Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Kwa nini viumbe "majini" yanatumia majina ya Kiislamu? Mfano: Fatuma, Maimuna, Makata n.k.
Usije kumuamini kiumbe kinachoitwa Jinni hata siku moja. Waongo balaa, atakuja kwa sura ya Fatma wakati yeye ni Zwangedaba. Alafu makata ni jina la asili ujue !!.

Joke aside, Majinni au mapepo au kwa kiingereza Genie (Refer: if you want to be with me, there's some price to pay, am a genie in a bottle...) ni viumbe vilivyopo, wameumbwa kwa moto na wana advantage ya kutuona wakati sie bin Adam hatuwaoni.

Wamekuwepo duniani kabla ya bin adamu, kwa kuwa binadamu ndie kiumbe cha mwisho kuumbwa.

Kisheria, majinni wanapaswa kuishi kama wao katika communities zao, na ni makosa kwao kuwaingia binadamu na kuwasababishia madhara mbali mbali.

Na hapo ndipo tunapoambiwa kuwa Jinni anapokuwa mwema basi si Shetani na binadamu anapokuwa muovu naye huitwa Shetani kwa kuchukua yale matendo ya kishetwani.

Binadamu Mcha Mungu ana fadhila zaidi kuliko Kiumbe kingine chochote, na kwa ucha Mungu huo Nabii Suleiman kwa mfano alipewa uwezo wa kutawala jeshi kubwa la majinni waliokuwa watiifu kwake na waliomtumikia kwa kila jambo.

Back to your question, Uislamu ni dini iliyoshushwa kwa binadamu na majinni. Kama isemavyo aya kuwa 'Mwenyezi Mungu amewaumba binadamu na majinni ili wamuabudu.' Wale wanaomuabudu watakuwa ni waislamu kwa kuwa wamejisalimisha na kunyenyekea kwa Mola wao na wale wasioabudu si Waislamu. Hivyo hautamuona Jinni mwenye kuabudu akimuingia binadamu ili amdhuru, lakini utawaona wale wasioabudu wakifanya hivyo na kujiita majina wayatakayo wao ili ku create confusion.
 
sasa mnapopata div zero mnalalama kwa necta MNA akili?
pateni degree za judo mukome kulalamikia necta elim elim elim
Unaonaje kwa mfano Tanzania kama nchi ingerasimisha michezo kama Judo, Karate na basketball ikawepo mashuleni na ktk mashindano ya kimataifa kama Olympic Watanzania wenzako wanaenda kuiwakilisha nchi na maybe wakarejea na [emoji471][emoji471][emoji146][emoji146]. Huoni kuwa in the long run ingekuwa ni chanzo kingine cha ajira na ingetupunguzia tatizo kwa wale vijana ambao wana Degree na hawana wa kuwaajiri?
 
Nakubaliana nawewe kamanda 100%. Respect kwa bibi yangu tumu. Mungu ampe umri mrefu na taqwa.
 
habar Dada Faiza F. nahsi uko powa, Nilikuwa naomba tofauti kati ya "Scholarship" na "Sponsorship" , na ntaweza vipi kupata sponsor ya kwenda kusoma abroad huwa watu wanapata vipi?
 
habar Dada Faiza F. nahsi uko powa, Nilikuwa naomba tofauti kati ya "Scholarship" na "Sponsorship" , na ntaweza vipi kupata sponsor ya kwenda kusoma abroad huwa watu wanapata vipi?

Wanajamvi tujuzeni tafsiri ya Scholarship Kiswahili.
 
habar Dada Faiza F. nahsi uko powa, Nilikuwa naomba tofauti kati ya "Scholarship" na "Sponsorship" , na ntaweza vipi kupata sponsor ya kwenda kusoma abroad huwa watu wanapata vipi?
Nijuavyo scholarship hutolewa na vyuo au serikali yetu au ya wahisani kwa wanafunzi waliofanya vizuri ili waendelee na masomo ya juu.

Na Sponsorship ni udhamini ama ufadhili wa aidha taasisi, watu binafsi, ndugu, jamaa, marafiki, wahisani. Au mtu ajitolee sadaka yake kukuwezesha kusoma.

Kuna taasisi huwa zinatowa Sponsorship lakini kwa sasa sizijuwi za Tanzania, ntafanya utafiti.

Kuhusu Scholarship anzia wizara ya elimu ukapate utaratibu na vigezo na pia ulizia kwenye balozi za nchi wahisani hata kwa kuwaandikia tu .
 
Too good to be true
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…