Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Sitta kishajiondokea zamani, wanajitesa tu kumuweka mpaka leo. Allah amhukumu kwa amal yake ya alipokuwa hai.

Inna li Lllahi wa Inna Ilayhi Rajiun.
Bi mkubwa katika uislam kuna vitabu ndani ya Biblia Takatifu mnavyoviamini Torati na Injili sasa katika hayo kuna Maandiko yameandikwa Mtu asiape na amelaaniwa mtu yule anaeapa chini ya ardhi maana hapo ndipo ninapoweka miguu yangu kama ikitokea mtu akiulizwa na aseme ndio au sio na sio kuapa kwa sasababu mimi Mungu ni mwenye wivu na huwapatiliza wana maovu ya baba zao sasa nataka nijue kipindi cha uchaguzi tunapita mapito mengi wapo wanaokuwepo pale kwa ushindi wa ulaghai wengine dhulma mwisho wa siku anakuja mtu tena bila hofu ya Mungu anashika Biblia Takatifu , Quran Tukufu na kuapa chini ya ardhi tena kwa binaadamu mwenzie huku katika nafsi yake akijua wazi ushindi alioupata umepitia mapito mengi yasiyo halali na hata akimaliza kuapa anafanya kinyume na kile alichokiapa pale mbele ya umma wa watu na je hii si laana ya ardhi juu ya nchi?
 
Mimi nina certificate ya electronics ya mwaka 2006 veta, je unaweza kunisaidia mwongozo nijiendeleze level gani na chuo gani bora kwangu kujiendeleza

Sijuwi kwa Tanzania lakini kama certificate yako inakuruhusu kuanza kuchukuwa degree basi anza, kama haikuruhusu nnahisi unaweza kujiunga na kuchukuwa Diploma. Canada kuna system inaitwa "Post Secondary Education" ambayo unaweza kuchukuwa certificate, diploma, halafu degree.
 
Ahsante nashukuru kwa majibu yako mazuri "Baarakallahu fiik"
 
Bi mkubwa katika uislam kuna vitabu ndani ya Biblia Takatifu mnavyoviamini Torati na Injili sasa katika hayo kuna Maandiko yameandikwa Mtu asiape na amelaaniwa mtu yule anaeapa chini ya ardhi maana hapo ndipo ninapoweka miguu yangu kama ikitokea mtu akiulizwa na aseme ndio au sio na sio kuapa kwa sasababu mimi Mungu ni mwenye wivu na huwapatiliza wana maovu ya baba zao sasa nataka nijue kipindi cha uchaguzi tunapita mapito mengi wapo wanaokuwepo pale kwa ushindi wa ulaghai wengine dhulma mwisho wa siku anakuja mtu tena bila hofu ya Mungu anashika Biblia Takatifu , Quran Tukufu na kuapa chini ya ardhi tena kwa binaadamu mwenzie huku katika nafsi yake akijua wazi ushindi alioupata umepitia mapito mengi yasiyo halali na hata akimaliza kuapa anafanya kinyume na kile alichokiapa pale mbele ya umma wa watu na je hii si laana ya ardhi juu ya nchi?

Waislam tunaamini katika Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an.

Tunasema kama kuna Old testament na new testament basi Qur'an ni final testament.

Unajuwa Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi na kuna madhehebu mengine ya Wakristo kuna vitabu vingine vya biblia hawaviamini kabisa.

Pia hakuna ubishi kuwa kuna watu wanakaa na kuamua hiki kiongezwe, hiki kiondolewe, hiki kibadilishwe. Ndiyo sababu kubwa ya kuwa na versions nyingi sana za Biblia. Kumbuka versions, siyo translations.

Sisi tunaamini kuwa humo humo kwenye mkusanyiko wa hivyo vitabu kuna maneno machahe sana yamebaki kuwa ni kweli mafundisho ya Mwenyeezi Mungu. Na yale ambayo si ya Mwenyeezi Mungu na ni mikono ya watu tu ndiyo mengi zaidi.

On the other hand, Qur'an toka imetujia miaka zaidi ya 1,400 iliyopita haijabadilishwa na haitoweza kubadilishwa kwa sababu Allah ameahidi kuilinda, cha ajabu ni kuwa katupa uwezo sisi wenyewe wa kuilinda. Hakuna kitabu leo hii duniani kilichohifadhiwa kwenye mioyo ya watu kama Qur'an. Kama kipo nijulishe. Jee, kwanini?
 
Mali, mali, mali. Unakuja kuposa binti mwenye mali zake nawe huijuwi mali, kutwa kushinda vibarazani, huijuwi dini, huna nasaba, unategemea u "handsome" wako tu, si kasheshe hiyo? Allah awajaalie vijana wetu wa kike na wa kiume wapate wenza wenye vigezo vyote hivyo kwa manufaa yao na vizazi vyao.
Mali kila mtu anayo isipokuwa tofauti inakuja kwenye wingi wa Mali.. Sasa sijajua inatakiwa nimzidi Au anizidi?
 
Waislam tunaamini katika Taurati, Zaburi, Injili na Qur'an.

Tunasema kama kuna Old testament na new testament basi Qur'an ni final testament.

Unajuwa Biblia ni mkusanyiko wa vitabu vingi na kuna madhehebu mengine ya Wakristo kuna vitabu vingine vya biblia hawaviamni kabisa. Pia hakuna ubishi kuwa kuna watu wanakaa na kuamua hiki kiongezwe, hiki kiondolewe, hiki kibadilishwe. Ndiyo sababu kubwa ya kuwa na versions nyingi sana za Biblia. Kumbuka versions, siyo translations.

Sisi tunaamini kuwa humo humo kwenye mkusanyiko wa hivyo vitabu kunamaneno machahe sana yamebaki kuwa ni kweli mafundisho ya Mwenyeezi Mungu. Na yale ambayo si ya Mwenyeezi Mungu na ni mikono ya watu tu ndiyo mengi zaidi.

On otherhand, Qur'an toka imetujia miaka zaidi ya 1,400 iliyopita haijabadilishwa na haitoweza kubadilishwa kwa sababu Allah ameahidi kulinda, cha ajabu ni kuwa katupa uwezo sisis wenyewe wa kuilinda. Hakuna kitabu leo hii duniani kilichohifadhiwa kwenye mioyo ya watu kama Qur'an. Kama kipo nijulishe. Jee, kwanini?
Hujajibu swali langu nililokuuliza laana ya kuapa chini ya ardhi ndio inayotumaliza usikwepe jibu kiufasaha hata ndani ya Biblia imeandikwa usipunguze nukta wala neno lolote ndani ya Bliblia
 
Kuna hizi sheet za kufugia samaki .
Una uzoefu nazo unaweza jua zinauzwa wapi.

Dah, yes, kama unamaanisha zile plastics kubwa kubwa za kuweka kwenye mabwawa nimezisikia, lakini sijawahi kuzitumia.

Kwa Tanzania na kama upo Dar nnakushauri nenda pale Bagamoyo, Mbegani kama sikosei kuna chuo kabisa cha mambo yote ya samaki, pale utafaidika sana. Lazima watajuwa hivyo vitu na kama kuna vingine pia utapata kuelewa,

Unajuwa hizo plastics nilizisikia Tanzania wakati nafanya bwawa langu la samaki, na nilipopata safari ya kuja Canada nikaziuliza huku Canada na nikakuta huku wanaziita membranes au liners lakini mostly membranes.

pond-liner-examples.jpg

pond-liner-canadas.jpg
 
Hujajibu swali langu nililokuuliza laana ya kuapa chini ya ardhi ndio inayotumaliza usikwepe jibu kiufasaha hata ndani ya Biblia imeandikwa usipunguze nukta wala neno lolote ndani ya Bliblia

Punguza ghadhab, sasa mbona kwenye biblia wanawaondolea vitabu kamili na maneno mazima mazima na nyinyi mnachekelea tu.

Mimi siyo biblia, ngoja niipitie tena post yako, labda nimepitiwa tu, ulifikiri mimi ni robot?
 
Mali kila mtu anayo isipokuwa tofauti inakuja kwenye wingi wa Mali.. Sasa sijajua inatakiwa nimzidi Au anizidi?
Maana sahihi ya hadithi ya Mtume alipotaja kuwa mwanamke huolewa kwa sifa hizo nne ni;
Kwa kawaida mwanaume huvutiwa na kutamani hadi kufikia kuoa mqanamke akiwa na moja ya sifa hizo.
1. Ni mzuri wa sura,umbo(uzuri wake)
2. Mali anazomiliki (mali zake)
3. Awe ametoka kwenye familia mashuhuri. Kwa utajiri,uongozi,busara nk.(kwa nasaba yake)
4. Au awe mcha Mungu. Mwenye maadili na tabia za kidini.(kwa dini yake)

Kisha akatusisitiza kati ya hao wanne mke bora ni yule mwenye dini. Iwapo utampata mwenye dini utakuwa umefaidi.
Si maana ya hadithi kuwa,awe na sifa hizo nne bali sifa hizo zimetajwa kuonesha kuwa ndizo humpelekea mwanaume kuvutiwa ikiwa mwanamke atakuwa na moja ya sifa hizo.
Kwa muislamu unatakiwa kuangalia dini.

Iwapo utampata mwenye dini kisha mrembo sawa.
Ana dini kisha tajiri,sawa.
Ana dini kisha anatoka kwenye ukoo bora pia ni vizuri.
Akiwa na sifa zote nne ni bora zaidi.
Muhimu hapo ni dini
 
Faiza una uhusiano gani na Mohammed Said?

Alama Mohamed Said ni kaka yangu, si kwa kuzaliwa bali kwanza kwa Uislam, pili ahli zangu karibia wote anajuana nao, tatu mimi mwenyewe ananijuwa fika, kasoro ni hizi pen names tu za humu JF, lakini siku nikimwambia ndiyo mimi, atacheka na kushangaa sana. Nne, mitaa aliyokulia yeye ndiyo niliyokulia mimi na kwa aijuae Dar ya enzi hizo, hususan mitaa ya Kariakoo, Gerezani na Jangwani, tuliishi kama one big family. Tano, kwa umri wake, Alama ni mchezo mmoja na kaka zangu na wajomba zangu halisa kabisa na ni marafiki zake sana. Sita, tumeoleana katika ndugu jamaa na marafiki wa kwenye ukoo. Saba, amenifundisha mengi kuhusu historia ya nchi yetu kuliko mwengine yeyote yule. Nane, awajuao yeye wengi mno nami nnawajuwa fika, Tisa, Ana heshima kubwa sana hata katka majibu yake tu utaliona hilo.

Tuwachie hapo kwenye "witr".

Kwa hayo, nadhani umeuona uhusiano tulio nao.
 
Alama Mohamed Said ni kaka yangu, si kwa kuzaliwa bali kwanza kwa Uislam, pili ahli zangu karibia wote anajuana nao, tatu mimi mwenyewe ananijuwa fika, kasoro ni hizi pen name tu za humu JF, lakini siku nikimwambia ndiyo mimi, atacheka na kushangaa sana. Nne, mitaa aliyokulia yeye ndiyo niliyokulia mimi na kwa aijuae Dar ya enzi hizo, hususan mitaa ya Kariakoo, Gerezani na Jangwani, tuliishi kama one big family. Tano, kwa umri wake, Alama ni mchezo mmoja na kaka zangu na wajomba zangu halisa kabisa na ni marafiki zake sana. Sita, tumeoleana katika ndugu jamaa na marafiki wa kwenye ukoo. Saba, amenifundisha mengi kuhusu historia ya nchi yetu kuliko mwengine yeyote yule. Nane, awajuao yeye wengi mno nami nnawajuwa fika, Tisa, Ana heshima kubwa sana hata katka majibu yake tu utaliona hilo.

Tuwachie hapo kwenye "witr".

Kwa hayo, nadhani umeuona uhusiano tulio nao.
aya kachukue udhu twende msikitini leo ijumaa
 
Maana sahihi ya hadithi ya Mtume alipotaja kuwa mwanamke huolewa kwa sifa hizo nne ni;
Kwa kawaida mwanaume huvutiwa na kutamani hadi kufikia kuoa mqanamke akiwa na moja ya sifa hizo.
1. Ni mzuri wa sura,umbo(uzuri wake)
2. Mali anazomiliki (mali zake)
3. Awe ametoka kwenye familia mashuhuri. Kwa utajiri,uongozi,busara nk.(kwa nasaba yake)
4. Au awe mcha Mungu. Mwenye maadili na tabia za kidini.(kwa dini yake)

Kisha akatusisitiza kati ya hao wanne mke bora ni yule mwenye dini. Iwapo utampata mwenye dini utakuwa umefaidi.
Si maana ya hadithi kuwa,awe na sifa hizo nne bali sifa hizo zimetajwa kuonesha kuwa ndizo humpelekea mwanaume kuvutiwa ikiwa mwanamke atakuwa na moja ya sifa hizo.
Kwa muislamu unatakiwa kuangalia dini.

Iwapo utampata mwenye dini kisha mrembo sawa.
Ana dini kisha tajiri,sawa.
Ana dini kisha anatoka kwenye ukoo bora pia ni vizuri.
Akiwa na sifa zote nne ni bora zaidi.
Muhimu hapo ni dini

Naam, na mimi natazama hayo hayo kwa mwanamme atakae kuja kuoana na wa kwangu.
 
Back
Top Bottom