Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

🤣Umetumia bible na logic in one word. 🤣Aya niambie Yesu alienda wapi baada ya kuzaliwa Egypt au Nazareth? 🤣Na kulikuwa na watu wangapi au malaika wangapi baada ya kufufuka kaburini... 🤣Kwanza mathayo anakuambia watu kibao walifufuka pamoja na Yesu wakaenda kutokea watu mitaani mbona Hawa wote hawakuwa Kristo aliyehai...🤣 Biblia ni mkusanyiko wa story za mababu wayahudi wasio na ujuzi Wala maarifa ya uhalisia wa dunia
Mkuu umeongelea kuhusu Mathayo.

Injili ya Mathayo iliandikwa kwa ajili ya waty wasio wasomi, haswa ililenga wayahudi wa kipindi kile.

Mathayo alikuwa ni Muongo.
Historia ya herode mkuu kuagiza watoto kuchinjwa ni story ya kujitungia tu.
Kwanza kaandika mathayo peke yake, hakuna sehemu yeyote ile ambayo utakuta hiyo habari hata uyahudini penyewe.

Katika kujaribu kuunga unga hadithi zake na kumvuta yesu aonekane alitabiriwa tangu kale kwenye imani ya wayahudi, kasome mstari huu Ndugu Mathayo katika kuzima moto alijichanganya yeye mwenyewe Matthew 27:9–10.

Na hapo ndipo unajua kuwa hadithi ya Mungu Muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote si ya kweli, na wala huyo Mungu hajaandika kitabu. Kwa sifa alizo nazo asingeruhusu kitabu chake kiwe na makosa maelfu.
Ni watu waliamua kujitungia hadithi zao tu.
 
Ni hivi kijana Mungu alimuumba binadamu na lengo la Mungu ni kwamba binadamu asife ,kifo kilikuja baada ya binadamu kutenda dhambi ya kula lile tunda ambalo lilikuwa la kutambua mema Na mabaya Na kabla ya kula tunda binadamu alikua haujui ubaya wowote so kula tunda kulifanya binadamu aondoke kwenye lengo la Mungu Kwa kuujua ubaya,na ubaya ndio uliozaa mauti so mauti ilikuja baada ya binadamu kuujua ubaya automatically kifo kikatokea
Mbona wanyama wengine wanakufa pia? Nao walitenda Dhambi? And Kobe anapiga life miaka mamia ya kutosha.. na Nyoka pia nasikia Hawafi hadi wauawe au akose msosi kwa muda mrefu sana...
 
The GOD is almighty, he is able, he can do anything at any time. ikiwa hivyo means alikuwa na uwezo wa kupredict kuliwa kwa tunda la mti wa kati kati, kiumbe binadamu aliemuumba kwa mfano wake ilikuaje akaruhusu hilo jambo litokee na aingize kiumbe chake alichokiumba kitawale vitu vyote matatizoni? in kiranga's voice
 
Mkuu, unafahamu history ya bible vizuri?

Unawajua watu wanaitwa Masoreti!?

Hizo hadithi za mafarao zimekuja ingizwa baadae sana, na zikawa updated kwenye issue ya majira na nyakati za utawala wao.
Hiyo imefanyika baadae sana.

Hiki unachokisoma leo sio hiko kilichosomwa kale!

Kwahyo madai yako haya nayatupilia mbali na badala yake nakuvutia ukafanye uchunguzi na kusoma historia ya biblia.

Mungu hayupo ndo maana hata kitabu cha biblia kina makosa mengi ya wazi kabisa.
Makosa yapi mfano
 
Kwa maelezo yako tu hapo moja kwa moja huyo Mungu hawezekani kuwepo.

Kwa wanaofikiria vizuri na kwa uhuru watanielewa,
Kwa sifa zile basic ambazo anazo huyo Mungu, haingekuwa na ugumu huo kumuelewa mpaka tumtafute mtu anayejua zaidi.

Kwanini wengine ametunyima kumuelewa kama anaupendo wote?

Na kwa definition yako ni kwamba ili useme mwalimu ni mzuri na mbobezi wa masuala ya Mungu ni yule atayeniambia nikubali kuamini tu kwa hiari.

Nmeshakaa na walimu wa kila namna, kwa mahojiano na kufuata kanuni tu, hayupo mwalimu aliyeweza kufaulu hilo.
Utofauti ni kwamba mwalimu huyo lazima atataka kufanya indoctrination, hatapenda kuhojiwa.

Yani akikwambia nyeupe ni nyeusi ukae kwa kutulia, ukihoji ama kwenda against anakwambia unapepo.

huyo Mungu alifail kwenye jaribio dogo sana la mantiki.

Usihangaike sana mkuu kuhusu jambo hilo.
Kwamaana Huyo Mungu hayupo kwenye uhalisia maybe kama unaweza kumthibitisha.

Labda tuanzie hapo “kwa sifa zile basic ambazo anazo huyo Mungu”..

Kwa haraka haraka kama ni mtu makini na wa kureason, huoni kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kwamba hata hizo sifa ulizonazo kuhusu Mungu inawezekana si sahihi na pengine hazijawekwa kwako vizuri?

Msingi ukishakuwa mbovu nadhani unajua namna utaathiri uelewa wako juu ya jambo fulani.

Its like a domino effect, erroneous basics will always lead to confusion.

What if taarifa ulizonazo mpaka sasa kuhusu Mungu si sahihi?

Uwepo wa waalimu fake haimaanishi kwamba hakuna waalimu sahihi wenye kunyoosha doctrine vizuri, ni kwamba una bahati mbaya sana umeangukia kwa wasaka tonge. Ila waalimu wazuri wapo. Just don’t give up.

Its very funny mtu kwa ujasiri kabisa anaclaim kwamba hakuna Mungu. Nilishawahi kukuuliza embu nisaidie kujua source ya mwanadamu ni nini? Nani aliweka moyo ndani ya mtu, mrija mmoja utoe damu na mwingine uingize damu? Nani alisuka ubongo ndani ya binadamu?

Bro unahitaji kuwa na moyo mgumu sana kuamini kuwa hakuna Mungu.

Mungu yupo, na wewe kutokuelewa how things are in the bible haimaanishi kwamba hakuna Mungu. Ni wewe ndo hujaelewa.

Sayansi inapoishia, hapo ndo you should start thinking uwezekano wa uwepo wa Mungu.

Bado hujareason strongly enough, endelea kufanya research mkuu.
 
Mkuu umeongelea kuhusu Mathayo.

Injili ya Mathayo iliandikwa kwa ajili ya waty wasio wasomi, haswa ililenga wayahudi wa kipindi kile.

Mathayo alikuwa ni Muongo.
Historia ya herode mkuu kuagiza watoto kuchinjwa ni story ya kujitungia tu.
Kwanza kaandika mathayo peke yake, hakuna sehemu yeyote ile ambayo utakuta hiyo habari hata uyahudini penyewe.

Katika kujaribu kuunga unga hadithi zake na kumvuta yesu aonekane alitabiriwa tangu kale kwenye imani ya wayahudi, kasome mstari huu Ndugu Mathayo katika kuzima moto alijichanganya yeye mwenyewe Matthew 27:9–10.

Na hapo ndipo unajua kuwa hadithi ya Mungu Muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote si ya kweli, na wala huyo Mungu hajaandika kitabu. Kwa sifa alizo nazo asingeruhusu kitabu chake kiwe na makosa maelfu.
Ni watu waliamua kujitungia hadithi zao tu.

Hiyo Mathayo 27:9-10 ina shida gani mkuu embu nifumbue macho[emoji23]

Mkuu Mungu hajawahi kuandika kitabu mkuu.. hii sumu iondoe kichwani, watu ndo wameandika biblia, kwa uvuvio wa Mungu.

Pia makosa unayaona wewe leo ktk bible sio doctrinal mistakes, ni makosa ambayo mengi ni matokeo ya kutafsiri bible kutoka kiebrania au kigiriki kuja kiswahili.

Ndio maana unahitaji mwalimu[emoji23]
 
Unataka kusema kuwa muda uliwekwa na Mungu duniani!?
The Universe with all creation is subject to time. Mungu na viumbe wengine walioumbwa katika ulimwengu wa kiroho hawapo katika dimension ya muda.
 
Hiyo Mathayo 27:9-10 ina shida gani mkuu embu nifumbue macho[emoji23]

Mkuu Mungu hajawahi kuandika kitabu mkuu.. hii sumu iondoe kichwani, watu ndo wameandika biblia, kwa uvuvio wa Mungu.

Pia makosa unayaona wewe leo ktk bible sio doctrinal mistakes, ni makosa ambayo mengi ni matokeo ya kutafsiri bible kutoka kiebrania au kigiriki kuja kiswahili.

Ndio maana unahitaji mwalimu[emoji23]
Huo uvuvio unaweza kunieleza,

Huyo Mungu hayupo, unaweza kumthibitisha yupo?
 
Kwahyo haujawahi ona kosa lolote kwenye biblia!?

Au ni kama mziki wa kizungu, hata usipoelewa unatembea na biti
Bible ni kitabu kamili kisicho shaka kimefungwa muhuri hakuna kuongeza Wala kupunguza.
 
Habari zenu,

Natumaini wote wazima.

Huwa najiuliza swali hili kila siku. Na jibu sijawahi kupata, sasa kuna umuhimu gani wa kuishi duniani hali ya kuwa utakufa?

Biblia inasema kuwa Adamu na Hawa walikula tunda pale edeni eti ndo sababu tunakufa. Ina maana kuwa kifo hakikuwa kabla ya kula lile tunda na hata sijui nitunda gani hilo, biblia imetuficha kutupa ukweli.

Sasa kifo na tunda linahusiana na nini? kama MUNGU hakutaka Adam na Hawa wale lile tunda yanini aliliweka kwenye bustani ya edeni? majaribio mengine bana.

Hilo tunda lina ubaya gani? Kitu umekiumba kwanini ukataze kisiliwe? Biblia imetudanganya hapo.

Jamani hata kwa akili ya kawaida kweli upande mazao yako shambani halafu ukataze familia yako kula kweli inakuja? Biblia imeficha ukweli.

Hivi kweli uzae watoto wako alafu uje kuwauwa kisa hawajakutii au hawajafanya utakacho??

Kama tuliumbwa ili tufe ina faida gani kuishi duniani. MUNGU angetuuliza kila mmoja kama utakubali kuishi ili uje kufa baadae kuliko kutufanyia umafia kama huu.

Mtu unahangaika kutafuta maisha kwa kila hali hata mda mwingine hupati milo yako vizuri ili kujibana upate maisha manzuri, sasa unafanya yote ya nini wakati utakufa?

Mambo haya yanachanganya kichwa sana.

Labda kwa kukusaidia; Kila mahala binadamu atakapokaaa iwe Nyumbani kwako, au niseme Duniani na hata mbinguni, kuna utaratibu
Sasa wewe kujitoa ufaham kuwa kwa Mungu hakuna utaratibu; ulitakiwa ujitafakari kwanza kabla ya kuandika hii mada.
Labda kwa heading yako; Unataka kutuambia kuwa, hakuna haja ya kumiliki vitu mfano vya dhamani kwa sababu mwishoni vitaharibika na kutupwa?
Ujue Mungu anatumiliki kama moja ya Viumbe wake na ana full authority na sisi....
 
Unajua elimu ya kiroho watu hawaijui vizuri ,kwanza unatakiwa utambue tunakufa mwili lakini nafsi ni immortal yani haifi so sisi binadamu wote tulishaumbwa toka zamani Kwa iyo kuna transition kuanzia rohoni kuja kwenye mwili then rohoni tena kwenye u milele Kwa iyo sasa Mungu alipoona binadamu kaujua upande wa pili wa ubaya Na kumbuka Mungu kiasili hakai na ubaya wowote so ili kutuokoa kwenye hii dhambi ndipo akamleta yesu ili aweze kutusaidia kuuona uzima ule wa milele yani kufanya restoration
Umesema vyema kabisa mimi nimejifunza kanisani kwetu.Nasali kanisa la Yesu Christo la watakatifu wa siku za mwisho.
 
Unajua kuna vitu huvielewi I used to be like u but elimu ya mambo ya kiroho ni elimu pana sana na inahitaji imani kuielewa Kuna for nutshell mambo ya rohoni yanaongozwa Kwa kanuni binadamu tuliumbwa Kwa mfano wa Mungu so tuna uwezo mkubwa sana ndani yetu nafsi yako inauwezo wa kufanya maamuzi binafsi rejea kwenye mfano wa ibrahim wakati Mungu anampa mtihani wa kumpima imani Kwa kumtoa sadaka mwanawe so kama Mungu angekua anajua ya kwamba ibrahimu hawezi Kwa nn Mungu alimjaribu ibrahimu so Kuna nguvu flani Au nafsi flani binadamu kapewa ambayo Mungu hawezi kuijua
Sisi ni mfano wake tuna nguvu ndani yetu ambayo hata malaika hawana tuna uwezo wa kufanya maamuzi.Hicho ndicho kitu cha pekee.
 
Ni hivi kijana Mungu alimuumba binadamu na lengo la Mungu ni kwamba binadamu asife ,kifo kilikuja baada ya binadamu kutenda dhambi ya kula lile tunda ambalo lilikuwa la kutambua mema Na mabaya Na kabla ya kula tunda binadamu alikua haujui ubaya wowote so kula tunda kulifanya binadamu aondoke kwenye lengo la Mungu Kwa kuujua ubaya,na ubaya ndio uliozaa mauti so mauti ilikuja baada ya binadamu kuujua ubaya automatically kifo kikatokea
Tunda gani hilo🤣lisilojulikana
 
Labda tuanzie hapo “kwa sifa zile basic ambazo anazo huyo Mungu”..

Kwa haraka haraka kama ni mtu makini na wa kureason, huoni kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kwamba hata hizo sifa ulizonazo kuhusu Mungu inawezekana si sahihi na pengine hazijawekwa kwako vizuri?

Msingi ukishakuwa mbovu nadhani unajua namna utaathiri uelewa wako juu ya jambo fulani.

Its like a domino effect, erroneous basics will always lead to confusion.

What if taarifa ulizonazo mpaka sasa kuhusu Mungu si sahihi?

Uwepo wa waalimu fake haimaanishi kwamba hakuna waalimu sahihi wenye kunyoosha doctrine vizuri, ni kwamba una bahati mbaya sana umeangukia kwa wasaka tonge. Ila waalimu wazuri wapo. Just don’t give up.
Jamii zetu za kitanzania mara nyingi huwa tunazaliwa katika imani.
Unapelekwa hata ukiwa mdogo.
Labda nikubakikishie tu kuwa nnazijua imani vizuri.
Ilihali kuna miungu zaidi ya 3000+, Ninajua habari za miungu zaidi ya 70 ambayo ni inaaminika/iliaminika na jamii kubwa kubwa.

Na kwa muktadha wa Tanzania hapa, moja kwa moja tunamzungumzia Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote yulee wa kwenye mawingu. (mbinguni)

Huyu mungu mwenye sifa hizi ndiye ambae huwa naongezea kusema hayupo + hawezekani kuwepo.

Kwahyo Mungu huyu ambae unamhubiri kila siku na mnabishana kila siku hayupo, wala hana uwezekano wa kuwepo.

Unaweza kushare na mimi taarifa sahihi za huyo Mungu wako kama si hizi nimeziainisha?

Its very funny mtu kwa ujasiri kabisa anaclaim kwamba hakuna Mungu. Nilishawahi kukuuliza embu nisaidie kujua source ya mwanadamu ni nini? Nani aliweka moyo ndani ya mtu, mrija mmoja utoe damu na mwingine uingize damu? Nani alisuka ubongo ndani ya binadamu?
Sijajua ni lini, lakini huwa najibu haraka sana kwa kusema kuwa sijui.
Na hakuna ajuaye mpaka sasa, zaidi ya kuwa kuna nadharia tu.

Ila kutokujua kwa jibu sahihi siwezi kukubali kudanganywa.
Silazimiki kujua mama ake Mandela90 mwenye umri wa miaka 30 ni nani kukataa kuwa Salome mwenye umri wa miaka 28 si mama wa Mandela90.

Wazo la Mungu ni la mwisho kwenye kufikiri. Na ni jibu la uongo.
Yaani kama hutaki kufikiri, kisingizio cha wewe ni kumtaja Mungu tu na case inakuwa closed.

Kwanza Uulizaji wa swali lako lipo katika uwezo hafifu sana na ni limited.
Kwanini unataka kujua ni nani aliyeweka moyo kwa mtu hujawaza kuwa ni nini kiliweka moyo kwa mtu.!?

Hauoni kuwa mawazo yako yanataka yakutane na jibu ambalo unalitaka!?

Yaani hapo kwa mfano uliodhahiri ni kwamba kipofu kwa uzoefu wake wa kusikia sauti tu, anataka kujua bendera ya taifa ina sauti ya aina gani!?

Kwahyo nature ya swali lako wewe (kipofu) kuhusu nani kaweka moyo (bendera) ni illogical kwasababu linahitaji kujua nani (sauti) na haujawaza kuwa ni nini (rangi) kisa tu wewe experience yako ni unachokiwaza muda huo.

Kwahiyo uulizaji mbaya wa swali ni mwanzo wa kupata majawabu yasiyo sahihi.

Hata nkikubali kwa mujibu wako Kama unasema Mungu ndiye kaweka hayo yote, yeye hiyo akili hadi ya kuumba hivyo vitu kaitoa wapi.
Unadhani kuwa yeye katengenezwa na nani!?
♦️ Nijibu hili
Mungu yupo, na wewe kutokuelewa how things are in the bible haimaanishi kwamba hakuna Mungu. Ni wewe ndo hujaelewa.
Kwamba wewe unaelewa kwenye bible ambayo ina contradiction za wazi kiasi kile.

Kabla ya yote thibitisha uwepo wa Mungu.
Sayansi inapoishia, hapo ndo you should start thinking uwezekano wa uwepo wa Mungu.
Sayansi kila siku inamuendelezo.
Sasa huoni kuwa unatumia deus ex machina hapo kumkimbiza Mungu.

Unaweza kunieleza mwisho wa sayansi.

Hujaweza kumthibitisha huyo Mungu zaidi ya madhanio uliyojitengenezea akilini mwako.
Bado hujareason strongly enough, endelea kufanya research mkuu.
Kwasababu hatujawaza kwa mtzamo mmoja haimaanishi kuwa siko sahihi.

Usahihi wa kitu hauexist.
Usahihi wa kitu unapimwa kutokea kwenye point ya marejeleo.

Mfano,
♦️Yesu alisulubiwa na kupaa kama utatumia biblia kama point ya kurejelea.
♦️Lakini pia Yesu hakusulubiwa lakini alipaa kama utatumia Quran kama point ya rejea.
Na ni ukweli kulingana na hizo point husika.
♦️Na ukifuata kanuni za dunia hii na ushahidi wa kihistoria kama point ya rejea, habari ya yesu ni uongo na haiwezekani.

Ushauri wangu kwako ni kwamba,
Tusiwe na anthropic bias katika kuwaza ukweli wa mambo, we need extra uchunguzi hasa katika kustudy ulimwengu.

Haikuwa rahisi mtu kukubali kuwa dunia ni tufe, maana lazima ufikirie inakuwaje watu wahang tu na wasidondoke south poles!?
Kumbe hata concept ya up_bottom ni jinsi tunavyoona tu ukiwa duniani ama sayari nyingine.

Haikuwa rahisi mtu kukubali kuwa dunia inazunguka jua ama kujizungusha katika mhimili wake,
Kwamaana ukiangalia kwa mawazo na experience za duniani hapa ni kama illogical hivi.

Hata mawazo ya mwanzo na mwisho ni mawazo ya kizamani.
Wenzio walioandika vitabu vya dini walikuwa na mawazo hayo kuwa dunia ni flat na ina pembe
Hujawaza kuwa wewe unaweza kuwa unawaza tofauti kwa kudhani tu kuwa kila lenye mwanzo lina mwisho?

Kumbuka hata muda tu sio absolute, Muda unatofautiana sehemu na sehemu na hii ni proved kabisa.
Gravit na speed zinaathiri muda.

Unajua kuwa nkikupelea sehem yenye gravit kubwa kama black hole 🕳, ukiishi dakika 45 za pale tu kwa duniani inaweza kuwa ni miaka kadhaa zaidi ya 15+.

Inawezekana ukaenda pale ukaja kurudi duniani ukakuta mwanao amekupita umri.

Nimechomekea tu hapo
Mambo ni mengi tusiyoyajua, hivyo ni vyema kuepuka anthropic biased idea katika kuutafiti ulimwengu.

Je uko tyari kufungua akili ili kujifunza tafiti zenye kuuelewa ulimwengu!?
 
Back
Top Bottom