Faida ya mabarafu kwenye recovery ya wachezaji

Very true
 
Aaaah hiyo ni kweli, Moja ya njia mwili unatumia kupambana na kushuka kwa joto ni kusinjaa kwa mishipa midogo ya mbali na moyo (peripheral vasoconstriction) ili kuzuia damu isije kwenye ngozi kwa wingi. Hali hii inazuia mtu kutoka jasho na mishipa kupungua ukubwa wa tundu(lumen). Halisi hii inaweza kusababisha shinikizo la damu kidogo kutokana na
Ndio maana kumbe mtoto asipolia inaashiria shida au sio boss?
Asipolia kitu cha kwanza kuumia haraka ni ubongo, atakuwa na shida ya akili.
 
Wachezaji wanaumia zaidi siku hizi kuliko wakati wowote ule.
 
Yaa uko sahihi lakini sio kwa 100% Kuna watu ambao tayari Wanayo shida ya moyo na every high blood pressure. Hawa lazima wachukue tahadhari kabla ya kuoga maji ya baridi. Mwili unapambana na baridi kwa njia nyingi, njia mojawapo ni kusinyaa kwa mishipa iliyoko mbali na moyo (peripheral vasoconstriction) ili kuepuka damu isije kwa wingi kwenye ngozi na kupoteza joto zaidi . Kama mishipa itasinyaa damu nyingi itabakia kwenye mishipa mikubwa TU hivyo kusababisha kiwango cha shinikizo la damu kuongezeka kidogo. Hivyo kama ulikuwa na shida ya pressure au moyo itakuwa ni tatizo kidogo kwakuwa pressure itaongezeka kidogo. Kama pressure Yako ilikuwa kubwa mno basi unaweza kupata madhara ya kuongezeka pressure kama kiharusi au shida ya moyo kuongezeka kidogo.

Lakini hakuna mchezaji wa mpira mwenye shinikizo kubwa la damu au shida ya moyo kama alipimwa vizuri mwanzo wa msimu. Lakini hata kukaa kwenye barafu ni kwa muda maalumu na Kuna mtu ana stop watch anawahesabia wachezaji. Lakini pia hata wewe unapotaka kuoga maji ya baridi usianzie kichwani kujimwagia maji mengi bali anzia mikononi, miguuni , kiunoni, tumboni mabegani hadi malizia kichwa ili mwili uzoee baridi kidogo kidogokidogo (adaptation ) kuanzia mbali ya moyo.

Hata sauna Kuna watu hawaruhusiwi kwenda.
 
Wachezaji wanaumia zaidi siku hizi kuliko wakati wowote ule.
Mechi ni nyingi mno kuliko zamani, na siku hizi wanajituma zaidi kugombania nafasi ya kucheza.
 
Pia kwa wale dada zetu wapenda urembo, wasio penda mikunjo kwenye ngozi zao za usoni ,chunusi na wanaotaka kuonekana warembo mda wote, watumie parafu kupitisha kwenye nyuso zao .
 
Mechi ni nyingi mno kuliko zamani, na siku hizi wanajituma zaidi kugombania nafasi ya kucheza.

Hata zamani match zilikuwa nyingi.

Michezo mingine pia tofauti na soka wachezaji wanaumia zaidi. Basketball ya sasa ni rahisi kuliko 80s or 90s na number of matches ni almost zile zile ila nao wanaumia kila siku.

Kuna uwezekano over dieting na hizi physiotherapy zinafanya wawe weak in the long term kuliko kuwasaidia.
 
Umeelezea kwa making na kwa ufasaha sana jinsi gani nguvu inazalishwa mwilin...
Lakin kuna sehemu umewapotosha wasomaji....
Swali langu nauliza ...wachezazi wanaingiaga kwenye mapipa ya mabarafu baada ya mechi tu kuisha...iweje kwenye mechi watumie energy na nguvu kubwa alafu waje waingizwe kwenye mabarafu wazalishe tena nguvu....
Bado itakua aujajibu kwanin wachezaji wanaingizwa kwenye yale mapipa
 
Unaujua usingizi vizuri lakini šŸ˜‚

Sikupingi itafanya kazi lakini sio never sleep, usingizi ni nyoko mzee.
 
Pia kwa wale dada zetu wapenda urembo, wasio penda mikunjo kwenye ngozi zao za usoni ,chunusi na wanaotaka kuonekana warembo mda wote, watumie parafu kupitisha kwenye nyuso zao .
Maji ya moto yanaichosha ngozi yaepuke usoni.
 
Kuna tear and were kwa wachezaji, Njia pekee ya kuzalisha mitochondria kwa haraka ni kwa njia hii ya barafu, tear and were za viungo ni kwa misosi mizuri kulingana na mahitaji ya mwili. Kaka unapingana na sayansi au wape sayansi ya kwanini waingie kwenye mabarafu.
 
Mimi nilijika kwenye faida Wewe waelemishe hasara zake.
 
Leo nimeangalia mechi ya Chelsea na Manchester United ya mwaka 2001,nimejifunza kua Zamani wachezaji hawakua Fit Kama Sasa,hawakimbii Sana..hawakutani Sana Kama Sasa... now mpira wa kutumia nguvu Sana na kukimbia Sana..hata aina ya training now tupo level kubwa Sana so wachezaji kuumia lazima..
 
Siku hizi nafasi ya kuonyesha kipaji ni ndogo sana, mchezaji ww sasa anatakiwa amridhidhe kocha kwa kucheza kama kocha alivyomuagiza acheze. Hatari ya kuonyesha ufundi wako kama makudubela hapana, utakaa benchi. Mtu kama kibadeni na Sunday manara Leo hii wasingepata namba kwa kocha.
 

Kusema walikuwa hawakimbii sana maybe ila walikua rough na refs didn't bat an eye sio kama sasa hata ukimuangalia mwenzio vibaya tu unapewa card.

Unakumbuka battle ya Vieira na Keane? Seedorf vs Edgar Davids? CDM roho mbaya Gattuso, slide tackle za Maldini. Nani anacheza hata robo yao ya level yao hivi sasa? Ukiondoa kizazi cha kina Ramos na Pepe wanaofuata wote ni divas tu.
 
Asante sana nilikua sijui kwanini wachezaji wanaingia kwenye mabarafu wakimaliza mazoezi.

Rai kwa wataalamu wetu kwenye kila nyanja tuanze kufanya haya mambo sisi wenyewe kuliko kusubiri wazungu wafanye halafu sisi ndio tuanze kuelezea theory zao.

Hii ishu ya wachezaji kuingia kwenye barafu kibongo bongo nimeanza kuona miaka ya karibuni ukilinganisha na wachezaji wa ulaya ambao nimeona wakifanya ivyo mida mredu kidogo.

Tufanye tafiti, tuhoji na tuje na gunduzi zetu ili wazungu nao waje kujifunza kutoka kwetu.
 
Anaudhoofisha mwili wake vibaya sana, ni hatari mno kwa mwili hata uzazi. Usiende. Kama unaweza oga maji ya baridi utajisikia nguvu nyingi baada ya kuoga. Ndio maana wanaoishi sehemu za baridi Wana uwezo mkubwa wa kutenda na kufikiria.
Hizi sasa fix
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…