ukiwa na mke huwezi kufanya mbele yake hata kidogo.

Unaweza kutumia pesa nyingi bila hofu sababu uko na washkaji,ukioa lazma kwanza uwaze familia kwanza ndio marafiki wafuate.

KUSAVE MUDA WAKO WA ZIADA
Kabla hujaoa unaweza ukawa ni mtu wa kujichanganya popote bila ratiba na mwaliko,hutojali sehemu ya kulala au utakapoamkia,lakini ukioa ni lazma ulale nyumbani tu.

ULINZI NA USALAMA WA AFYA YAKO
Hapa kabla hujaoa ulikuwa na tabia labda ya kuruka ruka(kudanga) au kufanya ngono zembe. Hapa kuna hatarisha afya yako kutokana na magonjwa ya zinaa,kulea mimba bandia au mimba zisizotarajiwa.

Ukishaoa kama utamweshimu mwenzio badi yote hayo hutopata, utakuwa unafaidika na mwenzi wako mida wowote na kwa usalama zaidi.

MLO BORA NA MZURI KWA AFYA
Ukiwa bachela unaweza kula vyakula vya hovyo hovyo na hata kama utakula hotelini basi utakula chakula kilichopo na pia gharama itakuwa ni kubwa kuliko ungekula nyumbani.

Ukioa,utachagua chakula unachopenda, garama zitakuwa ndogo,utawekewa matunda na utaulizwa kama umeshiba au la,raha iliyoje?

MSAIDIZI BORA KABISA WA MAISHA
Hapa kumbuka utapikiwa na kuoshewa vyombo,utafuliwa nguo zako vizuri,utashauriwa nguo ya kuvaa,utatizamwa kama umependeza,utafarijiwa ukiwa na mawazo,umechoka,unaumwa n.k

Changamoto za ndoa zipo lakini haziondoi hizo faida. Zoote hizo ni faida je una nyingine ujazie? Au kama bado hujaoa Ukiwa kijana ni kipi kinachokufanya usioe?

Karibuni.
 
Upvote 21
Ndo maana nataka nivute pisi mapema sana nianze kula mema ya nchi
Subir kidogo mkuu. Usitembelee reli ya jamaa tu. Aliyoandika ni sahihi lakin not guaranteed! Jambo moja linalozorotesha kuharakisha ndoa ni hali ya kuitoa ndoa kuwa suala la kijamii na kuwa la binafs. Ndoa ikilindwa kijamii inaweza kuwa imara kuliko mkiilinda wanandoa peke yenu. Yan yaliyosemwa yote yanakuja kufutwa na kitendo kimoja tu cha mwanandoa asiye mwaminifu, asiye na mlengo wako kimalez, asiyetambua tofaut ya ndoa na mapenz! Had unakimbia kwako au kujichelewesha. Au mke analazmishwa kuchepuka! Wazaz warudi kwenye majukum yao kwa watoto wao. Ndoa ni jambo zuri sana kama tutazitii kanun za asili kuliko uhanaharakat, tamaa na ubinafs!
 
ANTI VIRUS 😂😂😂😂 alimaarufu kama pinga pinga FC
 
Muda kwako bado ila ukifika utaoa tu
 
Sasa kwanini unatafuta hela au maisha mazuri?
Kwa sababu napenda maisha mazuri.. Kwani ww haupendi maisha mazuri? Unapenda shida ndugu yangu? Pia napenda kusaidia jamii na pia napenda kusaidia vijana wenzangu kuwapatia kazi nk. Suala la ndoa mnakosea sana kuandika makala kama hii unaonyesha uzuri wa ndoa wakati ina Matatizo Mengi. TENA KWA DUNIA YA LEO.. Matatizo ni makubwa kuliko raha.. wewe haujayasema hayo.

Kama ni ndoa au familia, itakuja tu.. katika muda wake. Kama ndugu alivyosema Marriage is a Big Scam. Tatizo Watu mnashinikiza watu waingie kwenye ndoa. Utadhania mtu asipooa mapema ndio hana maisha tena..

INATAKIWA ITOKEE NATURALLY. Watu wanapambana mchana na usiku kupata mke sababu eti umri umeenda, ndugu wananisukuma. Rafiki zangu wameoa.. anatafuta.... anahangaika.. NA HAPO NDIO KAMA KU-FORCE KITU NA NDIO ANAPATA MTU SIO SAHIHI KWAKE.

Inatakiwa itokee tu na tena iwe na mtu ambaye roho zimetulia kwa kila mmoja. Na wanaendana vizuri tokea awali. Wawe na malengo sawa ya kupambania kitu sawa, pamoja, kwa roho moja, bila kuvutana na kukasirikiana.

NA MTU ASISUKUMWE NA JAMII. Afanye kama yeye.. katika muda wake yeye.. anaoona unafaa kwake yeye. Kama bado ana ndoto za kutimiza, na kama ndoa itamharibia, basi na iwe ivyo. Apambanie ndoto izo sababu ndoa ipo tu.

Pia naona ndoa yako ina miaka miwili tu na sasa umeshakuwa expert wa ndoa.. Be careful my brother, and do not jump the gun.
 
Hii siyo story for change

It’s a mere speculation

Ndoa za siku hizi ha ziko hivi…. Most of them ni total confusion
 
Umeoa mke au umeoa ndugu+mke?
Kwa Tanzania, kama una uwezo na kuna matatizo kwa mkeo, utakaa tu? Usisaidie? Lazima usaidie. Kwa ujumla ndoa inaongeza majukumu ya kifedha kwa asilimia kubwa sana... upende usipende.. hasa kwa jamii zetu hizi za kiafrika
 
acha kuzunguka, faida ya kwanza ni

1. kupata unyumba halali any time ambao unakuwa hutendi dhambi,

2. kuzaa watoto

3. kupata soulmate mwenye commitment ya maisha yote atakayekuwa anakufariji kwenye shida na raha

4. kusaidiana kwenye mipango ya maisha. hivyo tu. vingine vyote ni porojo tu.
 
nakubaliana na wewe kwa 100.0% na atakayekupinga ni mchawi
 
Ungetaja na hasara za ndoa ingekuwa vizuri zaidi, mtu achague mwenyewe kunyoa au kusuka.
NB:
MAISHA HAYANA FOMULA.
Weka uzi hapo utaje hasara,mm naona hasara ni ndogo kuliko faida
 
kila kitu kina sheria zake so ukikiuka sheria lazima adhabu uipate.

note: nina experience ya zaidi ya miaka nane kwenye ndoa na ndoa yangu ni imara sana mpaka sasa na nimeoa damu bado inachemka
Unaijuliaje ndoa? Unaoa mtu amelelewa kwao.. ana tabia zake.. na ni mtu mzima. Hakuna cha kujulia ndoa. Ndoa siku izi ni mvutano sana. Una ndoto za hivi.. yeye ana za hivi.. Hapo ndio utajua hujui.
 
kila kitu kina sheria zake so ukikiuka sheria lazima adhabu uipate.

note: nina experience ya zaidi ya miaka nane kwenye ndoa na ndoa yangu ni imara sana mpaka sasa na nimeoa damu bado inachemka
Huyo ni wale wanaookotana uchochoroni n kwenda kufunga ndoa,badala ya kuchunguzana na kujua kula mmoja ana malengo gani,je yanaendana? Changamoto zipo lakini haimaanishi ndio hasara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…