Faida ya mabarafu kwenye recovery ya wachezaji

Faida ya mabarafu kwenye recovery ya wachezaji

Asante sana nilikua sijui kwanini wachezaji wanaingia kwenye mabarafu wakimaliza mazoezi.

Rai kwa wataalamu wetu kwenye kila nyanja tuanze kufanya haya mambo sisi wenyewe kuliko kusubiri wazungu wafanye halafu sisi ndio tuanze kuelezea theory zao.

Hii ishu ya wachezaji kuingia kwenye barafu kibongo bongo nimeanza kuona miaka ya karibuni ukilinganisha na wachezaji wa ulaya ambao nimeona wakifanya ivyo mida mredu kidogo.

Tufanye tafiti, tuhoji na tuje na gunduzi zetu ili wazungu nao waje kujifunza kutoka kwetu.
Mweee...bongo yenyewe watu wanapenda story za ngono 🤣🤣🤣🤣
Speaking of ngono, vipi kama katikati ya round za mizangamuano mtu akajidumbukiza kwa ice bath...ata rudi round ifuatayo kwa nguvu zaidi?
 
Mweee...bongo yenyewe watu wanapenda story za ngono 🤣🤣🤣🤣
Speaking of ngono, vipi kama katikati ya round za mizangamuano mtu akajidumbukiza kwa ice bath...ata rudi round ifuatayo kwa nguvu zaidi?
Mtaalamu wetu atakuja kutupa ufafanuzi kuhusu hili suala
 
Siku hizi ni rahisi kuona timu ngeni zikija na mapipa yake kwaajili ya kuweka maji yenye barafu (maji baridi sana) kwaajili ya wachezaji. Faida hizi ya maji baridi sana sio TU kwa wwchezaji lakini ni kwa watu wote wanaooga maji baridi sana.

Ili mwili ufanyekazi zake vizuri unahitaji nguvu (ATPs), nguvu hizi ndizo anazozihitaji mchezaji ili kumudu kukimbia uwanjani kwa mafanikio makubwa.

Nguvu inazalishwa wapi na nini? Kuna vyanzo viwili vya kupata nguvu mwili, glucose (wanga) kutoka kwenye nafaka na mafuta kutoka kwenye nyama na mimea.

Kivipi? Ili mwili kutoa nguvu lazima chakula ulichokula kisangwe tumboni na kufyonzwe kwenye damu (glucose/fat acid), kisha chakula hiki kisafirishwe kutoka kwenye damu kuingia ndani ya seli za misuli ya mwili yaliko matanuli (mitochondria) ya kuunguzia chakula (glucose) na kuzalisha nishati (ATPs) pamoja na joto, carbon dioxide, na maji. Hivyo, ili mwili uzalishe nguvu unahitaji chakula kingi, mitochondria nuingi, oxygen nyingi na Insulin nyingi. Ingawa wakati wa mazoezi hata bila insulin chakula kitaunguzwa TU.

Mabarafu yanafanya nini? Ukizamishwa kwenye maji baridi sana joto la mwili litashuka ghafla sana, Hali hii itasababisha mwili kuwasha mitambo yote ya kuongeza joto haraka kujiokoa hivyo kuongeza kiwango cha kuchakata chakula (metabolism) ili kupata joto jingi haraka sana. Kitendo hiki kitazalisha glucose nyingi, mitochondria (matanuli) nyingi, oxygen nyingi kutoka mapafuni (hyperventilation) ili kuzalisha nishati kubwa sana mwilini, hatimaye nguvu nyingi kwa mchezaji ambazo zilipotea kwenye mechi iliyopita.

Kifupi kabisa mabarafu yanasaidia kuongeza na kurudisha matanuli (mitochondria) ya kuchomea na kuzalisha nguvu kwenye seli za misuli hivyo kumrejeshea nguvu zake mchezaji kwa kipindi kifupi sana kuliko kama angezirudisha kwa kupewa siku nyingi za kupunzika.

Nimejaribu kufupisha hii sayansi lakini nadhani umenipata.
Oya vipi kwa sie wazee wa kugegeda...ice vath betwin rounds itafanya nirudi kwenye game na nguvu zaidi?

Alafu mbona wengine wanasema ice bath ni fikra truu...true recovery ni sleep na msosi wa maana
 
Umeongea kitaalam Sana mkuu,
Hapa ambao hawana DD mbili umewaachaa solemba😊😊

Nukuu ya baba wa taifa.
""UTII UKIZIDI SANAA HUZAA UOGA, UOGA UKIZIDI SANA HUZAA UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA NA MWISHO WAKE NI MAUTI""
Hayo maneno yalisemwa na baba wa Taifa baada ya kutoka kwenye pipa la Maji baridi!?
 
Hizi sasa fix
Kama huna uhakika tulia na soma comments za wengine ili kuongeza maarifa. Sauna ni nini kwani? Bila shaka ni mvuke unaotokana na kuchemka maji. Faida pekee za zoezi hili ni kutananua mishipa ya damu (vasodilation) na kufungua vinyweleo vya ngozi kwa kutoa jasho jingi.

Lakini mwili wetu umetengenezwa kwa proteins ambazo kwenye joto hupoteza sifa yake(denatured) na wadudu wenyeji kwenye ngozi (normal flora) hawahitaji joto kubwa, na mafuta asilia ya ngozi huyeyushwa na kuondoshwa na joto. Hata enzymes na metabolism inakuwa weak.
 
utarudi upya kama vile hakuna ulichokifanya. Hali Yako itakuwa Tete kama utawasha heater ya shower ili uoge majimoto.

Hii knowledge sio mpya, watoto wetu zamani na vijijini huwa wanapenda kucheza kwenye mvua au kunyeshewa na mvua kwa bahati mbaya. Uimara wao ni tofauti kabisa na watoto wanaoogeshwa maji ya moto na kuvingirishwa kwenye mablangeti.
Mtaalamu wetu atakuja kutupa ufafanuzi kuhusu hili suala
 
Kama huna uhakika tulia na soma comments za wengine ili kuongeza maarifa. Sauna ni nini kwani? Bila shaka ni mvuke unaotokana na kuchemka maji. Faida pekee za zoezi hili ni kutananua mishipa ya damu (vasodilation) na kufungua vinyweleo vya ngozi kwa kutoa jasho jingi.

Lakini mwili wetu umetengenezwa kwa proteins ambazo kwenye joto hupoteza sifa yake(denatured) na wadudu wenyeji kwenye ngozi (normal flora) hawahitaji joto kubwa, na mafuta asilia ya ngozi huyeyushwa na kuondoshwa na joto. Hata enzymes na metabolism inakuwa weak.
Mbona jamaa wa maseru akili zao kama sie wabongo tuu...i.e mambumbumbuu japo kwao baridi kweli kweli
 
Mbona jamaa wa maseru akili zao kama sie wabongo tuu...i.e mambumbumbuu japo kwao baridi kweli kweli
Fanya utafiti mdogo kati ya watu wa Iringa, mbeya, Kilimanjaro, lushoto, Kagera kwenye baridi na watu wa Tabora, Pwani, Tanga kwenye joto.
 
Fanya utafiti mdogo kati ya watu wa Iringa, mbeya, Kilimanjaro, lushoto, Kagera kwenye baridi na watu wa Tabora, Pwani, Tanga kwenye joto.
Mbona wote mabwege tuu...hamna ata mmoja kati yao kafanya jambo la maaana sana hapa duniani.
 
Umeongea kitaalam Sana mkuu,
Hapa ambao hawana DD mbili umewaachaa solemba😊😊

Nukuu ya baba wa taifa.
""UTII UKIZIDI SANAA HUZAA UOGA, UOGA UKIZIDI SANA HUZAA UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA NA MWISHO WAKE NI MAUTI""
Mambo ya Mitochondria,,Mambo ya Cells(a smallest unit of life)
 
Anaudhoofisha mwili wake vibaya sana, ni hatari mno kwa mwili hata uzazi. Usiende. Kama unaweza oga maji ya baridi utajisikia nguvu nyingi baada ya kuoga. Ndio maana wanaoishi sehemu za baridi Wana uwezo mkubwa wa kutenda na kufikiria.
Mkuu hapa nikekupata ndo maana wanaume wa dar es salaam hawana akili kabisa nazani wameasiliwa na joto siyo kama wanaume wa mbeya
 
Hatimaye nimeujua ukweli, mi nilidhani wanajiloweka ili kupunguza maumivu ya misuli
 
Mkuu hapa nikekupata ndo maana wanaume wa dar es salaam hawana akili kabisa nazani wameasiliwa na joto siyo kama wanaume wa mbeya
Ngono inanoga sana sehemu zenye baridi kali kuliko sehemu ya joto jingi.
 
Max mzee mello anatokea kwenye barid leo hii tunaenjoy matunda ya jamiiforum
🤣🤣🤣🤣 Na magu naye alitoka sehemu ya baridi kali? Maana yule jamaa alikuwa na akili kuzidi watz wote hapa duniani
 
🤣🤣🤣🤣 Na magu naye alitoka sehemu ya baridi kali? Maana yule jamaa alikuwa na akili kuzidi watz wote hapa duniani
Kwani misenyi na biharamulo hakuna kabaridi?
 
Back
Top Bottom