Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Waislamu muna uhusiano gani na majini na kwa nn yanaitwa kwa majina ya kislamu tu

Majinni ni viumbe vya Allah kama ilivyo wewe na mimi.

Kuna Majinni Waislam na kuna Majinni Wakristo na kuna Majinni yasiyoamini.

Hakuna uhusiano wote zaidi ya kulitambua hilo.

Kuhusu majina, si kigezo kizuri kwani mie nnamfahamu kijana mmoja anaitwa Abdallah lakini si Muislam. Ni maarufu sana katika kanisa la Wasabato hapo Dar.
 
Uislam haujakaa kimya kwa baya lolote.

Sikiliza Radio Imaan ujisikilizie jinsi Uisla unavyokatazza na kukemea mabaya na kuamrisha mema siku zote, Pitia miskitini siku ya Ijumaa, hata kama hutaki kuingia ndani kaa nje ya msikiti usikilize Uislam unavyokataza mabaya na kuamrisha mema.

Nnakushangaa sana unaposema Uislam "umekaa kimya...haukemei". Ajib.
Mama Nmefuatilia kwa ukarbu Sana... Hayo unayodai yanafanyika sidhani Kama ni kweli... Nina mahubir mengi tu ya masheikh maarufu tu.. Hawakemei na wakisema ni mafumbo mafumbo.. Na Wengine wnaunga mkono moja kwa moja.. Mfano sheikh Rogo na wenzie...
 
Njia nyepesi ya kukomboa Talaka ambayo weengi huifanya ni kufanya tendo la ndoa! Yaani ukifanya tendo La ndoa na mwanaume aliyekupa talaka unakua umerudiana nae automatically
Huko no kufanya zinaa hebu tafuta jibu la kweli!
 
Majinni ni viumbe vya Allah kama ilivyo wewe na mimi.

Kuna Majinni Waislam na kuna Majinni Wakristo na kuna Majinni yasiyoamini.

Hakuna uhusiano wote zaidi ya kulitambua hilo.

Kuhusu majina, si kigezo kizuri kwani mie nnamfahamu kijana mmoja anaitwa Abdallah lakini si Muislam. Ni maarufu sana katika kanisa la Wasabato hapo Dar.
Hakuna majini Wakristo, au leta andiko la kuthibitisha.
 
Hivi Alla (Molla) unayemwamini amekuwa dhaifu kiasi cha kuhitaji msaada wetu wanadamu kupigana kwa ajili yake?

Hivi Molla (Alla) unayemwamini hana REHEMA (hasamehe wanadamu).

Ahsante

Si kweli.

Uislam haufundishi ugaidi wala haufungamani na kundi lolote la kigaidi.

Uislam unafundisha:

Qur'an 5:
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

33.Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
 
General Knowledge.

Naam, kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Natumia fursa hii ya mtandao adhyim wa JF kuwapa fursa wanamtandao wote wapate fursa ya kuuliza kuhusu mada au jambo lolote ambalo unataka upatiwe majibu.

Si majibu yote yatatoka kwangu binafsi, bali nitajitahidi iwezekenavyo kukupatia majibu murwa na yanayolingana na swali lako na ambapo sina jibu itakuwa fursa kwa wengine kutoa majibu.

Hapa ni kwa ajili ya kuelimishana na kujuzana bila kikomo, iwe swali lolote liwalo.
Hiyo prfl ni wewe?
 
Sina ubia na FF katika huu uzi lakini next time unapouliza kama ulivyofanya hapa; unatakiwa ku-quote hilo swali ambalo uliuliza manake kwa jinsi ulivyouliza; unatarajia jibu gani zaidi ya "jibu la swali lipi?!" Manake sioni ni namna gani ataanza kurudi nyuma kutafuta hilo swali!!!
Wewe ni msemaji wake?

Je kama nimemuuliza hilo swali sekunde au dakika chache tu zilizopita?
 
Acha uandazi wewe. Angejua kua atachoka kujibu asingeweka Uzi huu
Awe mwanaume awe mwanamke wote hufunzwa nn cha kufanya Mara baada ya tendo la ndoa , kwaiyo sioni mantiki mtu kama kaoa au kaolewa aje aulize kuhusu kutoa Janaba, msimchoshe Faiza wa watu
 
Si kweli.

Uislam haufundishi ugaidi wala haufungamani na kundi lolote la kigaidi.

Uislam unafundisha:

Qur'an 5:
32. Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.

33.Basi malipo ya wale wanao mpiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa.
Utashi wangu unaligomea jibu lako.
 
Back
Top Bottom