Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Bi mkubwa katika uislam kuna vitabu ndani ya Biblia Takatifu mnavyoviamini Torati na Injili sasa katika hayo kuna Maandiko yameandikwa Mtu asiape na amelaaniwa mtu yule anaeapa chini ya ardhi maana hapo ndipo ninapoweka miguu yangu kama ikitokea mtu akiulizwa na aseme ndio au sio na sio kuapa kwa sasababu mimi Mungu ni mwenye wivu na huwapatiliza wana maovu ya baba zao sasa nataka nijue kipindi cha uchaguzi tunapita mapito mengi wapo wanaokuwepo pale kwa ushindi wa ulaghai wengine dhulma mwisho wa siku anakuja mtu tena bila hofu ya Mungu anashika Biblia Takatifu , Quran Tukufu na kuapa chini ya ardhi tena kwa binaadamu mwenzie huku katika nafsi yake akijua wazi ushindi alioupata umepitia mapito mengi yasiyo halali na hata akimaliza kuapa anafanya kinyume na kile alichokiapa pale mbele ya umma wa watu na je hii si laana ya ardhi juu ya nchi?


Nnakusihi hebu, weka para na liandike swali lako upya kwa kituo, maana nnahisi kama nimelijibu tayari. Labda kuna swali zaidi ya moja hapo?
 
Alama Mohamed Said ni kaka yangu, si kwa kuzaliwa bali kwanza kwa Uislam, pili ahli zangu karibia wote anajuana nao, tatu mimi mwenyewe ananijuwa fika, kasoro ni hizi pen name tu za humu JF, lakini siku nikimwambia ndiyo mimi, atacheka na kushangaa sana. Nne, mitaa aliyokulia yeye ndiyo niliyokulia mimi na kwa aijuae Dar ya enzi hizo, hususan mitaa ya Kariakoo, Gerezani na Jangwani, tuliishi kama one big family. Tano, kwa umri wake, Alama ni mchezo mmoja na kaka zangu na wajomba zangu halisa kabisa na ni marafiki zake sana. Sita, tumeoleana katika ndugu jamaa na marafiki wa kwenye ukoo. Saba, amenifundisha mengi kuhusu historia ya nchi yetu kuliko mwengine yeyote yule. Nane, awajuao yeye wengi mno nami nnawajuwa fika, Tisa, Ana heshima kubwa sana hata katka majibu yake tu utaliona hilo.

Tuwachie hapo kwenye "witr".

Kwa hayo, nadhani umeuona uhusiano tulio nao.
Sawa bana...nimeinua mikono juu.
 
Bi Faiza we ndo mke pekee kwa mme wako.. Au mpo zaid ya mmoja.. Na kama Ndio ulijiskiaje alipoongeza mke mwingine.

Ukizungumza binafsi bila kuegemea kwenye dini.. Suala la mke zaid ya mmoja unalisemeaje
 
Bi Faiza we ndo mke pekee kwa mme wako.. Au mpo zaid ya mmoja.. Na kama Ndio ulijiskiaje alipoongeza mke mwingine.

Ukizungumza binafsi bila kuegemea kwenye dini.. Suala la mke zaid ya mmoja unalisemeaje


Mimi ndiyo mke pekee.

Suala la zaidi ya mke mmoja siwezi kuliongelea zaidi ya kwenye dini yangu ya Kiislam, nnaomba soma hii: Nini Hikma Ya Kuoa Wake Zaidi Ya Mmoja? | Alhidaaya.com
 
Rais wa Marekani Donald Trump alitoa msimamo wake wakati wa kampeni kuhusu mpango wa kuwazuia Waislamu kuingia Marekani kwa muda ................... toa maoni yako.
Nataka nione kwanza atawafanya nini' white american muslims'
 
Hujajibu swali langu nililokuuliza laana ya kuapa chini ya ardhi ndio inayotumaliza usikwepe jibu kiufasaha hata ndani ya Biblia imeandikwa usipunguze nukta wala neno lolote ndani ya Bliblia

Hilo la Biblia mbona nimekujibu? Au hujaelewa hili jibu, rudia kusoma tena:

Waislam tunaamini katika Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an.

Tunasema kama kuna Old testament na new testament basi Qur'an ni final testament.

Unajuwa Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi na kuna madhehebu mengine ya Wakristo kuna vitabu vingine vya biblia hawaviamini kabisa.

Pia hakuna ubishi kuwa kuna watu wanakaa na kuamua hiki kiongezwe, hiki kiondolewe, hiki kibadilishwe. Ndiyo sababu kubwa ya kuwa na versions nyingi sana za Biblia. Kumbuka versions, siyo translations.

Sisi tunaamini kuwa humo humo kwenye mkusanyiko wa hivyo vitabu kuna maneno machahe sana yamebaki kuwa ni kweli mafundisho ya Mwenyeezi Mungu. Na yale ambayo si ya Mwenyeezi Mungu na ni mikono ya watu tu ndiyo mengi zaidi.

On the other hand, Qur'an toka imetujia miaka zaidi ya 1,400 iliyopita haijabadilishwa na haitoweza kubadilishwa kwa sababu Allah ameahidi kuilinda, cha ajabu ni kuwa katupa uwezo sisi wenyewe wa kuilinda. Hakuna kitabu leo hii duniani kilichohifadhiwa kwenye mioyo ya watu kama Qur'an. Kama kipo nijulishe. Jee, kwanini?


Hili la "laana ya kuapa" nnaomba niwekee reference (quotations) ya hivyo viapo ili niione "context" ya unachouliza.
 
Maana sahihi ya hadithi ya Mtume alipotaja kuwa mwanamke huolewa kwa sifa hizo nne ni;
Kwa kawaida mwanaume huvutiwa na kutamani hadi kufikia kuoa mqanamke akiwa na moja ya sifa hizo.
1. Ni mzuri wa sura,umbo(uzuri wake)
2. Mali anazomiliki (mali zake)
3. Awe ametoka kwenye familia mashuhuri. Kwa utajiri,uongozi,busara nk.(kwa nasaba yake)
4. Au awe mcha Mungu. Mwenye maadili na tabia za kidini.(kwa dini yake)

Kisha akatusisitiza kati ya hao wanne mke bora ni yule mwenye dini. Iwapo utampata mwenye dini utakuwa umefaidi.
Si maana ya hadithi kuwa,awe na sifa hizo nne bali sifa hizo zimetajwa kuonesha kuwa ndizo humpelekea mwanaume kuvutiwa ikiwa mwanamke atakuwa na moja ya sifa hizo.
Kwa muislamu unatakiwa kuangalia dini.

Iwapo utampata mwenye dini kisha mrembo sawa.
Ana dini kisha tajiri,sawa.
Ana dini kisha anatoka kwenye ukoo bora pia ni vizuri.
Akiwa na sifa zote nne ni bora zaidi.
Muhimu hapo ni dini
Asante Sana mkuu, umenitoa tongotongo
 
Ni kweli kabisa, labda nilikuwa sijakuelewa lakini baada ya ufafanuzi wako nimekuelewa, nnaomba pitia hapa uone Rense anasemaje: Absolute Proof More Modern Jews Not Biblical Israelites
FaizaFoxy, asante ila am sure umenifanyia kazi ambayo hujui uthamani wake. Lingine kama hautajali, Mimi ni Mfuasi mzuri sana wa Hon. Minister Louis Farrakhan, Dr. Khalid Mohammad, Elijah Mohammad (Nation of Islam). Huwa sipitishi siku bila kusikiliza clips zao kupitia youtube. Swali, je wewe unakubaliana nao kuhusu mawazo yao??? siku moja wasikilize kama bado hujawasikiliza (Jibu lisiwe ndiyo, ukii elaborate utakuwa umenisaidia)
 
Unamfahamu Salman Rushdie? Nitajie jina la kitabu kimoja tu alichoandika.
 
FaizaFoxy, asante ila am sure umenifanyia kazi ambayo hujui uthamani wake. Lingine kama hautajali, Mimi ni Mfuasi mzuri sana wa Hon. Minister Louis Farrakhan, Dr. Khalid Mohammad, Elijah Mohammad (Nation of Islam). Huwa sipitishi siku bila kusikiliza clips zao kupitia youtube. Swali, je wewe unakubaliana nao kuhusu mawazo yao??? siku moja wasikilize kama bado hujawasikiliza (Jibu lisiwe ndiyo, ukii elaborate utakuwa umenisaidia)


Nimewasikiliza sana tu na nnaendelea kuwasikiliza, mengine nnakubaliana nao na mengine sikubaliani nao. Simply ni different schools of thought tu.

Kama unawasikiliza hao, msikilize na Blagrove, ingawa si Muislam lakini to me he makes a lot of sense nikimsikiliza:

 
Unamfahamu Salman Rushdie? Nitajie jina la kitabu kimoja tu alichoandika.


Simfahamu bali nimemsikia sana tu na kumuona kwenye mtandao, nnajuwa kuwa kaandika kitabu alichokiita satanic verses.

Wewe unamfahamu?
 
Hivi unaamini nini katika suala la kusema fulani ana "nyota kali".

Je,mafanikio ya mtu ni bidii zake mwenyewe au kudra tu za Mungu?

Na kama muumba anajua yote si inamaanisha kuwa fate ya mtu tayari iko pre-destined
 
Mmmmmh sina Uhakika ebu tujuze..

Naamin bibilia pia imesema hivyo..


Nioneshe wapi biblia imesema hivyo.

Halafu unaonesha link niliyokuweka hujaisoma. Jisomee:


Qur'an 4:
3. “Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu...” An-Nisaa: 3
 
Back
Top Bottom