SoC01 Faida atakayopata kijana baada ya kuoa

Stories of Change - 2021 Competition

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Pamoja na uwepo wa utitiri wa ndoa sasa lakini bado katika ulimwengu wa sasa kuna vijana wanaogopa kuoa.

Kwanza kijana acha uoga kila kijana akiamua anaweza kuoa na kumudu familia hata kama ana kipato kidogo tu. Nina miaka miwili ndani ya ndoa na hizi ni faida nilizopata.

MATUMIZI BORA YA FEDHA.
Kabla sijaoa ni rahisi sana kutumia pesa bila mpangilio mzuri, unaweza kwenda baa ukagawa 🍻 na ofa mbalimbali,kula kula hovyo sababu nyumbani hakuna chakula lakini ukiwa na mke huwezi kufanya mbele yake hata kidogo.

Unaweza kutumia pesa nyingi bila hofu sababu uko na washkaji,ukioa lazma kwanza uwaze familia kwanza ndio marafiki wafuate.

KUSAVE MUDA WAKO WA ZIADA
Kabla hujaoa unaweza ukawa ni mtu wa kujichanganya popote bila ratiba na mwaliko,hutojali sehemu ya kulala au utakapoamkia,lakini ukioa ni lazma ulale nyumbani tu.

ULINZI NA USALAMA WA AFYA YAKO
Hapa kabla hujaoa ulikuwa na tabia labda ya kuruka ruka(kudanga) au kufanya ngono zembe. Hapa kuna hatarisha afya yako kutokana na magonjwa ya zinaa,kulea mimba bandia au mimba zisizotarajiwa.

Ukishaoa kama utamweshimu mwenzio badi yote hayo hutopata, utakuwa unafaidika na mwenzi wako mida wowote na kwa usalama zaidi.

MLO BORA NA MZURI KWA AFYA
Ukiwa bachela unaweza kula vyakula vya hovyo hovyo na hata kama utakula hotelini basi utakula chakula kilichopo na pia gharama itakuwa ni kubwa kuliko ungekula nyumbani.

Ukioa,utachagua chakula unachopenda, garama zitakuwa ndogo,utawekewa matunda na utaulizwa kama umeshiba au la,raha iliyoje?

MSAIDIZI BORA KABISA WA MAISHA
Hapa kumbuka utapikiwa na kuoshewa vyombo,utafuliwa nguo zako vizuri,utashauriwa nguo ya kuvaa,utatizamwa kama umependeza,utafarijiwa ukiwa na mawazo,umechoka,unaumwa n.k

Changamoto za ndoa zipo lakini haziondoi hizo faida. Zoote hizo ni faida je una nyingine ujazie? Au kama bado hujaoa Ukiwa kijana ni kipi kinachokufanya usioe?

Karibuni.
 
Upvote 21
Wewe Jombaa unaonekana unajielewa sana. Safi sana keep it up!

Marriage is an expense to a man. Kama wewe una kipato kidogo halafu uoe utafilisika zaidi. Kama wewe ni tajiri halafu uoe, lakini usiongeze kipato, uta-downgrade lifestyle to accommodate the additional expenses.

From a financial standpoint, marriage is only beneficial to women because they share the man's resources. It doesn't work the other way though i.e women don't share resources with men - they leave. (filisika ujue tabia ya mkeo)

Remember that women only marry up. So, from the first day of a relationship, the woman reaps financial dividends right away. Women can escape poverty through marriage but men can't. (Ni rahisi CEO mwanaume kuoa binti mpika bagia Singida ila sio rahisi CEO mwanamke kuolewa na mwanaume mlina asali Tabora)
 
You have made my day Joh Doe
Thank you for the nice reply.
Be blessed mate.
 
Kikubwa uwe umepatia kwenye kuchagua mwenza wako au hizo faida ulizozitaja utazisoma kwenye vitabu tu. Watu wengi walikua wana progress vizuri walipokua mabachela, baada ya kuoa dreams zao zikakoma siku ya harusi
Ukipatia kuoa mbingu unaianzia hapa hapa duniani.
 
Kweli kabisa
 
Sawa kabisa...huwa natafakari hizi mambo halaf sielewi...ngoja nizeekezeeke kwanza labda ntaelewa
 
Haya uliyosema hapa ni sawa na kuwambia watu waendele kunywa bia na wasinunue mabati kwa ajili kujenga kwakua yanaweza kuwakata.
 
Bado hujakomaa sawasawa km bado unadhani wewe una maisha mazuri kwa vile eti hujaoa.
 
Acha uoga we we
 
Dahh we jmaaa
 
Ndoa ni nzuri tena ni nzuri, nasema hivyo kama shuhuda kwa miaka 6 sasa.
Lakini katika ndoa kuna changamoto nyingi mno mno ambazo kitu pekee kitakachoweza kufanya hiyo ndoa iendelee ni busara na uvumilivu.

Wakati ule sijaoa nilisema wazi kabisa nimekwisha kuvuka viunzi vingi kwenye maisha,badala yake nimekuja kukutana na milima mirefu mno ambayo nisingependa kuiandikia hapa.

Hapo mwanzo nilijua labda ni mimi peke yangu ndio napitia haya labda ni bahati mbaya yangu tu, lakini kumbe ni kilio cha kila alieko kwenye ndoa.

Ukikutana na wenye kua ndoa 10 basi kama sio tisa basi nane wanalia.

Na bahati mbaya nyingine sisi wengine tuko kwenye kifungo cha mke mmoja ndio hakuna rangi ambayo hatuachi kuiona.

Kwa hiyo hakuna furaha ya moja kwa moja ndugu zangu kwenye ndoa msidanganywe, kitu pekee unachotakiwa kuwa nacho kwenye ndoa ni uvumilivu, tena uvumilivu haswa.pia busara na akili kubwa ya kuweza kuishi na mwenzako jamii ukiwaona mnacheka lakini mna kuumia kwa namna moja ama nyingine mioyoni.

Furaha pekee inayoweza kupatikana kwenye ndoa ni watoto, na asante Mungu kwa hilo maana isingekuwa hivyo sijui ingekuwaje.

Huu ni mtazamo wangu kulingana na uzoefu wangu huo mdogo, inaweza kuwa kinyume chake kwa wengine.
 
Watoto , kuheshimika katika jamii
 
Bandiko zuri kweli ....Kura 2 tu dah

Yule Liverpool keshawadanganya maskini...
 
Kuna watu mnajua Sana,dahh mbaandika ukweli unaouma Sana,the naked truth, lakini SASA mkuu,ndio tusioe kabisa kabisa yaani tuzeeeke tukiwa mabachelor au,tuchase Kwanza dreams zetu , after awhile ndio tuoe huku tukijua fika ukweliculioundika hapo juu!?
 
Sawa kabisa...huwa natafakari hizi mambo halaf sielewi...ngoja nizeekezeeke kwanza labda ntaelewa
Kabisa mkuu,ngoja nikuekue Kwanza huenda nikawa miongoni mwa kuishi kwingi kuona mengi
 
Hapa kila mtu anavutia kwake kulingana na faida anazopata

kila upande una faida na hasara zake

ngoja nibaki neutral nisome comments
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…