Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa



Hiyo hapo...
 
Soma Timotheo 1-1:2
 


Sasa kijana hapo ndiyo kuoa mmoja tu? Hicho ni kisa cha Adam na hapo ni mambo ya kimwili, hebu kisome vizuri.

Biblia kuhusu kuoa zaidi ya mmoja inasema hivi:

Kutoka 21:
10 Kwamba ajitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.

2 Samweli 5
13 Naye Daudi akazidi kujitwalia masuria na wake huko Yerusalemu baada ya kutoka Hebroni; wakazaliwa zaidi kwa Daudi wana na binti.

1 Wafalme 11
3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.
 
Ught Faiza hivi ulishawahi kusoma kitabu cha "Secret terrorist"? Unaweza kuyaelezeaje yaliyomo ndani
 
Hivi unaamini nini katika suala la kusema fulani ana "nyota kali".

Je,mafanikio ya mtu ni bidii zake mwenyewe au kudra tu za Mungu?

Na kama muumba anajua yote si inamaanisha kuwa fate ya mtu tayari iko pre-destined

Siamini hayo mambo ya "Nyota Kali" ni katika mambo ya ramli ambayo Uislam unakataza.

Mafanikio ya mtu ni kutoka kwa Mwenyeezi Mungu na bidii ya mtu. Mtihani.

Kuhusu "predestined" ni ilm ndeeefu na ina maelezo mengi sana. Naam, kwa maana hiyohiyo, Allah ni mjuzi wa yote na si sisi.

Nnakushauri pitia mjadala huu, kuhusu hayo: Is everything predestined in a muslim's life?
 
Sina chuki na Joyce Ndalichako bali nnauhakika si kiongozi mzuri, alivurunda kama mkuu wa NECTA mpaka baadhi ya Waislam wa Tanzania wakaandamana kumkataa. Jikumbushe:

Tatizo dada yangu unajua nini hapo??,Ukweli ni kwamba ninyi wenzetu huwa mnaweka nguvu nyingi kwenye kujifunza Quaran kuliko masomo mengine ya darasani halafu kwenu ninyi nasikia ni heri mtoto afeli masomo mengine kuliko kufeli Elimu ya Kiislamu.Kwa hiyo huna sababu ya kumchukia Prof.Ndalichako,maana kwa mtindo huo lazima madogo wafeli tu.
 


Nnakuomba pitia hapa, kuna mjadala kuhusu hilo: Waislam wa Tanzania na tatizo la udini katika Wizara ya Elimu
 
Yaani kama kweli we ni muislam ,,, nimekukubali kwa majibu yako hata kama umenidanganya lakini maelezo yako yamenyooka. Wengine ukiwauliza wanakuwa na jazba ila wewe umekubali kwamba waislam wana undugu na majini - rejea usemi huu ... "MUISLAM NDUGUYE MUISLAM"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…