Kwanini Quran inakusha yaliyo katika biblia?
Ililetwa ili ikanushe biblia?
Napata shaka kwamba ilishushwa!!
Yesu aliungama kuwa hakuyasema yote aliyoyataka kuyasema, lakini huyo atakaye kuja yeye ndiye ataitimiza kazi. Mafunzo ya Muhammad juu ya dhambi, juu ya kuhisabiwa haki, na juu ya hukumu yamo katika Qur'ani, kitabu cha namna ya pekee ulimwenguni kwa usafi wake, kutokuwa na migongano yo yote na kuwa hakiwezekani kuigwa mfano wake. Tangu kilipoteremka kwa Mtume s.a.w. miaka 1400 iliyokwisha pita hakikubadilika hata kwa neno moja, na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, hakitobadilika mpaka Siku ya Kiyama. Sir William Muir, mtoa kombo maarufu wa Uislamu, akiandika katika kitabu chake
The life of Mohamet (Maisha ya Muhammad) amesema:
"Labda hapana kitabu cho chote kinginecho duniani ambacho kwa muda wa karne kumi na mbili kilichobaki na maandiko yake safi namna hii."
Tangu Sir William alipoandika hayo karne mbili nyenginezo zimekwisha biringita na Qur'ani imebaki vile vile safi kama siku alipoipokea Mtume Muhammad s.a.w. kwa Mwenyezi Mungu.
Kwa mintaraf ya Biblia lakini hatuwezi kuona msimamo mmoja, kwa sababu kwanza kuwa Biblia si kitabu kimoja, bali ni mkusanyiko wa vitabu vingi vilivyoandikwa na watu mbali mbali, katika zama mbali mbali. Makanisa yanazozana hata kuwa vitabu vipi vikubaliwe kuwa ndio Biblia, na vipi sivyo, vipi vimeandikwa kwa msaada wa Roho Mtakatifu na vipi sivyo. Mara nyingi inatokea katika kitabu kimojawapo hicho hicho kinapingana wenyewe kwa wenyewe, kama tulivyokwisha ona mfano wake katika hadithi ya kutanasari Paulo iliomo katika kitabu cha Matendo ya Mitume.
Hugh Schonfield akiandika katika kitabu chake
Those Incredible Christians, anasema:
"Ndani ya jalada za Biblia twaweza kukuta udanganyifu, mageuzo, na uzushi wa kukusudia kamaunavyokuta katika vitabu vyenginevyo nje. Wataalamu wanajua vyema haya; lakini inapokuwa andiko la ndani ya Biblia si la huyo anayedai kuwa ndiye muandishi kila juhudi inafanywa lisitumiwe neno udanganyifu. Hali ni hiyo hiyo kwa maneno anayoambiwa Yesu kayasema na yanajuulikana kuwa si kweli. Tunaviita vitabu kama hivyo kuwa ni vya kikundi cha mawazo ya Kipaulo au Kipetro, na maneno yaliyogeuzwa au yaliyozuliwa tunayaita kuwa ni "ya pili"(Secondary). Kama hatukutumia hila itaonekana kuwa Roho Mtakatifu alishirikiana katika udanganyifu.Ni jambo lililoandikwa na kujuulikana kuwa mpaka ilipokatwa shauri mwishoe vitabu gani vihisabiwe kuwa ni Maandiko Matakatifu baadhi ya vitabu viliomo katika Biblia vilipingwa. Ilitolewa hoja na Wakristo wa kweli kwamba vitabu fulani havikuwa hakika vimeandikwa na hao wanaodaiwa kuwa ni waandishi wake. Pengine jina la mwenye kufanya udanganyifu lilidhukuriwa. Paulo anataja wakati wa uhai wake zilikuwepo barua za uwongo zikienezwa kwa jina lake yeye. Liliokuwa laonekana lafaa ni maslaha ya Kanisa tu. Mawazo yasiyokhusiana hata chembe na ukweli yakitumika kuelekeza maandishi na fikra kinyume na hakika ya walivyosema wenyewe watu kadhaa wa kadhaa wenye maana. Mtindo kama huu ulikuwa ni jambo la kawaida katika kazi ya uenezi hapo kale, na yafaa tuelewe kuwa ilikuwa ni kawaida vile vile miongoni mwa Wakristo wa zamani. Hivi ndivyo mchezo wa kueneza na kupendekeza ulivyokuwa ukichezwa. Na kwa wale wasio na dhamiri wala haya, wanaoamini kuwa muhimu ni lengo sio njia uitumiayo, mchezo huo unachezwa hata hivi sasa."
Asli ya vitabu vya Biblia haipo na haijuulikani, kwa hivyo ndio tunapata nakala nyingi sana. Inakubaliwa kuwa vitabu hivyo kama vilivyo sasa vimeandikwa na waandishi wanaadamu. Juu ya hivyo waweza kugundua baadhi ya maneno ambayo yametokana na Mungu asli yake. Lakini jinsi maandishi yalivyochanganyika, na yalivyoongezwa na kupunguzwa hata inakaribia kuwa ni muhali kulitambua lipi la Mungu na lipi la mwanaadamu ambaye alikuwa anawania madhehebu yake fulani au wazo lake maalumu. Qur'ani ni kinyume cha hayo. Kila neno lake ni la mwenyewe Mwenyezi Mungu. Yote ni maneno yake Mola Mlezi kama alivyofunuliwa kwa ufunuo (
Wahyi) Mtume s.a.w., neno kwa neno, na yeye Mtume akiyatamka na wenye kuhifadhi kwa moyo wakihifadhi, na waandishi waaminifu wakiandika. Mkristo, Dr. John B. Taylor, Mwalimu wa Masomo ya Kiislamu katika Selly Oak Colleges, Birmingham anaandika katika kitabu chake
Thinking About Islam:
"Tumekwisha hakikisha kwamba Waislamu hawasemi kuwa Muhammad kaandika Qur'ani, lakini kuwa kaipokea na akaisoma. Kama alivyokuwa Muhammad mwenyewe alivyoishughulikia matini ya Qur'ani, vile vile Waislamu wa baada yake walichukua kila taabu kuuhifadhi kwa ukamilifu usafi wa vipande vyote vya Qur'ani. Miaka miwili tu baada ya kufa Muhammad, na kuwa baadhi ya wale waliokuwa wameihifadhi Qur'ani kwa moyo, wakifa vitani, vipande mbali mbali vilikusanywa...Miaka michache baadaye, katika enzi ya Uthman, Khalifa wa tatu kuwatawala Waislamu baada ya kifo cha Muhammad, matini ilipitiwa tena kusahihishwa. Twaweza kusema vipi wale Waislamu wa kwanza walivyoshughulikia na kuwa na hamu kwa kuwa hata khitilafu za matamshi ya pande mbali mbali za ulimwengu wa Kiislamu hazikuruhusiwa katika kuisoma Qur'ani; na kwa hivyo matini rasmi ikahakikishwa inayofuata lafdhi ya Makka, na nakala nyenginezo zote ziliteketezwa kwa amri ya Khalifa. Kwa hivyo tunaweza kuwa na imani ya yakini kuwa hii Quran tuliyo nayo hii leo kama inavyomkinika kibinaadamu ndio ile ile iliyohakikishwa mnamo miaka michache tu baada ya kufa Mtume."
Hayo ni maoni ya mtoa kombo wa Kikristo. Qur'ani ni neno la Mwenyezi Mungu lisio na toa. Hiyo ndiyo maana ya maneno ya Yesu aliponena: "
Hatanena kwa shauri lake mwenyewe lakini yote atayoyasikia atanena."
Soma zaidi:
http://www.quranitukufu.net/Biblia/index.htm