SoC01 Faida atakayopata kijana baada ya kuoa

Stories of Change - 2021 Competition

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Pamoja na uwepo wa utitiri wa ndoa sasa lakini bado katika ulimwengu wa sasa kuna vijana wanaogopa kuoa.

Kwanza kijana acha uoga kila kijana akiamua anaweza kuoa na kumudu familia hata kama ana kipato kidogo tu. Nina miaka miwili ndani ya ndoa na hizi ni faida nilizopata.

MATUMIZI BORA YA FEDHA.
Kabla sijaoa ni rahisi sana kutumia pesa bila mpangilio mzuri, unaweza kwenda baa ukagawa 🍻 na ofa mbalimbali,kula kula hovyo sababu nyumbani hakuna chakula lakini ukiwa na mke huwezi kufanya mbele yake hata kidogo.

Unaweza kutumia pesa nyingi bila hofu sababu uko na washkaji,ukioa lazma kwanza uwaze familia kwanza ndio marafiki wafuate.

KUSAVE MUDA WAKO WA ZIADA
Kabla hujaoa unaweza ukawa ni mtu wa kujichanganya popote bila ratiba na mwaliko,hutojali sehemu ya kulala au utakapoamkia,lakini ukioa ni lazma ulale nyumbani tu.

ULINZI NA USALAMA WA AFYA YAKO
Hapa kabla hujaoa ulikuwa na tabia labda ya kuruka ruka(kudanga) au kufanya ngono zembe. Hapa kuna hatarisha afya yako kutokana na magonjwa ya zinaa,kulea mimba bandia au mimba zisizotarajiwa.

Ukishaoa kama utamweshimu mwenzio badi yote hayo hutopata, utakuwa unafaidika na mwenzi wako mida wowote na kwa usalama zaidi.

MLO BORA NA MZURI KWA AFYA
Ukiwa bachela unaweza kula vyakula vya hovyo hovyo na hata kama utakula hotelini basi utakula chakula kilichopo na pia gharama itakuwa ni kubwa kuliko ungekula nyumbani.

Ukioa,utachagua chakula unachopenda, garama zitakuwa ndogo,utawekewa matunda na utaulizwa kama umeshiba au la,raha iliyoje?

MSAIDIZI BORA KABISA WA MAISHA
Hapa kumbuka utapikiwa na kuoshewa vyombo,utafuliwa nguo zako vizuri,utashauriwa nguo ya kuvaa,utatizamwa kama umependeza,utafarijiwa ukiwa na mawazo,umechoka,unaumwa n.k

Changamoto za ndoa zipo lakini haziondoi hizo faida. Zoote hizo ni faida je una nyingine ujazie? Au kama bado hujaoa Ukiwa kijana ni kipi kinachokufanya usioe?

Karibuni.
 
Upvote 21
Mkuu asante umeyasema yote niliyokua nayafikiria.
 
Naqubali [emoji817]
 
usicheze na Ke wewe kijana shukuru Mungu amekusaidia hapo! lkn pia lazima umjaribu kwa kumpa wkt mgumu!.ili ujue ni jembe au kichwa cha panzi....muendekeze kifara lkn ..

siku ukijichanganya akikugeuka ndo utajua kuwa hujui, ke huwa hatu tumii nguvu sisi kuwaumiza endelea kukoroma yeye anasoma mchezo....... kwanza yeye mwenyewe Mungu, ke tuliwahi kumpa changamoto palee Bustanini Eden!!.

akawaagiza me wote muuishi nasi kwa akili alikuwa hatanii.... wewe ni nani? alisha sema kaeni nao kwa akili!!! huyo katumwa usomeshe wanae wafike UNIVER. tena si ajabu watoto si wako, ukisha tia mjengo wa maana..magari..ndo utajua muziki kamili........

leo me mnapigika ajili ya ke''...endelea kucheza na ke! muziki utaujua baadaye kwenye 70 umesha choka!! huyo wkt wa kuvurugana ni sasa mvuruge maksudi tu!! asibweteke uone reaction yake! mpaka avumilie hasa!!

mwanamke/familia kuijenga ni Mungu tu!! akusimamie sana wewe!! na uombe usiku na mchana akunusuru wengi wamekufa na kuparalyse ajili ya mbunye! wanakufa wanawake wana baki jiulize kwa nini??
 
kamata kinywaji hapo naja kulipa chap
mtoa mada ameongea kinadharia, wewe umeandika kiuhalisia
 
Wapingaji ni wengi sana ktk maswala ya ndoa,na wengi wao ni hao wasiooa.
Mtu bachela kuelewa swala la ndoa ni kazi flan ya ziada akuelew,msingi bora wa mtu bachela kuoa wew mpe mda tu utamfikia siku yake.

Mtu Bachela hana adabu na wala busara hana kwake kila kitu ni kibaya ktk ndoa.

Mtu bachela ni mpinzani mkubwa na mtu ambae ameoa au kuolewa,swala la ndoa kwake ni mfupa mgum usiotafunika.

Mtu bachela kutana nae maskani tu mpige story nasio kwako usimkaribishe, kua nae makin akija kwako anataka kuja kupata mawazo namna gani anaweza kuoa imeisha na urafik wenu upambe hapo.

Kiufupi mtu bachela au muhuni sio mtu mzuri
 
Haya uliyosema hapa ni sawa na kuwambia watu waendele kunywa bia na wasinunue mabati kwa ajili kujenga kwakua yanaweza kuwakata.
Yani wewe ndio zero kabisa sijui umeandika nini ,,kwani wanao kunywa hawajengi na wanao jenga hawanywi...
 
Umeandika vizuri ila 95% una maumivu kuliko furaha
 
Kwenye Afya na mlo kamili siyo wote wanakutana na hiyo.

Wapo walioletewa magonjwa wakiwa kwenye ndoa.

Kuna jamaa yangu alioa ka sister duu kakawa "kamshindishia" chapati msukuma yule aka-retreat.
 
Pamoja mkuu umetisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…