Kweli nje kuna fursa nyingi sana lakini, nnawashauri vijana wa Kitanzania kabla ya kukurupuka kwenda nje wasome kwa bidii sana, amma wasomee fani yoyote (vocational training) amma wasome elimu ya juu na ikiwa watatoka kwenda nje basi watoke amma kwa kufata elimu ya ziada amma kwa kufanya kazi ambazo tayari wanazijuwa na wamezitafuta kuanzia huku, yaani anakwenda nje kifuwa mbele na ana ujuzi wake na wasikurupuke.
Nchi zingine zinatowa kabisa mafunzo kwa vijana wao wanaotaka kwenda nje kutafuta maisha, nadhani na Tanzania wangefanya mikakati hiyo ili iwasaidie vijana wanaotaka "kuzamia".
Mfano Canada, hata ukiingia kwenye website ya "immigration" yao utakuta wameweka kabisa watu wanaowahitaji na kama unakidhi vigezo basi huna tatizo kabisa. Una apply na kuondoka kiulaini kabisa, nnawashauri pitieni kwenye tovuti ya ubalozi wa Canada.
In sha Allah, moja katika mikakati ninayofikiria kuianzisha Tanzania ni hilo la kuwawezesha vijana kwenda Canada kihalali na kisheria. Tatizo mimi siwezi kufanya kazi hizo kwa muda mrefu kwa sasa na nitahitaji watu wa kufanya hizo kazi na mimi ntawasimamia kwa "remote".
Kuhusu kufuga, nilianza kufuga kama kitoweo tu, maana nnaishi shamba muda mrefu nikiwa Tanzania, lakini mifugo inazaliana na kujijenga yenyewe kuwa "commercial" kwa kuwa imefikia nnazalisha zaidi kidogo ya matumizi yangu.
Ufugaji wa samaki ni mzuri sana, mimi nilianza kama mchezo mchezo tu lakini sasa nnawauza na wana demand sana. (quantities zangu si kubwa). Nnauhakika samaki wana soko zuri tu kwani watu wanakuja kuchukuwa kwangu Mkuranga kilo shillingi 7,000 na mara nyingi huwa sina wa kuwapa. Na wananishauri niweke kambare watachukuwa kwa 8,000 lakini bado sijaanza kuwaweka.
Nnakushauri anza tu, work hard na "mambo yatajipa".