Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Bi faiza shikamoo/za muda huu/ haujambo?

Acha na mimi nikuulize.
Hivi ndoa ya kwanza Tangu kuumbwa kwa ulimwengu ilikuwa ya nani na nani? Ilizingatia vigezo gani na ilifungishwa na nani?

Iliitwa ndoa au hili jina limekuja kutumiwa leo?

(Chimbuko la ndoa)
 
Watakujibu watu wa "sunna".

Binafsi salat zilizoainishwa kwenye Qur'an zinanitosha.
Uislam halisi ndio huwa wa sunna za Mtume unazokataa.

Answaar sunni are really muslim

Ni bora BALUKTA ipate nguvu kuliko ninyi wa BAKWATA bin CCM


Wabillah Tawfiq,
 
Bi faiza shikamoo/za muda huu/ haujambo?

Acha na mimi nikuulize.
Hivi ndoa ya kwanza Tangu kuumbwa kwa ulimwengu ilikuwa ya nani na nani? Ilizingatia vigezo gani?

Iliitwa ndoa au kuna hili jina limekuja kutumiwa leo?

(Chimbuko la ndoa)

Katika Uislam tunaamini Adam ni mtu wa kwanza na wote tuliobaki tunaitwa binaadam (bin Adam) kwa kuwa tumetokana na kizazi cha Adam.

Kuoana (to become a pair) au kwa Kiarabu "zawaj" (pair) kulianzia kwa Adam na Hawa pale Allah alipoamua kumpatia Adam "pair" yake.

Qur'an 4:1
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.

Qur'an 2:35
Na tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio dhulumu.

 
Ooouh, ubarikiwe.
 
Uislam halisi ndio huwa wa sunna za Mtume unazokataa.

Answaar sunni are really muslim

Ni bora BALUKTA ipate nguvu kuliko ninyi wa BAKWATA bin CCM


Wabillah Tawfiq,
Qur'an 6:19
Sema: Kitu gani ushahidi wake mkubwa kabisa? Sema: Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye shahidi baina yangu na nyinyi. Na nimefunuliwa Qur'ani hii ili kwayo nikuonyeni nyinyi na kila inayo mfikia. Ati kweli nyinyi mnashuhudia kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu wapo miungu wengine? Sema: Mimi sishuhudii hayo. Sema: Hakika Yeye ni Mungu mmoja tu, nami ni mbali na mnao washirikisha.
 
1. faiza foxy maandishi yako meng yanaonesha unawachukia wakristo, kwani walikufanya nin? Au dini ya uislam unawahimiza kuwachukia wasio waislam?

2. Unadhani uislam utakufikisha peponi? Kivipi?

3. Kuna uhusiano gan wa uganga wa jadi na quran?

4. Inasemekana hukuwahi kupata elimu rasmi ya dunia (formal educatiön) uliishia madrasa, ni kweli?
 
mnakimbia shule then mnasingizia mfumo#stupid
Umesahau mfumo wa kielimu uliokuwa unawabagua waislam? Usijifanye kipofu. Mwislam akiteuliwa kushika nyadhifa serikalini mnapiga kelele kuwa kapendelewa au kateuliwa kwa udini....ila mkristo akiteuliwa mnasema kateuliwa kwa sababu ya qualification zake. Kwani huyo mwislam kasoma shule gani mpaka msizione qualifications zake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FaizaFoxy nakuongezea swali

UMESEMA NDOA YA KWANZA NI KATI YA ADAMU NA HAWA.. NI DHAHIRI KUWA MWENYEZI MUNGU ALIMPA ADAMU MKE MMOJA

1. SASA KWANINI NYIE WAISLAM NA MTUME MMEJIPA RUHUSA YA KUOA WAKE HADI WANNE?
 
Naona malalamiko tu.....hoja hamna!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oh now nimekupata... Wew n ktk makund potofu linalojiita quraniyun wanaokataa hadith za mtume bila shaka umeshakufuru na s muislamu
..sabb miongon mwa vitenguz vya uislamu n kuchukia yale alokuja nayo mtume kama hivi hadith..... Ila nataka nkuulize...... Allah ktk quran anasema tusimamishe swala... Wala hakuelekeza io swala iswaliwe vp.... Swal langu umejuaje ka swala ya adhuhur ina rakaa nne na inaswaliwaje... Na subuh na ishaa je ikiwa una kataa hadith... Kuswal umejuaje ispokuwa mafundsho ya mtume ktk hadith??



Sent using Jamii Forums mobile app
 
1) Umenihukumu pasi na ushahidi. Sina chuki na binaadam yoyote yule.

Naomba nionyeshe hayo maandiko yangu yaliyokufanya wewe ufikirie kuwa nnachuki na Wakristo. Ukishindwa basi elewa kuwa umejenga hisia za chuki pasi na sababu.

Uislam ni dini ya walimwengu wote labda uwe haufahamu tu maana ya Uislam na maana ya dini.

Uislam ni kujisalimisha na unyenyekevu (submission) kwa aliye kuumba wewe na aliyeumba vyote vilivyomo kwenye ardhi na mbingu.

Jee wewe hujisalimishi na kumnyenyekea aliyekuumba?
 

Umeshanipachika majina lukuki na kunihukumu kuwa si Muislam halafu unaniuliza kuhusu sala?

Hivi mafundisho hayo ndiyo ya sunna?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…