Faida ya mabarafu kwenye recovery ya wachezaji

Faida ya mabarafu kwenye recovery ya wachezaji

Kama Kila mtu alisoma seli katika level mbalimbali. Kati ya zile cell organelles Iko inayoitwa mitochondria ambako vyakula vyetu vinaunguzwa na kupata nguvu, joto, hewa chafu (oxygen) na maji kidogo. Kama mkimmeagia mtu maji baridi sana atavuta hewa nyingi sana mapafuni ili akazalishe joto haraka kurekebisha uovu uliofanya. Mtoto akizaliwa anakutana na baridi kali sana nje ya tumbo la mama . Hii baridi kali ndiyo itasababisha mtoto aliye sana, kuvuta hewa nyingi mapafuni na kutengeneza nguvu na joto la kupambana na mazingira mapya ya nje ya tumbo kwenye joto kali.
Very true
 
Aaaah hiyo ni kweli, Moja ya njia mwili unatumia kupambana na kushuka kwa joto ni kusinjaa kwa mishipa midogo ya mbali na moyo (peripheral vasoconstriction) ili kuzuia damu isije kwenye ngozi kwa wingi. Hali hii inazuia mtu kutoka jasho na mishipa kupungua ukubwa wa tundu(lumen). Halisi hii inaweza kusababisha shinikizo la damu kidogo kutokana na
Ndio maana kumbe mtoto asipolia inaashiria shida au sio boss?
Asipolia kitu cha kwanza kuumia haraka ni ubongo, atakuwa na shida ya akili.
 
Wachezaji wanaumia zaidi siku hizi kuliko wakati wowote ule.
 
Yaa uko sahihi lakini sio kwa 100% Kuna watu ambao tayari Wanayo shida ya moyo na every high blood pressure. Hawa lazima wachukue tahadhari kabla ya kuoga maji ya baridi. Mwili unapambana na baridi kwa njia nyingi, njia mojawapo ni kusinyaa kwa mishipa iliyoko mbali na moyo (peripheral vasoconstriction) ili kuepuka damu isije kwa wingi kwenye ngozi na kupoteza joto zaidi . Kama mishipa itasinyaa damu nyingi itabakia kwenye mishipa mikubwa TU hivyo kusababisha kiwango cha shinikizo la damu kuongezeka kidogo. Hivyo kama ulikuwa na shida ya pressure au moyo itakuwa ni tatizo kidogo kwakuwa pressure itaongezeka kidogo. Kama pressure Yako ilikuwa kubwa mno basi unaweza kupata madhara ya kuongezeka pressure kama kiharusi au shida ya moyo kuongezeka kidogo.

Lakini hakuna mchezaji wa mpira mwenye shinikizo kubwa la damu au shida ya moyo kama alipimwa vizuri mwanzo wa msimu. Lakini hata kukaa kwenye barafu ni kwa muda maalumu na Kuna mtu ana stop watch anawahesabia wachezaji. Lakini pia hata wewe unapotaka kuoga maji ya baridi usianzie kichwani kujimwagia maji mengi bali anzia mikononi, miguuni , kiunoni, tumboni mabegani hadi malizia kichwa ili mwili uzoee baridi kidogo kidogokidogo (adaptation ) kuanzia mbali ya moyo.

Hata sauna Kuna watu hawaruhusiwi kwenda.
 
Pia kwa wale dada zetu wapenda urembo, wasio penda mikunjo kwenye ngozi zao za usoni ,chunusi na wanaotaka kuonekana warembo mda wote, watumie parafu kupitisha kwenye nyuso zao .
 
Mechi ni nyingi mno kuliko zamani, na siku hizi wanajituma zaidi kugombania nafasi ya kucheza.

Hata zamani match zilikuwa nyingi.

Michezo mingine pia tofauti na soka wachezaji wanaumia zaidi. Basketball ya sasa ni rahisi kuliko 80s or 90s na number of matches ni almost zile zile ila nao wanaumia kila siku.

Kuna uwezekano over dieting na hizi physiotherapy zinafanya wawe weak in the long term kuliko kuwasaidia.
 
Umeelezea kwa making na kwa ufasaha sana jinsi gani nguvu inazalishwa mwilin...
Lakin kuna sehemu umewapotosha wasomaji....
Swali langu nauliza ...wachezazi wanaingiaga kwenye mapipa ya mabarafu baada ya mechi tu kuisha...iweje kwenye mechi watumie energy na nguvu kubwa alafu waje waingizwe kwenye mabarafu wazalishe tena nguvu....
Bado itakua aujajibu kwanin wachezaji wanaingizwa kwenye yale mapipa
 
Si tu metabolism,hata kuifanya mishipa irejee kwenye balance ya msukumo wa oxygen na damu ndio maana hata madaktari uwanjani wanakua na barafu mtu akiumia tu anakandwa barafu ili kupoza misuli/cells za mwili zirejee ktk hali ya kawaida.
Kwa wanafunzi wanaoishi mazingira ya joto,chukua barafu or maji ya baridi weka kwenye beseni or ndoo kubwa weka miguu yako humo utasoma mpk uchoke mwenyewe never sleep
Unaujua usingizi vizuri lakini 😂

Sikupingi itafanya kazi lakini sio never sleep, usingizi ni nyoko mzee.
 
Umeelezea kwa making na kwa ufasaha sana jinsi gani nguvu inazalishwa mwilin...
Lakin kuna sehemu umewapotosha wasomaji....
Swali langu nauliza ...wachezazi wanaingiaga kwenye mapipa ya mabarafu baada ya mechi tu kuisha...iweje kwenye mechi watumie energy na nguvu kubwa alafu waje waingizwe kwenye mabarafu wazalishe tena nguvu....
Bado itakua aujajibu kwanin wachezaji wanaingizwa kwenye yale mapipa
Kuna tear and were kwa wachezaji, Njia pekee ya kuzalisha mitochondria kwa haraka ni kwa njia hii ya barafu, tear and were za viungo ni kwa misosi mizuri kulingana na mahitaji ya mwili. Kaka unapingana na sayansi au wape sayansi ya kwanini waingie kwenye mabarafu.
 
Mimi nilijika kwenye faida Wewe waelemishe hasara zake.
 
Hata zamani match zilikuwa nyingi.

Michezo mingine pia tofauti na soka wachezaji wanaumia zaidi. Basketball ya sasa ni rahisi kuliko 80s or 90s na number of matches ni almost zile zile ila nao wanaumia kila siku.

Kuna uwezekano over dieting na hizi physiotherapy zinafanya wawe weak in the long term kuliko kuwasaidia.
Leo nimeangalia mechi ya Chelsea na Manchester United ya mwaka 2001,nimejifunza kua Zamani wachezaji hawakua Fit Kama Sasa,hawakimbii Sana..hawakutani Sana Kama Sasa... now mpira wa kutumia nguvu Sana na kukimbia Sana..hata aina ya training now tupo level kubwa Sana so wachezaji kuumia lazima..
 
Leo nimeangalia mechi ya Chelsea na Manchester United ya mwaka 2001,nimejifunza kua Zamani wachezaji hawakua Fit Kama Sasa,hawakimbii Sana..hawakutani Sana Kama Sasa... now mpira wa kutumia nguvu Sana na kukimbia Sana..hata aina ya training now tupo level kubwa Sana so wachezaji kuumia lazima..
Siku hizi nafasi ya kuonyesha kipaji ni ndogo sana, mchezaji ww sasa anatakiwa amridhidhe kocha kwa kucheza kama kocha alivyomuagiza acheze. Hatari ya kuonyesha ufundi wako kama makudubela hapana, utakaa benchi. Mtu kama kibadeni na Sunday manara Leo hii wasingepata namba kwa kocha.
 
Leo nimeangalia mechi ya Chelsea na Manchester United ya mwaka 2001,nimejifunza kua Zamani wachezaji hawakua Fit Kama Sasa,hawakimbii Sana..hawakutani Sana Kama Sasa... now mpira wa kutumia nguvu Sana na kukimbia Sana..hata aina ya training now tupo level kubwa Sana so wachezaji kuumia lazima..

Kusema walikuwa hawakimbii sana maybe ila walikua rough na refs didn't bat an eye sio kama sasa hata ukimuangalia mwenzio vibaya tu unapewa card.

Unakumbuka battle ya Vieira na Keane? Seedorf vs Edgar Davids? CDM roho mbaya Gattuso, slide tackle za Maldini. Nani anacheza hata robo yao ya level yao hivi sasa? Ukiondoa kizazi cha kina Ramos na Pepe wanaofuata wote ni divas tu.
 
Siku hizi ni rahisi kuona timu ngeni zikija na mapipa yake kwaajili ya kuweka maji yenye barafu (maji baridi sana) kwaajili ya wachezaji. Faida hizi ya maji baridi sana sio TU kwa wwchezaji lakini ni kwa watu wote wanaooga maji baridi sana.

Ili mwili ufanyekazi zake vizuri unahitaji nguvu (ATPs), nguvu hizi ndizo anazozihitaji mchezaji ili kumudu kukimbia uwanjani kwa mafanikio makubwa.

Nguvu inazalishwa wapi na nini? Kuna vyanzo viwili vya kupata nguvu mwili, glucose (wanga) kutoka kwenye nafaka na mafuta kutoka kwenye nyama na mimea.

Kivipi? Ili mwili kutoa nguvu lazima chakula ulichokula kisangwe tumboni na kufyonzwe kwenye damu (glucose/fat acid), kisha chakula hiki kisafirishwe kutoka kwenye damu kuingia ndani ya seli za misuli ya mwili yaliko matanuli (mitochondria) ya kuunguzia chakula (glucose) na kuzalisha nishati (ATPs) pamoja na joto, carbon dioxide, na maji. Hivyo, ili mwili uzalishe nguvu unahitaji chakula kingi, mitochondria nuingi, oxygen nyingi na Insulin nyingi. Ingawa wakati wa mazoezi hata bila insulin chakula kitaunguzwa TU.

Mabarafu yanafanya nini? Ukizamishwa kwenye maji baridi sana joto la mwili litashuka ghafla sana, Hali hii itasababisha mwili kuwasha mitambo yote ya kuongeza joto haraka kujiokoa hivyo kuongeza kiwango cha kuchakata chakula (metabolism) ili kupata joto jingi haraka sana. Kitendo hiki kitazalisha glucose nyingi, mitochondria (matanuli) nyingi, oxygen nyingi kutoka mapafuni (hyperventilation) ili kuzalisha nishati kubwa sana mwilini, hatimaye nguvu nyingi kwa mchezaji ambazo zilipotea kwenye mechi iliyopita.

Kifupi kabisa mabarafu yanasaidia kuongeza na kurudisha matanuli (mitochondria) ya kuchomea na kuzalisha nguvu kwenye seli za misuli hivyo kumrejeshea nguvu zake mchezaji kwa kipindi kifupi sana kuliko kama angezirudisha kwa kupewa siku nyingi za kupunzika.

Nimejaribu kufupisha hii sayansi lakini nadhani umenipata.
Asante sana nilikua sijui kwanini wachezaji wanaingia kwenye mabarafu wakimaliza mazoezi.

Rai kwa wataalamu wetu kwenye kila nyanja tuanze kufanya haya mambo sisi wenyewe kuliko kusubiri wazungu wafanye halafu sisi ndio tuanze kuelezea theory zao.

Hii ishu ya wachezaji kuingia kwenye barafu kibongo bongo nimeanza kuona miaka ya karibuni ukilinganisha na wachezaji wa ulaya ambao nimeona wakifanya ivyo mida mredu kidogo.

Tufanye tafiti, tuhoji na tuje na gunduzi zetu ili wazungu nao waje kujifunza kutoka kwetu.
 
Anaudhoofisha mwili wake vibaya sana, ni hatari mno kwa mwili hata uzazi. Usiende. Kama unaweza oga maji ya baridi utajisikia nguvu nyingi baada ya kuoga. Ndio maana wanaoishi sehemu za baridi Wana uwezo mkubwa wa kutenda na kufikiria.
Hizi sasa fix
 
Back
Top Bottom