SoC01 Faida atakayopata kijana baada ya kuoa

Stories of Change - 2021 Competition

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Pamoja na uwepo wa utitiri wa ndoa sasa lakini bado katika ulimwengu wa sasa kuna vijana wanaogopa kuoa.

Kwanza kijana acha uoga kila kijana akiamua anaweza kuoa na kumudu familia hata kama ana kipato kidogo tu. Nina miaka miwili ndani ya ndoa na hizi ni faida nilizopata.

MATUMIZI BORA YA FEDHA.
Kabla sijaoa ni rahisi sana kutumia pesa bila mpangilio mzuri, unaweza kwenda baa ukagawa 🍻 na ofa mbalimbali,kula kula hovyo sababu nyumbani hakuna chakula lakini ukiwa na mke huwezi kufanya mbele yake hata kidogo.

Unaweza kutumia pesa nyingi bila hofu sababu uko na washkaji,ukioa lazma kwanza uwaze familia kwanza ndio marafiki wafuate.

KUSAVE MUDA WAKO WA ZIADA
Kabla hujaoa unaweza ukawa ni mtu wa kujichanganya popote bila ratiba na mwaliko,hutojali sehemu ya kulala au utakapoamkia,lakini ukioa ni lazma ulale nyumbani tu.

ULINZI NA USALAMA WA AFYA YAKO
Hapa kabla hujaoa ulikuwa na tabia labda ya kuruka ruka(kudanga) au kufanya ngono zembe. Hapa kuna hatarisha afya yako kutokana na magonjwa ya zinaa,kulea mimba bandia au mimba zisizotarajiwa.

Ukishaoa kama utamweshimu mwenzio badi yote hayo hutopata, utakuwa unafaidika na mwenzi wako mida wowote na kwa usalama zaidi.

MLO BORA NA MZURI KWA AFYA
Ukiwa bachela unaweza kula vyakula vya hovyo hovyo na hata kama utakula hotelini basi utakula chakula kilichopo na pia gharama itakuwa ni kubwa kuliko ungekula nyumbani.

Ukioa,utachagua chakula unachopenda, garama zitakuwa ndogo,utawekewa matunda na utaulizwa kama umeshiba au la,raha iliyoje?

MSAIDIZI BORA KABISA WA MAISHA
Hapa kumbuka utapikiwa na kuoshewa vyombo,utafuliwa nguo zako vizuri,utashauriwa nguo ya kuvaa,utatizamwa kama umependeza,utafarijiwa ukiwa na mawazo,umechoka,unaumwa n.k

Changamoto za ndoa zipo lakini haziondoi hizo faida. Zoote hizo ni faida je una nyingine ujazie? Au kama bado hujaoa Ukiwa kijana ni kipi kinachokufanya usioe?

Karibuni.
 
Upvote 21
1. Matumizi bora ya fedha.. Labda kama haumhudumii mke wako. Mwanaume ww ndio provider. Kabla haujaoa unajihudumia ww. Ukioa. Unahudumia wawili na watoto wakija.

2. Muda wako wa ziada ukiwa single.. Unautumia kwa mradi wowote kwa ndoto zako. Ukishaoa.. watu wengi ndoto zinakufa sababu sasa inabidi arudi home muda maalumu.. hana uhuru wa muda wake tena..

3. Ulinzi na usalama wa afya. Watu waliooa ni rahisi sana kupata magonjwa ya ngono sababu wanaaminiana. Nina mifano mingi ya mume kamletea mke. Au mke kamletea mume VVU. Ukiwa single.. unakaa kimachale muda wote na haumwamini mtu. NA WATU WALIOOA NA KUOLEWA WANACHEPUKA SANA. Sasa sijui ww unaongelea ndoa gani.. ila sio za hapa Tz. Kuchepuka ni kawaida sana.

4. Mlo bora. WaDada wengi wa leo hata kupika hawajui.

5. Msaidizi.. Binafsi nina wafanyakazi WENGI TU. Na hao wananisaidia kazi zangu za biashara, nyumbani nk. Nawalipa vizuri, na wanafanya kazi vizuri. Sasa ww utapata msaidizi mmoja na tena kama ni MVIVU ndio imekula kwako na hauwezi kumwachisha kazi na Mahari Ulishatoa. Mimi wasaidizi wangu kama ni mvivu au hana uaminifu wa kazi, anapata pink slip.
Mkuu asante umeyasema yote niliyokua nayafikiria.
 
Naqubali [emoji817]
 
Kama mtu wa ovyo ni mtu ambaye Nina Maisha Mazuri sana ya furaha YASIYO NA STRESS.. AMBAPO watu wengi waliooa ninaowafahamu wao wamejaa stress za ndoa na wanakuja kwangu kwa msaada na ushauri wakati mimi hata kuoa sijaoa.. NAKUBALI KABISA KUWA MTU WA OVYO. Nina maisha mazuri mazuri sana. Mmekaririshwa kwamba ni lazima muoe. Mwisho mnalia tu. Na hio jamii iliyowashinikiza muoe MKIPATA SHIDA .. Hamuoni mtu yeyote wa kuwasaidia.. mnakuja kusumbua watu kama sisi tuwasaidie.. Ila kumbe chanzo cha maisha ya furaha ni kutosikiliza watu bali kusimamia furaha yako
usicheze na Ke wewe kijana shukuru Mungu amekusaidia hapo! lkn pia lazima umjaribu kwa kumpa wkt mgumu!.ili ujue ni jembe au kichwa cha panzi....muendekeze kifara lkn ..

siku ukijichanganya akikugeuka ndo utajua kuwa hujui, ke huwa hatu tumii nguvu sisi kuwaumiza endelea kukoroma yeye anasoma mchezo....... kwanza yeye mwenyewe Mungu, ke tuliwahi kumpa changamoto palee Bustanini Eden!!.

akawaagiza me wote muuishi nasi kwa akili alikuwa hatanii.... wewe ni nani? alisha sema kaeni nao kwa akili!!! huyo katumwa usomeshe wanae wafike UNIVER. tena si ajabu watoto si wako, ukisha tia mjengo wa maana..magari..ndo utajua muziki kamili........

leo me mnapigika ajili ya ke''...endelea kucheza na ke! muziki utaujua baadaye kwenye 70 umesha choka!! huyo wkt wa kuvurugana ni sasa mvuruge maksudi tu!! asibweteke uone reaction yake! mpaka avumilie hasa!!

mwanamke/familia kuijenga ni Mungu tu!! akusimamie sana wewe!! na uombe usiku na mchana akunusuru wengi wamekufa na kuparalyse ajili ya mbunye! wanakufa wanawake wana baki jiulize kwa nini??
 
1. Matumizi bora ya fedha.. Labda kama haumhudumii mke wako. Mwanaume ww ndio provider. Kabla haujaoa unajihudumia ww. Ukioa. Unahudumia wawili na watoto wakija.

2. Muda wako wa ziada ukiwa single.. Unautumia kwa mradi wowote kwa ndoto zako. Ukishaoa.. watu wengi ndoto zinakufa sababu sasa inabidi arudi home muda maalumu.. hana uhuru wa muda wake tena..

3. Ulinzi na usalama wa afya. Watu waliooa ni rahisi sana kupata magonjwa ya ngono sababu wanaaminiana. Nina mifano mingi ya mume kamletea mke. Au mke kamletea mume VVU. Ukiwa single.. unakaa kimachale muda wote na haumwamini mtu. NA WATU WALIOOA NA KUOLEWA WANACHEPUKA SANA. Sasa sijui ww unaongelea ndoa gani.. ila sio za hapa Tz. Kuchepuka ni kawaida sana.

4. Mlo bora. WaDada wengi wa leo hata kupika hawajui.

5. Msaidizi.. Binafsi nina wafanyakazi WENGI TU. Na hao wananisaidia kazi zangu za biashara, nyumbani nk. Nawalipa vizuri, na wanafanya kazi vizuri. Sasa ww utapata msaidizi mmoja na tena kama ni MVIVU ndio imekula kwako na hauwezi kumwachisha kazi na Mahari Ulishatoa. Mimi wasaidizi wangu kama ni mvivu au hana uaminifu wa kazi, anapata pink slip.
kamata kinywaji hapo naja kulipa chap
mtoa mada ameongea kinadharia, wewe umeandika kiuhalisia
 
Wapingaji ni wengi sana ktk maswala ya ndoa,na wengi wao ni hao wasiooa.
Mtu bachela kuelewa swala la ndoa ni kazi flan ya ziada akuelew,msingi bora wa mtu bachela kuoa wew mpe mda tu utamfikia siku yake.

Mtu Bachela hana adabu na wala busara hana kwake kila kitu ni kibaya ktk ndoa.

Mtu bachela ni mpinzani mkubwa na mtu ambae ameoa au kuolewa,swala la ndoa kwake ni mfupa mgum usiotafunika.

Mtu bachela kutana nae maskani tu mpige story nasio kwako usimkaribishe, kua nae makin akija kwako anataka kuja kupata mawazo namna gani anaweza kuoa imeisha na urafik wenu upambe hapo.

Kiufupi mtu bachela au muhuni sio mtu mzuri
 
Haya uliyosema hapa ni sawa na kuwambia watu waendele kunywa bia na wasinunue mabati kwa ajili kujenga kwakua yanaweza kuwakata.
Yani wewe ndio zero kabisa sijui umeandika nini ,,kwani wanao kunywa hawajengi na wanao jenga hawanywi...
 
Ndoa ni nzuri tena ni nzuri, nasema hivyo kama shuhuda kwa miaka 6 sasa.
Lakini katika ndoa kuna changamoto nyingi mno mno ambazo kitu pekee kitakachoweza kufanya hiyo ndoa iendelee ni busara na uvumilivu.

Wakati ule sijaoa nilisema wazi kabisa nimekwisha kuvuka viunzi vingi kwenye maisha,badala yake nimekuja kukutana na milima mirefu mno ambayo nisingependa kuiandikia hapa.

Hapo mwanzo nilijua labda ni mimi peke yangu ndio napitia haya labda ni bahati mbaya yangu tu, lakini kumbe ni kilio cha kila alieko kwenye ndoa.

Ukikutana na wenye kua ndoa 10 basi kama sio tisa basi nane wanalia.

Na bahati mbaya nyingine sisi wengine tuko kwenye kifungo cha mke mmoja ndio hakuna rangi ambayo hatuachi kuiona.

Kwa hiyo hakuna furaha ya moja kwa moja ndugu zangu kwenye ndoa msidanganywe, kitu pekee unachotakiwa kuwa nacho kwenye ndoa ni uvumilivu, tena uvumilivu haswa.pia busara na akili kubwa ya kuweza kuishi na mwenzako jamii ukiwaona mnacheka lakini mna kuumia kwa namna moja ama nyingine mioyoni.

Furaha pekee inayoweza kupatikana kwenye ndoa ni watoto, na asante Mungu kwa hilo maana isingekuwa hivyo sijui ingekuwaje.

Huu ni mtazamo wangu kulingana na uzoefu wangu huo mdogo, inaweza kuwa kinyume chake kwa wengine.
Umeandika vizuri ila 95% una maumivu kuliko furaha
 
Kwenye Afya na mlo kamili siyo wote wanakutana na hiyo.

Wapo walioletewa magonjwa wakiwa kwenye ndoa.

Kuna jamaa yangu alioa ka sister duu kakawa "kamshindishia" chapati msukuma yule aka-retreat.
 
1. Matumizi bora ya fedha.. Labda kama haumhudumii mke wako. Mwanaume ww ndio provider. Kabla haujaoa unajihudumia ww. Ukioa. Unahudumia wawili na watoto wakija.

2. Muda wako wa ziada ukiwa single.. Unautumia kwa mradi wowote kwa ndoto zako. Ukishaoa.. watu wengi ndoto zinakufa sababu sasa inabidi arudi home muda maalumu.. hana uhuru wa muda wake tena..

3. Ulinzi na usalama wa afya. Watu waliooa ni rahisi sana kupata magonjwa ya ngono sababu wanaaminiana. Nina mifano mingi ya mume kamletea mke. Au mke kamletea mume VVU. Ukiwa single.. unakaa kimachale muda wote na haumwamini mtu. NA WATU WALIOOA NA KUOLEWA WANACHEPUKA SANA. Sasa sijui ww unaongelea ndoa gani.. ila sio za hapa Tz. Kuchepuka ni kawaida sana.

4. Mlo bora. WaDada wengi wa leo hata kupika hawajui.

5. Msaidizi.. Binafsi nina wafanyakazi WENGI TU. Na hao wananisaidia kazi zangu za biashara, nyumbani nk. Nawalipa vizuri, na wanafanya kazi vizuri. Sasa ww utapata msaidizi mmoja na tena kama ni MVIVU ndio imekula kwako na hauwezi kumwachisha kazi na Mahari Ulishatoa. Mimi wasaidizi wangu kama ni mvivu au hana uaminifu wa kazi, anapata pink slip.
Pamoja mkuu umetisha sana
 
Back
Top Bottom