Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Tufafanulie kidogo, "Khilafa" ilianzishwa na nani? Na ilikuwaje ikatoweka? Sijaiona toka nizaliwe.

Mimi nijuavyo, binaadam sote ni ma Khalifa.
Daulat Islamiya, usiangalie eti tangu hujazaliwa hujaona hiyo sio pointing kabisa , angalia historian ya uislam tangu zama za Mtume swalalahu alayh wassalaam , pia lazima utambue kwamba sio kila anayejiita muislam basi yupo ktk njia sahihi wakati fikra Na mienendo ya kiislamu haifuati Na lazima ujiulize ni kwann Siku ya hukumu waislam watakuwa wamegawanyika ktk makundi 73 km sijakosea Na kati ya hayo moja tu ndio kitakalo salimika , je unafikiri ni kundi gani? Ukirudi ktk Quran Na hadithi za mtume bila shaka utakuwa ndio nusra ya muislamu Siku hiyo Na je ndani ya Quran Na Sunna kuna sehemu utawala wa kidemokrasia umehalalishwa? Bila shaka hakuna hivyo demokrasia ni haramu Na Allah kaahid kabla ya kiama kusimama dola ya kiislamu itakuja kusimama tena
 
Kwanza kabisa hongera sana FaizaFoxy wewe ni mmoja ya member wa JF ninaowakubali sana kwa kujenga hoja na uvumilivu hapa JF,nakumbuka huko nyuma ulipigwa ban tukakuombea kwa Mod wakufungulie,Maswali yangu

1.Unafikiri vyama vya siasa vya upinzani vinakosea wapi ili kuiondoa CCM ?

2.Tanzania ni maskini licha ya rasilimali nyingi tulizonazo na wanasiasa wanatudanganya kila wakati wa uchaguzi,kwa mtazamo wako ni mambo gani tunapaswa kuyapa kipaumbele ili tuweze kusonga mbele ?

3.Umekuwa mmoja ya watu ambao mnalalamika sana waislamu wananyimwa fursa kwenye teuzi mbalimbali za serikali,huoni kama chanzo cha tatizo ni kwamba waislamu hawajaweka kipaumbele kwenye elimu dunia na pia wamekuwa hawana umoja kama walivyo wakristu ?
 
Tusiharamishe ambayo Allah hajaharamisha.

Khilafah sijaisoma popote kuwa ilikuwepo wakati wa Mtume Muhammad Salla Allahu Alayhi Wasalaam. Nnaelewa ilikuja baada yake.

Qur'an inasema sisi ni Ma Khalifa. Hulikubali hilo?
 
Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.
Naam, vyema sana. Sasa malizia ulichoandika na kuninukuu ni wapi nimesema nisiulizwe.
 
Mungu anapongea hutumia nafsi ya kwanza uwingi(sisi) , wala hajinati kwa nafs ya kwanza umoja (mimi). Pia refer suratul kauthar
"Hakika tumekupa kheri nyingi sana ewe Muhammad (s. a. w) "
Cjaridhika na Jibu hili..
Una umejibu swali moja la pili Vp.. Tupe shule.
 

1. Refer to post #11
2. Pwani na Dar akiwa Tanzania.
3. Ni mwanamke, haoleki na hajaolewa bali ameoana na mumewe kwa miaka takriban 38 sasa, AlhamduliLlah.
4. Hatawaliki wala hatawali ni "mutual consent" baina yake na mshirika wa maisha yao "shirkatil hayaa".
5. Ameonelea sadaka mojawapo ni kugawa ayajuayo na amejikita zaidi kwenye hilo kwa sasa.
6. Bado ni mwanafunzi kwa ilm zote na anajifunza kila kukicha.

Ahsante kwa mengine yote.
 

Faizafoxy, je mtanzania yeyote anaweza kwenda kubadilisha pesa za kigeni BOT kwa rate zile zile zinazooneshwa ktk website ya BOT kila siku?
 
= majinni

"majini" ni kwenye maji.
Ibrahim Kauli,na wewe acha kupotosha watu kuhusu utamkwaji na uandishi sahihi wa neno MAJINI.Kwa mujibu wa kanuni za sarufi maumbo na matamshi neno MAJINI linatakiwa liandikwe kama hivi nilivyoandika bila double N,yaani ni makosa kuandika MAJINNI kwa kutofautisha maji na mapepo.Sarufi matamshi na maumbo kwa kutumia KIIMBO neno moja linaweza kuleta maana nyingi kutokana na kupanda na shuka kwa kutamaka baadhi ya silabi.Km Barabara ukitamka bila kupanda utakuwa una maana ni njia ya magari,eg ajali nyingi zinatokea kwa sababu barabara ni mbovu,na ukitamka kwa kupanda na kushuka utakuwa na maana ya sawa sawa e.g. umempiga barabara yaani umempiga sawa sawa.Vivyo hivyo MAJINI ukitamka bila kupanda utakuwa una maanisha maji ya kuoga au kunywa,lakini ukitumia KIIMBO yaani utamke kwa kupanda na kushuka utamaanisha mapepo.Kwa hiyo kwenye Kiswahili fasaha hakuna neno Majinni.
mnafundishana karate ndii mtegemee mtafaulu? endeleen kusubiri meli airport
 
Samahani kumbe alietokota kwa kuchapia ni Faiza foxy na sio Ibrahim.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…