Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Usingeweka hii kitu basi ingekua murua sana, nikushauri tu uiondoe na uwe flexible kujibu swali lolote ndio maana iko huku chit-chat. ni mtazamo wangu tu.
Amesema mwenyew "uliza lolote ujibiwe" hiindo shida ya kukurupuka[emoji196] [emoji86]
 
Sina chuki na Joyce Ndalichako bali nnauhakika si kiongozi mzuri, alivurunda kama mkuu wa NECTA mpaka baadhi ya Waislam wa Tanzania wakaandamana kumkataa. Jikumbushe:

DSC08684.jpg
Tetea waislam[emoji216]
 
Kasome post namba 43.

Licha ya hiyo, kuna kozi nyingi sana na seminars nyingi sana za taaluma mbali mbali nimepitia sehemu nyingi duniani. Lakini katika yote hayo hakuna taaluma niliyoipata zaidi na iliyonifunguwa ubongo na macho kama Qur'an, kusafiri na kujisomea mwenyewe kila nnapopata nafasi.
Ndo mana medulo imekolapsi[emoji90]
 
Ahsante sana kwa darsa adhim bi Faizafoxy.,
Mimi ningependa kufahamu nini Fatwaha yako katika Mwezi mwandamo, kwa kufunga/kufungua kwa Mwezi wa Kimataifa ama unaotangazwa na BAKWATA kuwa umeonekana maeneo fulani kwa Tanzania?
Na je ww huwa unafuata Mwezi mwandamo wa Kimataifa ama unaotangazwa nchini mwako hususani ukiwa Canada?
 
Binafsi huwa sijiingizi sana kwenye ikhtilafu hizo bali huwa nnafata Waislam waliowengi kwenye mji niliopo.

Natumai umenielewa.
 
Ahsante bi Faiza,nimekufatilia mwanzo mwisho vitu vingi nimejufunza sana.umejaribu kujibu hoja zako vizuri kwa quote na reference za kutosha aliekuwa na lengo la kujifunza.swali langu ni kama ifuatavyo
1.wewe kama Faiza unahisi wazazi wanakosea wapi kwenye malezi na imekua vigumu sana hasa kwa sasa kuwa na watoto wenye uwezo hata wa kujielezea wenyewe hasa watoto wa kike wapo lakini kama hawajui kwa nini wapo hapo
2.nini kilikufanya ukafika hapo ulipo unauwezo flani binafsi sitaki kuueleza
3.nini unakifanya kuhakikisha mikoba yako/madini yako unayarithisha hasa kwa jamii inayokuzunguka yasiwe yanaishia
4.Unahis umma wa Kiislam unakosea wapi kwa sasa na kuleta image isiofaa kwa jamii na tabia chafua ambazo uislam haujatufunza
 
Ahsante kwa sifa njema ulizonipa na ahsante kwa maswali yako mazuri.

Maswali kama haya ndiyo tunayataka humu si wengine wanakuja na mizaha na kebehi na kejeli zisizoweza kutuletea tija yoyote.

1) Suala la ulezi ni pana sana na tunaweza tukalijadili kwa marefu na mapana na tusifikie mwisho.

Nnawaomba wachangiaji wengine wote kwenye huu mjadala wa ulezi tujikite na tutoe maoni na mawazo yetu kwa kadri ya muono wetu ambayo nnatumai yatatusaidia sote na vizazi vyetu.

Hapo zamani kidogo wakati mimi nnakuwa mitaa ya Kariakoo kuna kitu nnakikumbuka ambacho sasa sikioni, sijuwi hilo lilikuwa suluhisho la malezi au la. Ni hivi; Kila mtu mzima, awe mzazi wako asiwe mzazi wako alikuwa ni mlezi na muangalizi wako ukipenda usipende, ilifikia hata unaweza kuchapwa kwa kuonekana unafanya utovu wa adabu mtaani na mtu usiyemjuwa.

Kuna siku nnakumbuka, mdogo wangu aliletwa nyumbani huku kakamatwaa mikono asikimbie, kesi yenyewe ilikuwa ni kakamatwa na huyo kijana mitaa ya upanga (enzi hizo upanga bado kuna kimsitu kidogo) na alikamatwa kwa kuwa ana winda ndege na manati na ulikuwa ni wakati wa shule na alikuwa amevaa uniform za shule. Yule kijana aliyemkamata hakupendezwa na hilo na akamshika akamwambia sikuachi mpaka twende kwenu, kufika nae nyumbani akaanza kuelezea kwanini kamleta vile, basi mama'ngu (Allah amrehemu) akamwambi yule kijana subiri, akaingia akatoa mkwaju akmwambia mchape hapa hapa atie adabu. Naam, akachapwa.

Nnakuelezzea hicho kwa uchache ili kuonesha jamii ilivyokuwa zamani, kila mmoja alikuwa na wajib wa kuhakikisha watoto wanakuwa wema. Leo hii yapo hayo?

Tutarudi kwenye mjadala huu wa ulezi, nimelipenda swali lako, napenda wachangiaji tuchangie kwa wingi kwenye hili.

2) Hili sina majibu ya haraka ila nnasema AlhamduliLlah.

3) Umma wa Kiislam hauna unapokosea ila nguvu nyingi zinatumika kuupiga vita Uislam directly na indirectly, hii ni duniani na hasa imelengwa zilipo jamii za Kiislam kwa wingi.

Yasome haya, kisha ufikirie:

A) Nchi zenye Waislam wengi hususan za Mashariki ya kati, utakuta ving'amuzi vinakamata channel za ngono zaidi 100 na ni bure, kilichofanywa ni kuwafanya kama mjione mna akili sana ya ku hack ving'amuzi kumbe ni njama za kuwafanya muingie kwenye mkumbo na tamaduni hasi.

b) Tazama pwani ya Afrika mashariki inavyojazwa mahoteli ya kitalii kwenye fukwe zake ambako 99% ya wakazi wake ni Waislam. Cha kushangaza 99% ya hizo hoteli ni za Wataliano. Imeanzia Malindi, Kenya inashuka hadi kujaza Zanzibar na sasa inashuka Mafia, na kuelekea kusini ya pwani yote.

Jee, ni biashara tu? Ni maswali ya kujiuliza.

Natumai kuanzia hayo inabidi tujifikirie na tuendeleze mjadala.

Nnaamini wao wanapanga lakini hakuna shaka kuwa mbora wa wapangaji ni Allah Subhana wa Taala.
 
Naomba ushauri:Nashukuru Mungu ameniwezesha kuwa na elimu nzuri ya kawaida lakini ni mchache katika elimu ya dini kiasi ninaona wivu napowaona wengine wenye elimu ya dini.Niliishia juzuu ya kwanza tu na mara nyingi natumia msahafu wenye tafsiri.Natamani niweze kuhifadhi quran juzuu zote,nimejaribu kusoma articles mbalimbali mitandaoni bado hazijanisaidia.Tafadhali kwa hekima,elimu na maarifa uliyo nayo naomba unisaidie.
 
Nnakushauri hapo ulipo nenda msikitini kaonane na immam na umueleze hilo naye atakuwa msaada mkubwa sana kwako.
 
Back
Top Bottom