Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Awww ukipewa fursa ya kuchagua mtu mashuhuri wa kukutana nae hivi sasa atakuwa nani? Na kwanini?
 
Sura zote zinaanza na bismillahi kutoa moja tu. Hakuna suala la kulipa.
Kiongozi.

Je wafahamu kwanini Suuratu TAWBA haikuanza na Bismillah?

Naomba tuwekana sawa.

Na hesabu Sura zote 114, utakuta kila Sura ina Bismillah kasoro Suuratu TAWBA, ili upate idadi ya Bismillah 114 ihesabie na Bismillah iliyomo kwenye Suuratu NAMLI, ambayo kwa jumla yote unapata,

Sura 114, na Bismillah 114.

Je hapo haijalipia?
 
Wewe sio Faiza bhana tena ni bora ungenijibu, Faiza jibu Post 56 na 244 tafadhali
Nukuu Maneno ya Bibie FAIZA.

"Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu"
 
AUDHU BILLAAHI MINASHAYTWAANI RRAJIIM.

AUDHU BILLAAHI MINASHAYTWAANI RRAJIIM.

AUDHU BILLAAHI MINASHAYTWAANI RRAJIIM.

LadyAJ na Wonderful Basi, inatosha.

Msifikie hatua hiyo, nyie wote kitu kimoja.

Nendeni hata kwa PM mrekebishane, msifike mbali Ndugu zanguni.

Elekezaneni taratibu.

Mnapishana sehemu ndogo sana
 
Ujue mnashindwa kuelewa.

Hizo ni Siasa ambazo zinatumiwa migongoni mwa Dini.

Na hii yote ni kwa ajili ya kuuchafua Uislam.

Hao wana maslahi yao binafsi.

Uislam ambao mnausikia kwenye vyombo vya Habari na Uislam wenyewe ni vitu viwili tofauti
 
Sijaelewa hapo..
Maana kwa ufahamu Jihad..ni Islamic holy war
Sasa ukitohoa kwa kiswahili haileti hiyo maana
Sio kweli.

JIHAD kwa Kiswahili ni KUFANYA JUHUDI.

Sisi WAISLAM tunasisitizwa tufanye JUHUDI katika kila jambo letu.

Nakupa mfano mmoja,

WAMINALLAYLI FATAHAJJAD BIHII, je wafahamu maana yake?

Maana yake ni kwamba, Na fanyeni JUHUDI nyakati za Usiku.

Kivipi?

Ngoja kidogo nikufafanulie.

Wenzako wamelala nyakati za Usiku, wewe unaacha Kitanda chako, labda pengine Mke wako, Watoto wako, Usingizi wako, na kuendelea na Kisimamo cha Usiku.

Hiyo ni moja ya JUHUDI.

Hapo nimekufafanulia kiasi sijataka kuzama sana, Nataka niishie hapa kwa siku ya leo.

InshaAllah nitaendelea kufungua kurasa nyingine kesho kunapo Majaliwa.

Maana huu Uzi unanihusu sana, na nitakuwepo sana
 
Kwa sasa unajishughulisha na nini???

AlhamduliLlah muda mwingi sana nnalea wajukuu nnapokuwa nje ya Tanzania, kama hivi sasa.

Nikiwa Tanzania AlhamduliLlah kuna mambo mengi sana ya kufanya, tafauti tafauti.
 
Umewahi kushika wadhifa gani katika serekali ya JMT

Sijawahi kushika wadhifa wowote serikalini na sijawahi kuajiriwa serikalini bali nimefanya kazi nyingi sana na wizara, idara na taasisi tofauti za kiserikali.
 
swali: Kwa nini Faizafoxy anatetetea wagala kama akina makonda?

Wanapofanya vyema ni haki yao kuwasifia na wasipofanya vyema ni haki yao pia kuwa "criticize", haijalishi ni nani, awe au asiwe "mgala".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…