Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Bible ni kitabu kamili kisicho shaka kimefungwa muhuri hakuna kuongeza Wala kupunguza.
Unaongelea biblia ipi kwanza, ya kiorthodox, ya kiroma ama ya Kiprotestanti.

Na unaongelea vision ipi KJV au ipi!?

Hzo biblia ziko the same!?

Wewe unatumia biblia ipi!?
 
Jamii zetu za kitanzania mara nyingi huwa tunazaliwa katika imani.
Unapelekwa hata ukiwa mdogo.
Labda nikubakikishie tu kuwa nnazijua imani vizuri.
Ilihali kuna miungu zaidi ya 3000+, Ninajua habari za miungu zaidi ya 70 ambayo ni inaaminika/iliaminika na jamii kubwa kubwa.

Na kwa muktadha wa Tanzania hapa, moja kwa moja tunamzungumzia Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote yulee wa kwenye mawingu. (mbinguni)

Huyu mungu mwenye sifa hizi ndiye ambae huwa naongezea kusema hayupo + hawezekani kuwepo.

Kwahyo Mungu huyu ambae unamhubiri kila siku na mnabishana kila siku hayupo, wala hana uwezekano wa kuwepo.

Unaweza kushare na mimi taarifa sahihi za huyo Mungu wako kama si hizi nimeziainisha?


Sijajua ni lini, lakini huwa najibu haraka sana kwa kusema kuwa sijui.
Na hakuna ajuaye mpaka sasa, zaidi ya kuwa kuna nadharia tu.

Ila kutokujua kwa jibu sahihi siwezi kukubali kudanganywa.
Silazimiki kujua mama ake Mandela90 mwenye umri wa miaka 30 ni nani kukataa kuwa Salome mwenye umri wa miaka 28 si mama wa Mandela90.

Wazo la Mungu ni la mwisho kwenye kufikiri. Na ni jibu la uongo.
Yaani kama hutaki kufikiri, kisingizio cha wewe ni kumtaja Mungu tu na case inakuwa closed.

Kwanza Uulizaji wa swali lako lipo katika uwezo hafifu sana na ni limited.
Kwanini unataka kujua ni nani aliyeweka moyo kwa mtu hujawaza kuwa ni nini kiliweka moyo kwa mtu.!?

Hauoni kuwa mawazo yako yanataka yakutane na jibu ambalo unalitaka!?

Yaani hapo kwa mfano uliodhahiri ni kwamba kipofu kwa uzoefu wake wa kusikia sauti tu, anataka kujua bendera ya taifa ina sauti ya aina gani!?

Kwahyo nature ya swali lako wewe (kipofu) kuhusu nani kaweka moyo (bendera) ni illogical kwasababu linahitaji kujua nani (sauti) na haujawaza kuwa ni nini (rangi) kisa tu wewe experience yako ni unachokiwaza muda huo.

Kwahiyo uulizaji mbaya wa swali ni mwanzo wa kupata majawabu yasiyo sahihi.

Hata nkikubali kwa mujibu wako Kama unasema Mungu ndiye kaweka hayo yote, yeye hiyo akili hadi ya kuumba hivyo vitu kaitoa wapi.
Unadhani kuwa yeye katengenezwa na nani!?
[emoji3532] Nijibu hili

Kwamba wewe unaelewa kwenye bible ambayo ina contradiction za wazi kiasi kile.

Kabla ya yote thibitisha uwepo wa Mungu.

Sayansi kila siku inamuendelezo.
Sasa huoni kuwa unatumia deus ex machina hapo kumkimbiza Mungu.

Unaweza kunieleza mwisho wa sayansi.

Hujaweza kumthibitisha huyo Mungu zaidi ya madhanio uliyojitengenezea akilini mwako.

Kwasababu hatujawaza kwa mtzamo mmoja haimaanishi kuwa siko sahihi.

Usahihi wa kitu hauexist.
Usahihi wa kitu unapimwa kutokea kwenye point ya marejeleo.

Mfano,
[emoji3532]Yesu alisulubiwa na kupaa kama utatumia biblia kama point ya kurejelea.
[emoji3532]Lakini pia Yesu hakusulubiwa lakini alipaa kama utatumia Quran kama point ya rejea.
Na ni ukweli kulingana na hizo point husika.
[emoji3532]Na ukifuata kanuni za dunia hii na ushahidi wa kihistoria kama point ya rejea, habari ya yesu ni uongo na haiwezekani.

Ushauri wangu kwako ni kwamba,
Tusiwe na anthropic bias katika kuwaza ukweli wa mambo, we need extra uchunguzi hasa katika kustudy ulimwengu.

Haikuwa rahisi mtu kukubali kuwa dunia ni tufe, maana lazima ufikirie inakuwaje watu wahang tu na wasidondoke south poles!?
Kumbe hata concept ya up_bottom ni jinsi tunavyoona tu ukiwa duniani ama sayari nyingine.

Haikuwa rahisi mtu kukubali kuwa dunia inazunguka jua ama kujizungusha katika mhimili wake,
Kwamaana ukiangalia kwa mawazo na experience za duniani hapa ni kama illogical hivi.

Hata mawazo ya mwanzo na mwisho ni mawazo ya kizamani.
Wenzio walioandika vitabu vya dini walikuwa na mawazo hayo kuwa dunia ni flat na ina pembe
Hujawaza kuwa wewe unaweza kuwa unawaza tofauti kwa kudhani tu kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho?

Kumbuka hata muda tu sio absolute, Muda unatofautiana sehemu na sehemu na hii ni proved kabisa.
Gravit na speed zinaathiri muda.

Unajua kuwa nkikupelea sehem yenye gravit kubwa kama black hole [emoji874], ukiishi dakika 45 za pale tu kwa duniani inaweza kuwa ni miaka kadhaa zaidi ya 15+.

Inawezekana ukaenda pale ukaja kurudi duniani ukakuta mwanao amekupita umri.

Nimechomekea tu hapo
Mambo ni mengi tusiyoyajua, hivyo ni vyema kuepuka anthropic biased idea katika kuutafiti ulimwengu.

Je uko tyari kufungua akili ili kujifunza tafiti zenye kuuelewa ulimwengu!?

Now umenarrow down to the core of our discussion.

Huyo Mungu wa juu mawinguni ndio Mungu ambaye hayupo na simjui pia, wala hajaelezewa hivo katika Bibilia.

Bibilia imemuwasilisha kwetu Mungu ambaye ni roho wala hakai sehemu inaitwa mawinguni.

Hiyo idea ya Mungu wa mawinguni ni doctrine ambayo ni potofu na ndio hicho nimekuwa nikikuambia kuwa, msingi wa doctrine yako ukiyumba huko mbele lazima uone biblia ni kitabu cha kutungwa.

Mimi sio mmoja wa hao wanaoamini Mungu anaishi mawinguni, ninaamini kwa ushahidi wa bibilia kuwa Mungu ni roho na anapatikana kila mahali.

Mara nyingi sana Bibilia imekuwa ikiaddress kama “Mungu wa mbinguni” na ikaeleweka vibaya kama Mungu anayeishi mawinguni. Hii ni matokeo ya usomaji mbovu wa maandiko pasipo kuzingatia kanuni zote za kutafsiri maandiko.

Consequently, idea hii imepelekea wengi kuamini kwamba kuna safari ya kwenda mbinguni huko ambako inaaminika Mungu anaishi, which is wrong and indoctrinal.

Ukishaamini hivo lazima uone bibilia ni kitabu cha uongo na cha kutungwa na watu tu.
 
Ni hivi kijana Mungu alimuumba binadamu na lengo la Mungu ni kwamba binadamu asife ,kifo kilikuja baada ya binadamu kutenda dhambi ya kula lile tunda ambalo lilikuwa la kutambua mema Na mabaya Na kabla ya kula tunda binadamu alikua haujui ubaya wowote so kula tunda kulifanya binadamu aondoke kwenye lengo la Mungu Kwa kuujua ubaya,na ubaya ndio uliozaa mauti so mauti ilikuja baada ya binadamu kuujua ubaya automatically kifo kikatokea
Kiongozi hii sawa na kuzaa watoto alafu unaweka shimo kuwa mtatumbukia. Unawawekea shimo la nini? Kuweka ule mti wa ujuzi wa mema na mabaya ilikuwa na haja Gani? Wakati hawakumkosea chochote.?

Na kwanini aliwafukuza bustanini ili wasile matunda ya mti wa uzima wakawa wazima.? Kuna maswali mengi sana hayako pouwa kabisa.
 
Unajua elimu ya kiroho watu hawaijui vizuri ,kwanza unatakiwa utambue tunakufa mwili lakini nafsi ni immortal yani haifi so sisi binadamu wote tulishaumbwa toka zamani Kwa iyo kuna transition kuanzia rohoni kuja kwenye mwili then rohoni tena kwenye u milele Kwa iyo sasa Mungu alipoona binadamu kaujua upande wa pili wa ubaya Na kumbuka Mungu kiasili hakai na ubaya wowote so ili kutuokoa kwenye hii dhambi ndipo akamleta yesu ili aweze kutusaidia kuuona uzima ule wa milele yani kufanya restoration
Hii inamaanisha Mungu alitengeneza tatizo alafu analitatua mwenyewe.
 
Now umenarrow down to the core of our discussion.

Huyo Mungu wa juu mawinguni ndio Mungu ambaye hayupo na simjui pia, wala hajaelezewa hivo katika Bibilia.

Bibilia imemuwasilisha kwetu Mungu ambaye ni roho wala hakai sehemu inaitwa mawinguni.

Hiyo idea ya Mungu wa mawinguni ni doctrine ambayo ni potofu na ndio hicho nimekuwa nikikuambia kuwa, msingi wa doctrine yako ukiyumba huko mbele lazima uone biblia ni kitabu cha kutungwa.

Mimi sio mmoja wa hao wanaoamini Mungu anaishi mawinguni, ninaamini kwa ushahidi wa bibilia kuwa Mungu ni roho na anapatikana kila mahali.

Mara nyingi sana Bibilia imekuwa ikiaddress kama “Mungu wa mbinguni” na ikaeleweka vibaya kama Mungu anayeishi mawinguni. Hii ni matokeo ya usomaji mbovu wa maandiko pasipo kuzingatia kanuni zote za kutafsiri maandiko.

Consequently, idea hii imepelekea wengi kuamini kwamba kuna safari ya kwenda mbinguni huko ambako inaaminika Mungu anaishi, which is wrong and indoctrinal.

Ukishaamini hivo lazima uone bibilia ni kitabu cha uongo na cha kutungwa na watu tu.
Roho ni nini?
 
Tafuta biblia zilizo halali utajua maana ya Tunda, achana na hizo nakala za kihuni walizotafsiri VATICAN kwa kuficha ficha mambo kwa maslahi yao.

Mtu wa kwanza hakuitwa Adam wala mkewe hakuitwa eve maana hawakuwa na asili ya Uzungu, pili hawakuishi huko walikotuaminisha hawa wachungaji na wanasayansi uchwara.

Tatu Tunda maana yake ilikuwa ni maarifa/Neno la ujuzi wa kutambua mambo fulani hapa dunian, na Mti ulito toa hayo matunda ni Malaika ambao waliishi dunian na walikuwa na mission zao hapa hapa dunian.

Mtu wa kwanza alipewa ONYO asiwasiliane na hao malaika wala kuwaomba wampe/wamwambie Habari za maarifa waliyonayo ambayo walukatazwa kuyajua maana yalikuwa nje ya uelewa wao(Tunda).

Baada ya kuumbwa kwa mwanamke ambaye biblia za uongo zinamuita eva/hawa huyu hakuumbwa kwa udongo kama Adam bali aliumbwa kutokana na Imagination+mawazo ya Adamu kuhusu uwepo wa kiumbe kitakachofanana nayeye kitakachomtoa upweke hivyo eva aliumbwa kwa staili hii.

Kwakuwa Eva hakuwa na Uelewa sawa ama nguvu sawa na adamu bali alishawishika na kiumbe ambacho biblia zenu zinasema ni nyoka(Dragon) ambaye ndiye alimshawishi eva na eva ndiye wa kwanza kuyasikiliza maarifa ya wale malaika walioambiwa wasiyasikie na baadae akamueleza Adam, hapa ndipo chanzo cha maovu kilipoanza.

Adam hakufa kama tunavyodanganywa bali alipewa laana kwa wazawa wake na hata eva hakufa tafuta ktk biblia yako hutoona maala wanaeleza hili jambo zaid ya kudanganya kuwa adam alikufa na umri wa miaka fulan which is nonsense.

Unatakiwa ujuwe kuwa Adam mission yake aliyoletwa dunian ilikuwa ni kuongeza idadi ya malaika waliosaliti ambao idadi yao ilitakiwa kuwa replaced na wana wa adam atakao wazaa na mkewe maana Adamu nae kabla ya kuumbiwa mwili alikuwa ni sehemu ya malaika, baada ya anguko la shetan na wenzie ndipo ikaja sababu ya adamu kushushwa dunian na akafanyiwa mwili ili aweze kuendeleza uumbaji wa malaika wapya(wanadamu).

Idadi inayotakiwa kwa wana wa adamu kureplace idadi ya malaika waliosaliti mbingu inajulikana na huenda ikatimia muda ukifika.

Shida za dunia hazitokwisha na hizo raha mnazotamani hazitopatikana maana huyo kiumbe anaeitwa shetan hataki idadi ya wana wa adamu itimie maana ikitimia na ule mwisho utafika na hukumu kwa shetan na wafuasi wake itafika.

Shetan si mjinga kuwapotosha watu na kuwafanya wamsaliti Muumba ili tu idadi isifikie na malengo ya shetani kuutawala ulimwengu yaendelee uku idadi ya wana wa adamu ikiendelea kudhorota na anguko la wengi liwepo.

Tutafute elimu nje ya box, Hilo kanisa la kizungu la Katolic wakishirikiana na madhehebu yote na dini zote hawa ndio wahuni nambari moja waliopotosha Biblia ya kweli kwa kufuta baadhi ya vitabu na vingine kuvipotosha kwa kuedit na kuweka uongo mwingi maana hawa wote wako chini ya shetan kuhakikisha wana wa Adamu hatuijui kweli na hatuifikii ile idadi inayotakiwa kureplace jeshi la shetani.

Tuendeleeni kushabikia mamipira, maushenzi ya kubishiana dini ya nani ndio sahihi, kuuwana sisi kwa sisi, kujadiri uwepo wa Mungu na ujinga mwingne tunajichelewesha sisi wenyewe
Hiyo Biblia ya Kweli tunapata wapi watu kama sisi wa kawaida. Accessibility yake ngumu sana Mkuu. Any assistance please.
 
Nani kakuambia kabla ya kula lile tunda kulikuwa hamna kifo? If kifo hakikuwepo why kulikuwa na mti wa uzima wa milele? Soma Biblia vizuri usisikilize wachungaji
Hapa Kuna point kubwa sana kiongozi umeiongea. Kuwepo mti wa uzima wa milele Kuna presuppose existence ya uwepo wa kifo. Na ndiyo maana aliwafukuza wasija wakala tunda la mti wa uzima wa milele.

You are very right KIONGOZI.
 
Nani kakuambia kabla ya kula lile tunda kulikuwa hamna kifo? If kifo hakikuwepo why kulikuwa na mti wa uzima wa milele? Soma Biblia vizuri usisikilize wachungaji

Umewaza vema.

Ukweli ni kwamba Adam na Hawa kabla ya kula lile tunda walikuwa katika state ambayo ni either immortal or mortal.
Ilikuwa ni state ambayo ni indecisive.
So uchaguzi wao ndio ulikuwa udetermine wataangukia katika state ipi.

Kama wangekula tunda la mti wa uzima that means wangekuwa immortals.

Uzima na mauti ni matokeo ya uchaguzi wa mtu. Ndio maana hata leo Mtu anapoamini katika masihi wake anapokea uzima wa milele.

Niko hapa kwa maswali zaidi…


Karibu
 
Mkuu umeongelea kuhusu Mathayo.

Injili ya Mathayo iliandikwa kwa ajili ya waty wasio wasomi, haswa ililenga wayahudi wa kipindi kile.

Mathayo alikuwa ni Muongo.
Historia ya herode mkuu kuagiza watoto kuchinjwa ni story ya kujitungia tu.
Kwanza kaandika mathayo peke yake, hakuna sehemu yeyote ile ambayo utakuta hiyo habari hata uyahudini penyewe.

Katika kujaribu kuunga unga hadithi zake na kumvuta yesu aonekane alitabiriwa tangu kale kwenye imani ya wayahudi, kasome mstari huu Ndugu Mathayo katika kuzima moto alijichanganya yeye mwenyewe Matthew 27:9–10.

Na hapo ndipo unajua kuwa hadithi ya Mungu Muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote si ya kweli, na wala huyo Mungu hajaandika kitabu. Kwa sifa alizo nazo asingeruhusu kitabu chake kiwe na makosa maelfu.
Ni watu waliamua kujitungia hadithi zao tu.
🤣🤣🤣It's a amalgamation of myths
 
Umewaza vema.

Ukweli ni kwamba Adam na Hawa kabla ya kula lile tunda walikuwa katika state ambayo ni either immortal or mortal.
Ilikuwa ni state ambayo ni indecisive.
So uchaguzi wao ndio ulikuwa udetermine wataangukia katika state ipi.

Kama wangekula tunda la mti wa uzima that means wangekuwa immortals.

Uzima na mauti ni matokeo ya uchaguzi wa mtu. Ndio maana hata leo Mtu anapoamini katika masihi wake anapokea uzima wa milele.

Niko hapa kwa maswali zaidi…


Karibu
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Okay basi wewe ni samaki na ni mbuzi upo katikati... Ongea point sio shiti sawa
 
Ni hivi kijana Mungu alimuumba binadamu na lengo la Mungu ni kwamba binadamu asife ,kifo kilikuja baada ya binadamu kutenda dhambi ya kula lile tunda ambalo lilikuwa la kutambua mema Na mabaya Na kabla ya kula tunda binadamu alikua haujui ubaya wowote so kula tunda kulifanya binadamu aondoke kwenye lengo la Mungu Kwa kuujua ubaya,na ubaya ndio uliozaa mauti so mauti ilikuja baada ya binadamu kuujua ubaya automatically kifo kikatokea
haujajibu swali mkuu
 
"MUNGU angetuuliza kila mmoja kama utakubali kuishi ili uje kufa baadae kuliko kutufanyia umafia kama huu."

Nakazia ni umafia wa hali ya juu sana.
 
Back
Top Bottom