Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Faida ya kuishi duniani ni ipi kama tulizaliwa ili tufe?

Usihangaishe Sana akili Yako kwa vitu invisible. Cha msingi kikubwa kabisa amini Kuna Super natural power anayesimamia Kila kitu ambaye ndiye Mungu Muumba mweza yote. Mafundisho na maandiko yamechezewa Sana . Ishi vizuri na Kila mtu, na viumbe wote maana ni Mali ya Mungu. Baada ya hapo utapata ufaham mkubwa wa kiroho
Habari zenu,

Natumaini wote wazima.

Huwa najiuliza swali hili kila siku. Na jibu sijawahi kupata, sasa kuna umuhimu gani wa kuishi duniani hali ya kuwa utakufa?

Biblia inasema kuwa Adamu na Hawa walikula tunda pale edeni eti ndo sababu tunakufa. Ina maana kuwa kifo hakikuwa kabla ya kula lile tunda na hata sijui nitunda gani hilo, biblia imetuficha kutupa ukweli.

Sasa kifo na tunda linahusiana na nini? kama MUNGU hakutaka Adam na Hawa wale lile tunda yanini aliliweka kwenye bustani ya edeni? majaribio mengine bana.

Hilo tunda lina ubaya gani? Kitu umekiumba kwanini ukataze kisiliwe? Biblia imetudanganya hapo.

Jamani hata kwa akili ya kawaida kweli upande mazao yako shambani halafu ukataze familia yako kula kweli inakuja? Biblia imeficha ukweli.

Hivi kweli uzae watoto wako alafu uje kuwauwa kisa hawajakutii au hawajafanya utakacho??

Kama tuliumbwa ili tufe ina faida gani kuishi duniani. MUNGU angetuuliza kila mmoja kama utakubali kuishi ili uje kufa baadae kuliko kutufanyia umafia kama huu.

Mtu unahangaika kutafuta maisha kwa kila hali hata mda mwingine hupati milo yako vizuri ili kujibana upate maisha manzuri, sasa unafanya yote ya nini wakati utakufa?

Mambo haya yanachanganya kichwa sana.
 
Duuh
 
Ni hivi kijana Mungu alimuumba binadamu na lengo la Mungu ni kwamba binadamu asife ,kifo kilikuja baada ya binadamu kutenda dhambi ya kula lile tunda ambalo lilikuwa la kutambua mema Na mabaya Na kabla ya kula tunda binadamu alikua haujui ubaya wowote so kula tunda kulifanya binadamu aondoke kwenye lengo la Mungu Kwa kuujua ubaya,na ubaya ndio uliozaa mauti so mauti ilikuja baada ya binadamu kuujua ubaya automatically kifo kikatokea
Kwani Mungu hakujua kama hilo tunda Adam atakula?
 
Habari zenu,

Natumaini wote wazima.

Huwa najiuliza swali hili kila siku. Na jibu sijawahi kupata, sasa kuna umuhimu gani wa kuishi duniani hali ya kuwa utakufa?

Biblia inasema kuwa Adamu na Hawa walikula tunda pale edeni eti ndo sababu tunakufa. Ina maana kuwa kifo hakikuwa kabla ya kula lile tunda na hata sijui nitunda gani hilo, biblia imetuficha kutupa ukweli.

Sasa kifo na tunda linahusiana na nini? kama MUNGU hakutaka Adam na Hawa wale lile tunda yanini aliliweka kwenye bustani ya edeni? majaribio mengine bana.

Hilo tunda lina ubaya gani? Kitu umekiumba kwanini ukataze kisiliwe? Biblia imetudanganya hapo.

Jamani hata kwa akili ya kawaida kweli upande mazao yako shambani halafu ukataze familia yako kula kweli inakuja? Biblia imeficha ukweli.

Hivi kweli uzae watoto wako alafu uje kuwauwa kisa hawajakutii au hawajafanya utakacho??

Kama tuliumbwa ili tufe ina faida gani kuishi duniani. MUNGU angetuuliza kila mmoja kama utakubali kuishi ili uje kufa baadae kuliko kutufanyia umafia kama huu.

Mtu unahangaika kutafuta maisha kwa kila hali hata mda mwingine hupati milo yako vizuri ili kujibana upate maisha manzuri, sasa unafanya yote ya nini wakati utakufa?

Mambo haya yanachanganya kichwa sana.
Kama huoni faida ya kuishi we Kufa tu
 
Kwanza kama unaaamini ukifa utarudi kwa Mungu , huoni kwa upande WA Mungu sio issue kubwa? Tatizo ni kwamba Ile mission uliletewa hapa duniani umeimaliza?
Kuna mauti ya aina mbili Moja ni Ile ya kuumaliza mwendo ie kufa kimwili baada ya mission (vita) na ya pili ni Ile ya kutokumuona Mungu kwa sbabu kumkana jemedari WA vita .
 
Za kuambiwa changanya na za kwako... Hilo tunda ni Bikra...
Okay let's assume walikatazwa kusex
1. Nyoka kafanyaje Sasa kala tunda la Eva ndo Adam Akala au Eva kala tunda la nyoka afu akampa Adam? Usitoke nje ya Biblia ni jibu accord to logic na verses.
2. Wamekatazwa kulana ehe watoto wanatoka wapi ambao wameambiwa wajaze dunia.
3. In short the analogy ya tunda kuwa bikra falls apart completely hii story sio valid coz it's impossible scientifically haiwi supported historically geologically na pia logically. It's not historical na imeigwa from older cultures so ni myth story tu.
 
mungu alitaka kujua je mtamuamini yeye? na je makatazo yake uliyazingatia ? na je unamuabudu yeye au una mungu wako uliyemshirikisha? baada ya kufa ndio utayakuta uliyoyatenda
Ye si mjua yote? We unaweza ukaweka bomb chumbani afu ukawaambia watoto wako chezeni huko ila msiguse bomb? Hizi ni story za mababu katika kujaribu kujua shida zimetokea wapi ndo maana wamemtunga Eva Kama mwenye kosa coz ni mwanamke
 
Usihangaishe Sana akili Yako kwa vitu invisible. Cha msingi kikubwa kabisa amini Kuna Super natural power anayesimamia Kila kitu ambaye ndiye Mungu Muumba mweza yote. Mafundisho na maandiko yamechezewa Sana . Ishi vizuri na Kila mtu, na viumbe wote maana ni Mali ya Mungu. Baada ya hapo utapata ufaham mkubwa wa kiroho
Why ni msingi kuamini Mungu yupo?
 
Sasa hiyo mitihani yanini??
Kwanini shule, kanisani au madrasaa kuna mitihani?
Hiyo ni mitihani ya imani. Lazima Imani iwe ktk mizani. Unaamini nini? Je ni sahihi? Unatenda unacho amini? Huo ndiyo mtihani, mtihani wa imani.
 
Tafuta biblia zilizo halali utajua maana ya Tunda, achana na hizo nakala za kihuni walizotafsiri VATICAN kwa kuficha ficha mambo kwa maslahi yao.

Mtu wa kwanza hakuitwa Adam wala mkewe hakuitwa eve maana hawakuwa na asili ya Uzungu, pili hawakuishi huko walikotuaminisha hawa wachungaji na wanasayansi uchwara.

Tatu Tunda maana yake ilikuwa ni maarifa/Neno la ujuzi wa kutambua mambo fulani hapa dunian, na Mti ulito toa hayo matunda ni Malaika ambao waliishi dunian na walikuwa na mission zao hapa hapa dunian.

Mtu wa kwanza alipewa ONYO asiwasiliane na hao malaika wala kuwaomba wampe/wamwambie Habari za maarifa waliyonayo ambayo walukatazwa kuyajua maana yalikuwa nje ya uelewa wao(Tunda).

Baada ya kuumbwa kwa mwanamke ambaye biblia za uongo zinamuita eva/hawa huyu hakuumbwa kwa udongo kama Adam bali aliumbwa kutokana na Imagination+mawazo ya Adamu kuhusu uwepo wa kiumbe kitakachofanana nayeye kitakachomtoa upweke hivyo eva aliumbwa kwa staili hii.

Kwakuwa Eva hakuwa na Uelewa sawa ama nguvu sawa na adamu bali alishawishika na kiumbe ambacho biblia zenu zinasema ni nyoka(Dragon) ambaye ndiye alimshawishi eva na eva ndiye wa kwanza kuyasikiliza maarifa ya wale malaika walioambiwa wasiyasikie na baadae akamueleza Adam, hapa ndipo chanzo cha maovu kilipoanza.

Adam hakufa kama tunavyodanganywa bali alipewa laana kwa wazawa wake na hata eva hakufa tafuta ktk biblia yako hutoona maala wanaeleza hili jambo zaid ya kudanganya kuwa adam alikufa na umri wa miaka fulan which is nonsense.

Unatakiwa ujuwe kuwa Adam mission yake aliyoletwa dunian ilikuwa ni kuongeza idadi ya malaika waliosaliti ambao idadi yao ilitakiwa kuwa replaced na wana wa adam atakao wazaa na mkewe maana Adamu nae kabla ya kuumbiwa mwili alikuwa ni sehemu ya malaika, baada ya anguko la shetan na wenzie ndipo ikaja sababu ya adamu kushushwa dunian na akafanyiwa mwili ili aweze kuendeleza uumbaji wa malaika wapya(wanadamu).

Idadi inayotakiwa kwa wana wa adamu kureplace idadi ya malaika waliosaliti mbingu inajulikana na huenda ikatimia muda ukifika.

Shida za dunia hazitokwisha na hizo raha mnazotamani hazitopatikana maana huyo kiumbe anaeitwa shetan hataki idadi ya wana wa adamu itimie maana ikitimia na ule mwisho utafika na hukumu kwa shetan na wafuasi wake itafika.

Shetan si mjinga kuwapotosha watu na kuwafanya wamsaliti Muumba ili tu idadi isifikie na malengo ya shetani kuutawala ulimwengu yaendelee uku idadi ya wana wa adamu ikiendelea kudhorota na anguko la wengi liwepo.

Tutafute elimu nje ya box, Hilo kanisa la kizungu la Katolic wakishirikiana na madhehebu yote na dini zote hawa ndio wahuni nambari moja waliopotosha Biblia ya kweli kwa kufuta baadhi ya vitabu na vingine kuvipotosha kwa kuedit na kuweka uongo mwingi maana hawa wote wako chini ya shetan kuhakikisha wana wa Adamu hatuijui kweli na hatuifikii ile idadi inayotakiwa kureplace jeshi la shetani.

Tuendeleeni kushabikia mamipira, maushenzi ya kubishiana dini ya nani ndio sahihi, kuuwana sisi kwa sisi, kujadiri uwepo wa Mungu na ujinga mwingne tunajichelewesha sisi wenyewe
Haya maarifa umeyapata wapi?
 
Tukiachana na maandiko ukitumia akili ya kawaida huu ulimwengu uwepo wake kila kitu kinategemea uwepo wa kingine. Kifo kipo sababu kuna maisha, bila maisha hakuna kifo, bila kifo hakuna maisha.

Just imagine, binadamu wawe wanaongezeka tu hawafi mwendokasi Dar ingekuaje? Ni swali la kijinga sana ila just imagine.
 
Habari zenu,

Natumaini wote wazima.

Huwa najiuliza swali hili kila siku. Na jibu sijawahi kupata, sasa kuna umuhimu gani wa kuishi duniani hali ya kuwa utakufa?

Biblia inasema kuwa Adamu na Hawa walikula tunda pale edeni eti ndo sababu tunakufa. Ina maana kuwa kifo hakikuwa kabla ya kula lile tunda na hata sijui nitunda gani hilo, biblia imetuficha kutupa ukweli.

Sasa kifo na tunda linahusiana na nini? kama MUNGU hakutaka Adam na Hawa wale lile tunda yanini aliliweka kwenye bustani ya edeni? majaribio mengine bana.

Hilo tunda lina ubaya gani? Kitu umekiumba kwanini ukataze kisiliwe? Biblia imetudanganya hapo.

Jamani hata kwa akili ya kawaida kweli upande mazao yako shambani halafu ukataze familia yako kula kweli inakuja? Biblia imeficha ukweli.

Hivi kweli uzae watoto wako alafu uje kuwauwa kisa hawajakutii au hawajafanya utakacho??

Kama tuliumbwa ili tufe ina faida gani kuishi duniani. MUNGU angetuuliza kila mmoja kama utakubali kuishi ili uje kufa baadae kuliko kutufanyia umafia kama huu.

Mtu unahangaika kutafuta maisha kwa kila hali hata mda mwingine hupati milo yako vizuri ili kujibana upate maisha manzuri, sasa unafanya yote ya nini wakati utakufa?

Mambo haya yanachanganya kichwa sana.
Kwa hiyo faida za kufa huzioni??

JIULIZE
1. Kama ingekuwa hakuna kufa, watu wote toka enzi hizo Hadi sasa, hivi idadi ya watu ingekuwaje??
2. Ikiwa watu wanakufa na idadi ya watu baadhi ya nchi na Miji mfano Dsm Ina watu wengi kupitiliza, ingekuwa watu hawafi hali ingekuwaje??

3. Unadhani dunia ingetosha kusupport maisha ya watu wote??

4. Umewahi kuchinja mbuzi, kuku, bata, ng'ombe??

Wenyewe wanaona dhiki na tabu kuchinjwa na kuukiwa lakini wewe unachinja tu bila kuwaonea huruma, ndio hivyo hivyo Mungu anaona kawaida na kitu chepesi tu kufa kwako.
 
Kwanini shule, kanisani au madrasaa kuna mitihani?
Hiyo ni mitihani ya imani. Lazima Imani iwe ktk mizani. Unaamini nini? Je ni sahihi? Unatenda unacho amini? Huo ndiyo mtihani, mtihani wa imani.
Shuleni mnafundishwa na walimu sawa na mnapewa syllabus moja ndo mnapewa mtihani Tena unatengenezwa uwe fair. niambie mtihani huo wa Imani ni fair au sio fair? Na unafauluje?
 
Uko fair kwasababu unachagua upande wewe mwenyewe
Okay Kuna dini zaidi ya 10k unajuaje umechagua upande sahihi, na Kama we ni mkristo au Muslim huko Kuna makundi Tena mengine, unajuaje umechagua upande wa Mungu na wengine wote wamekosea? Unatofauti gani na mcheza jackpot?
Kingine mtihani wa shule mnapewa mda sawa kujiandaa mda sawa kufanya mtihani ni mmoja na unajua unafaulu vipi kwa kujibu vipi. Mtihani wa maisha according to wewe haupo hivyo, mnapimwa tofauti mnapewa mda tofauti wa kujiandaa na pia kufanya na kila mtu anaamini majibu yake coz hamna majibu clear. So how do u pass this test, mbona ni Kama kubet it's not clear n fair
 
Ukichukulia kifo ni kibaya na hasara ni kwel hauna faida ya kuishi , majibu mengne tafuta njee ya dini .
 
Unajua elimu ya kiroho watu hawaijui vizuri ,kwanza unatakiwa utambue tunakufa mwili lakini nafsi ni immortal yani haifi so sisi binadamu wote tulishaumbwa toka zamani Kwa iyo kuna transition kuanzia rohoni kuja kwenye mwili then rohoni tena kwenye u milele Kwa iyo sasa Mungu alipoona binadamu kaujua upande wa pili wa ubaya Na kumbuka Mungu kiasili hakai na ubaya wowote so ili kutuokoa kwenye hii dhambi ndipo akamleta yesu ili aweze kutusaidia kuuona uzima ule wa milele yani kufanya restoration
70 % ili ni jibu
 
Hatukuumbwa tufe ila kutokana na kutotii maagizo ndio maana ikatolewa adhabu hiyo, mfano rahisi ni huu je wewe baba yako akikwambia usifanye hiki halafu we ukakaidi kipi kitakukuta??

Pamoja na hayo na kupewa kutokufa, lakini binadamu alipaswa kutii maagizo ili awe hai mfano Adamu alitakiwa aishi kama binadamu ili aendelee kubaki hai mfano. Isingetegemewa apande juu ya mti mrefu halafu ajitupe chini asijeruhiwe hapana vyote vilipaswa kuzingatiwa

By the way, maisha ni matamu sababu tunakufa sipati picha leo hii bado tungekuwa na kina kingunge, Yuda eskarioti, plato etc sasa si dunia ingekuwa inaboa sana, we unakutana na watu wamezaliwa enzi za nuhu😁😁
 
Back
Top Bottom