Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787]Ukioa mke msomi akaajiliwa akipangiwa dodoma ukimpigia video call usiku lazima uone kivuli chenye madevu au chenye kitambi kinavaa kondomu
Inasikitisha sana kiukweli kabisa kuna watu wameoa wanawake hawana elimu na mambo ni yale yale. Hii mentality tunayozidi kujijengea mi huwa naona inategemea na muhusika tu iwe msomi au hakwenda shule, all in all niishie hapo ila kusema kuoa mke ambaye hajasoma ni kujidanganya watu tuombe kupata kilicho chema tu.Watoto wenu wa kike msiwasomeshe
Ieleweke si wote waliosoma wana hayo mapungufu wala si wote ambao hawajasoma ndo wake bora ila asilimia kubwa ya wanawake waliosoma wana hizo tabia. Unaweza ukawa na bahati ukapata aliesoma na akakufaa na unaweza ukawa na mkosi ukampata ambae hajasoma na akawa na changamoto vile vile.Inasikitisha sana kiukweli kabisa kuna watu wameoa wanawake hawana elimu na mambo ni yale yale. Hii mentality tunayozidi kujijengea mi huwa naona inategemea na muhusika tu iwe msomi au hakwenda shule, all in all niishie hapo ila kusema kuoa mke ambaye hajasoma ni kujidanganya watu tuombe kupata kilicho chema tu.
Hapo sawa na bila shaka ndo umeweka kitu ambacho nilitaka kiwe hivyo kwamba kwendana na tafiti asilimia kubwa ndiyo imeonekana wasomi wana hizo shida. Umeeleweka.Ieleweke si wote waliosoma wana hayo mapungufu wala si wote ambao hawajasoma ndo wake bora ila asilimia kubwa ya wanawake waliosoma wana hizo tabia.
Ndoa ni makubaliano lakini wanaopenda kudhalilisha wanawake ndiyo wanaopiga kelele saaana.At the same time wazazi wangu wa kike mashangazi etc wamesoma Sana na Bado ndoa zao nahisi ziko vzr japo siwezi kujua Siri za ndani ila hawajaachwa.
Yeah! Tuone wasomeshe watoto wao wa kiume tu halafu waozeshe hao mabwana wanaopiga wanawake waone kama litawapendeza hilo.Watoto wenu wa kike msiwasomeshe
Kabisa mzeyaMchawi hela tuu hapo
Ni ndoto za wanaume wengi kuoa mwanamke mrembo na mwenye kipato ili wasaidiane kutengeneza familia bora ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba nzuri,kusomesha watoto kwenye shule bora n.k Hapo ndipo baadhi ya vijana hufikiria kuoa wanawake wasomi wenzao wenye kazi nzuri. Lakini kabla ya kufikiria kuoa mke msomi na mwajiriwa( hasa serikalini) ni vema ukajua faida na hasara zake.
Tukianza na faida
1. Mke mwajiriwa atakusaidia kuongeza kipato kwa maendeleo ya familia.
2. Pindi hali yako ya kiuchumi ikienda vibaya,familia inaweza isiyumbe na km itayumba basi ni kidogo.
3. Kazi/cheo cha mkeo kinaweza kuleta heshima fulani ndani ya familia.
Hasara zake:-
1. Kuna baadhi ya wanawake akichangia hela yake kununua kitu mfano kiwanja usishangae siku mkikosana akakudhalilisha kwamba kiwanja kanunua yeye,au nyumba kajenga yeye.
2. Wanawake waliosoma na wenye kazi wengi wao (SI WOTE ) huwa si watiifu kwa waume zao hasa ikitokea kipato chake ni kikubwa kuliko mme.
3. Jiandae na mivutano ya haki sawa. Kuna baadhi ya wanawake wasomi huigeuza ndoa kuwa sehemu ya kufanya uanaharakati. Hali hii inaweza kuibua mivutano ya mara kwa mara.
4. Ndoa kuongozwa na vichwa 2. Maandiko yanasema, "Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe" Efeso 5:23.
Kuna baadhi wanawake wakisha soma na kuwa na ajira nzuri hujipa mamlaka ndani ya nyumba. Baadala ya mume kuwa sauti ya mwisho kimaamuzi atataka yeye awe msemaji wa mwisho. "In nature"wanaume hatuko tayari kutawaliwa na mwanamke hapo inaweza kuwa chanzo cha ndoa yenu kusambaratika.
5. Ndugu wa mke kukudharau/ kutokupa heshima unayostahili hasa km familia yao ni ya kishua na wasomi.Hebu fikiria mkeo ni mkuu wa kitengo muhimu aafu wewe Mwalimu wa shule ya msingi( mfano tu), Usishangae kwa baadhi ya matukio ukawa wa mwisho kupewa taarifa. Tena usiombe iwe familia ya Kihaya( kidding).
6. Watoto wakigundua mama yao anapesa nyingi kuliko baba heshima yao kwako inaweza shuka na usishangae kuona shida zao nyingi wanamalizana na mama yao. Hapa usipokuwa makini unaweza jikuta km umetengwa ndani ya nyumba yako.
Kuna afande ni rafiki angu hiki kimemkuta,watoto hawana time nae kabisa.
7. Usitegemee neno pole na kazi au kupokewa mzigo utokapo kazini. Mwanamke mwenye kazi anajiona hata yeye ni mtafutaji. Hivyo anaweza asione sababu ya kukupokea kwani hata yeye katoka kutafta huo mkate.
8.Kuleta ubosi kitandani. Wanawake wengi wenye kazi na mabosi hujisahau na kuleta ubosi wao hadi nyumbani. Hivyo mkiwa faragha usishangae kauli za kibabe na wengi wao hawawezi kuwa romantic.
Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo mengi nimejifunza kwa brother angu aliyeoa Daktari mwenzake mwenye cheo kikubwa kuliko yeye na kwa baadhi ya wafanyakazi wenzangu.
NB: Niko tayari kurekebishwa.
Tusipo wasomesha watapata tabu maishani bora tuwasomeshe hata kama hawatakuja kuolewa lakini waweze kujitegemea kiuchumi.Watoto wenu wa kike msiwasomeshe
Kikubwa maelewano, though mahusiano mengi ambayo mwanamke yupo juu kielimu na kiuchumu kuna kadharau fulani hivi kapo kwenda kwa mwanaume wake...Smart911 Unasemaje katika hili
🤣🤣🤣Yule lazima ukae chiniKikubwa maelewano, though mahusiano mengi ambayo mwanamke yupo juu kielimu na kiuchumu kuna kadharau fulani hivi kapo kwenda kwa mwanaume wake...
Mpishano kidogo utasikia tafuta hela... hahahaha...
Kama yule aliyekuaga vice presidaa kipindi kilichopita...
Sii unaona jamaa alivyofichwa/ kumezwa...🤣🤣🤣Yule lazima ukae chini
Mi nimemfahamu sura majuz wakati anatoatoa tuzawadi🤣Sii unaona jamaa alivyofichwa/ kumezwa...