Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa



Umejifundisha Kiswahili shuleni, nimezaliwa na Waswahili, Kiswahili ni lugha mama kwangu na Jinni, si neno ni jina (noun).
 
Asante ff kwa kunijibu
 
Nadhani unachokifanya hapa hujibu hoja bali unatoa vihoja ili thredi ifikishe pg elfu 10.


Nnaona umeshindwa kunukuu uongo ulionizulia sasa unakuja kubwabwaja na kuhororoja bila mpango.

Na wewe roho inakuuma kwa mimi kujaza page? Kama unaweza panda juu nenda ukazibe.
 


FaizaFoxy ,nasubiri majibu
 
sawa mkuu nimekuelewa ila umeelewa maana ya post yangu
 
Umejifundisha Kiswahili shuleni, nimezaliwa na Waswahili, Kiswahili ni lugha mama kwangu na Jinni, si neno ni jina (noun).
Kwa hiyo noun si neno?Tafadhali rejea kamusi ya Kiswahili utapata usahihi wa neno husika.Pia kuzaliwa na Waswahili sio kigezo cha kujua kanuni za matumizi sahihi ya Kiswahili.Ingekuwa hivyo Wazaramo wote shuleni wangekuwa mabingwa wa lugha ya Kiswahili.
 
The Perfumed Garden ... NImekisoma hicho kitabu kitambo, kwa kwlei ni kizuri na kinafunda haswa.

Kaka ...
 
FaizaFoxy namn gani naweza kuwekeza katika dhahabu ?? kwa ajiri ya wakati ujao


Njia nzuri na salama ni kwenda kununuwa moja kwa moja kwa masonara ambayo itakuwa ni ghali kiasi lakini ni akiba. Wanawake wengi sana hupendelea kununuwa kwa masonara vyombo vya dhahabu kwani huwa wanavitumia kwa kuvivaa na huwa ni akiba pia. Hivyo ndiyo walivyofanya wazee wetu.

Kwa siku hizi ukitaka kununuwa dhahabu ya kutosha basi unaruka kwenda Dubai, sheria za huko hautakuta sonara wa kudanganya-danganya na soko la dhahabu ni kubwa sana kuna ushindani wa hali ya juu.

Huko utakuta kuna vipande (vinoo) kabisa vya dhahabu vya kila saizi vinauzwa, na wengi hununuwa kujiwekea akiba.

Hapa kwetu Tanzania unaweza kuchukuwa kibali rasmi cha kununuwa dhahabu na ukaenda sehemu zinazozalisha dhahabu kama Chunya ukajinunulia wanavyoita "vikole", ukija mjini ukimpata sonara unaemuamini anakuyeyushia na kukuwekea vinoo. Hii ndiyo njia ya kununua kwa urahisi kama hutaki kuitumia mwenyewe kwa kujipamba.
 


Hapana, usichanganye mada. Wazaramo wana lugha mama yao, nacho ni Kizaramo.

Jinni ni jina linalotokana na lugha ya Kiarabu, kumbuka hilo. Kwa hiyo kubadili jina ni ujinga tu. Kamusi ya Kiswahili imeandikwa na watu kama mimi na wewe na kama wameandika "jini" basi sina budi kusema uelewa wao kwa jina hilo ulikuwa ni finyu kama wako.

Jina si neno, neno linaweza kuwa jina pia na jina linaweza kuwa neno pia. Lakini Jinni kwa maana halisi inavyotumika hapa ni jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…