Faida na hasara za kutumia mafundi maiko kwenye ujenzi

mlinzi mlalafofofo

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2008
Posts
725
Reaction score
1,282
Tuanze na faida kwanza

1. Bei rahisi, uzuri bei zao mchekea sana na kama ukiwa mbishimbishi au mtu wa kukomaa kubargain sana unapata punguzo kubwa kabisa la bei bila kujali ugumu au ukubwa wa kazi yenyewe.

2. wanatumia vizuri rasilimali zilizopo, ukitaka fundi maiko akujengee ukuta anakuambia "bosi hii kazi inahitaji tofali mia na hamsini ila hapa uwanjani kwako nimeona tayari una tofali nzima na vipande, nitatumia hizihiz kwanza hlf tutaangalia kama kuna haja ya kuongeza". mwisho wa siku unajikuta umefanya kazi kubwa kwa kutumia rasilimali ambazo pengine hata wewe ulikuwa haujui kama unazo au kama zingeweza kutumika tena. unakuwa umeokoa pesa kwa mambo mengine.

3. wako fleksibo na mazingira yaliyopo
ukimuita fundi maiko ukamwambia skiza nataka ugawe hii sebule nipate chumba kinachojitegemea. hiyo siyo shida kwa fundi maiko na wala hana haja ya kuanza kuchora kwenye makaratasi, kila kitu kitamalizwa apoapo tena ni juu kwa juu mwisho wa siku unakabidhiwa chumba chako icho apo. wako fasta hawana urasimu.

4. unahudumiwa kadiri ya uwezo wako. wako vizuri kubalance uwezo wa bosi na mahitaji ya ujenzi. unaweza kuwa na kazi kubwa lakini yeye utamsikia "bosi hapa lete mifuko mitatu tu ya simenti kazi inaisha hii". kumbe mwenzio kashakusoma wewe ni hoehae huna ela mtasumbuana bure tu mwisho umnyime kazi. apo yeye atacheza na ratio ya simenti kwa mchanga hadi kazi yako inaisha.

5. Hasara ya mafundi maiko ni ubora wa kazi zao. kazi nyingi zinakuwa za viwango vya chini kwa sababu ya matumizi madogo ya matirio zinazotakiwa kwa mfano simenti inaumiwa kwa kiasi kidogo kuliko inayotakiwa, sehem ya kuweka mbao mpya unakuta mwenzio katumia zile used au za kukodisha zilizopindapinda matokeo yake kuta zinapinda. ila kiujumla ni wana sana hawa wamba. salute kwa fundi maiko wote.
 
🙌🙌🙌Mmenishinda tabia ya ha a jamaa
 
Kwa maisha ya watanzania wengi tunatumia mafundi maiko,ni wachache wanao watumia mainjinia kwenye ujenzi wao
KAZI NJEMA MAFUNDI MAIKO
Ma Engineer mimi siwezi fanya nao kao kwanza wao wanajionaga ndo wajumvi wa kila kitu. injinia hata ukimleta akutengenezee zizi tu basi atakuomba uwe na tape nk
 
huwa naona hata hawa wachina wanapenda sana kuwatumia mafundi maiko kwenye miradi yao. tena wanasisitiza kabisa. wao wanawasimamia tu.
 
Afu fundi maiko anajua kila kitu,we muulize kupaka rangi anajua,kuweka vigae anajua,kuweka bomba anajua,kupaua anajua

Kumbe unapompa kaz asiyoijua anawatafuta wengine wanaoijua na anaelewana nao kwa pesa ndogo wakat kaz ni kubwa,wale nao kwa tamaa zao za kukosa kazi wanakubal lakin kazi wanafanya kwa kulipua hapo ndo utakapo koma mwenye nyumba
 
Kuna wa hivyo niliwapa kazi yangu wakakomaa na kupaua mwisho wasiku nikuvujiwa tu ni mwendo wa kuweka silicon tu😂😂😂
 
asante mkuu je yuko vizuri kunyoosha kuta, kujenga mjengo wa hidden roof
Hidden roof hata kushauri maana yangu tulijenga nae tukavua bati tukapiga ya kusimama

Yeye ni fundi kujenga na plaster

Ni mkweli muwazi na asipo elewa anauliza

Ni vyema kumsimamia pale unapoweza ili kazi yako iwe bora

Ananyoosha vizuri haya ma banda nyuma alinyoosha huyo nilekupa namba

ila Kuna mwingine alinitengenezea fensi ya kucholea na msingi wa haya mabanda(bahati mbaya jamaa alipata shida ya hernia akafanyiwa operation) chapombe wangu hajapona vizuri bado tusimpe kazi ngumu mpaka apone vizuri
20241006_120427.jpg
 
Back
Top Bottom