Accumen Mo
JF-Expert Member
- May 15, 2022
- 18,036
- 39,882
Uko sahihi 💯 kwanza tujitambue nafasi yetu sisi wanaume kuhudumia hamna kingine mm dini yangu ya kiislamu nimeona majukumu mengi sana kama mume nikioa kwa mke kumuhudumia ngua, malazi mpaka mavaziKwa mtizamo wangu, ukioa mke kwa mtizamo kuwa aje akusaidie a.k.a kusaidiana, unakuwa ushaanza kwa mguu wa kushoto. Ni suala la mda tu utalia kimanga.
Unatakiwa kuoa mwanamke kwa jicho la wewe kumsaidia yeye. Ukiwa na mtizamo wa namna hiyo ni ngumu kuwa disappointed.
Kwa mantiki hiyo, kabla ya kuoa, unapaswa ujiulize, unayemuoa anahitaji msaada wako? Anahitaji aina ya msaada unaotaka kumpa? Kama jibu ndio oa, kama sio, wewe unachotakiwa ni kummzabzab kisha pita. Huyo sio wako, waachie wengine. Kumbuka hupaswi kulazimishia kumpa mtu huduma kama mwenyewe haoneshi kuihitaji ( haijalishi uzuri wa huduma yako)
Kwa ujumla dhana ya mwanaume kufikiria kusaidiwa na mwanamke kuanzia mwanzo ni mtego wa hatari sana. Kwa bahati mbaya zaidi ni kwamba kwa sasa wanawake wanakuwa na nguvu za kiuchumi na kimamlaka kuliko wanaume na hivyo taasisi ya ndoa kuwa miguu juu kifo cha mende. In the future, wanaume wanaweza kuolewa na wanawake. Kwa lugha nyingine wanawake kushika nafasi ya wanaume na wanaume kushika nafasi za wanawake kwenye familia na maisha kwa ujumla. Kwa bahati mbaya zaidi hatuna la kufanya kuzuia hii kutokea.
Kwa mfano zamani hata ukiongea na mwanamke alikuwa na aibu anaangalia chini, siku hizi anakutolea macho hadi wewe ndio unaona aibu.
In the future, wanawake wasomi watatongoza wanaume na wanaume wataanza kuringa ringa kama wanawake wa zamani.
Basi utakuta mwamba anatupiwa mistari na mwanadada, huku mwamba kainamia chini anachimba kashimo kwa miguu. Dunia ngumu sana hii ndugu zangu.
Ukikubalu tu mke awe na kipato umeumia akiwa na kipato labda angalau kitokane na wewe mfano umemfungulia biashara