Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Faidika na darasa la FaizaFoxy; Uliza chochote utajibiwa

Vipi kuhusu maisha ya kaburini, kuna kuonana kama tunavyoonana kwa hapa duniani, hiyo baada ya kufa?, na kutembeleana ?

Na mwili wako utakuwa unauona kama unavyouona ukiwa hai?

Shukralaki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi siamini kama kuna maisha ya kaburini.

Naamini maisha ni uhai na ukiuacha uhai unaingia kwenye umauti na utahuishwa tena siku ya Qiyama. Pia naamini hautaihisi tofauti ya muda, ni kama kulala na kuamka tu.

Allahu 'allam
 
Nimeshakujibu

Sasa kwa mujibu wa aya je mtume alikuwa anakosea kukata watu viganja badala ya mkono kama isemavyo Qurani?

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
Naona ume quote post wrong. Hiyo nilikuwa namjibu mtu mwengine.

Kuhusu swali lako la kukatana mikono, nitakujibu usiwe na haraka. Nimeliona.
 
Binafsi siamni kama kuna maisha ya kaburini.

Naamini maisha ni uhai na ukiuacha uhai unaingia kwenye umauti na utahuishwa tena siku ya Qiyama. Pia naamini hautaihisi tofauti ya muda, ni kama kulala na kuamka tu.

Allahu 'allam
Mada hizi ndo shule sasa, wakija malaika wasikutishe.

Na tunakufisha na kukuhuisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Qurani pekee inatosha bila hadithi n.k

Kama Qurani pekee inatosha,Kwa nini Allah aliwafunza mitume Kitabu na HIKMA?
Naona licha ya kujaribu kukufahamisha kuwa weka swali au hoja moja moja haikuingii. Ngoja nikusaidie. Tuanze na hilo la juu kwanza.

Je, aya hiyo niliyokuwekea umeisoma na kuielewa? Nairudia...

Qur'an 6:114. Je, nimtafute hakimu ghairi ya Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi? Na hao tulio wapa Kitabu wanajua ya kwamba kimeteremshwa na Mola wako Mlezi kwa Haki. Basi usiwe katika wanao tia shaka. 114

Je, bado unaitilia shaka Qur'an japo unasoma kwenye aya hiyo kuwa "Mwenyezi Mungu, naye ndiye aliye kuteremshieni Kitabu kilicho elezwa waziwazi" ?

Kama hiyo haikutoshi soma Allah anasema nini kuhusu Qur'an...

Qur'an 17:

17_45.gif

45. Na unapo soma Qur'ani tunaweka baina yako na wale wasio iamini Akhera pazia linalo wafunika. 45

17_46.gif

46. Na tunaweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasije wakaifahamu, na tunaweka kwenye masikio yao uziwi. Na unapo mtaja katika Qur'ani Mola wako Mlezi peke yake, basi wao hugeuka nyuma wakenda zao.46

Nifahamishe umeelewa nini katika hizo aya tuone kama tunakwenda sambamba.
 
Unaipinga Qurani?
Binafsi siamni kama kuna maisha ya kaburini.

Naamini maisha ni uhai na ukiuacha uhai unaingia kwenye umauti na utahuishwa tena siku ya Qiyama. Pia naamini hautaihisi tofauti ya muda, ni kama kulala na kuamka tu.

Allahu 'allam

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
 
Unaipinga Qurani?

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
Nnaipinga Qur'an? Mbona swali la kiajabu sana hilo?

Nipinge muongozo wetu kutoka kwa Allah?

Astaghafiru Allah. Naona sasa tunakoseana heshima.

NinI kilichokufanya mpaka uulize swali hilo la ajabu?
 
Hili ni darsa siyo darasa. Kuna tofauti ya darasa na darsa. Darasa ni lile lenye kuta nne shuleni. Darsa ni elimu inayotolewa popote kwa njia yoyote.

Hapa unaweza kuuliza chochote au kujibu chochote kwa swali lolote ili wote tuelimishane. Rejea post namba moja.
Mwenyezi Mungu ni mmoja, Allah, lakini anatumia uwingi, kwa mfano anasema "tumekutelemshieni..., tumekuumba..." hatumii umoja, kwanini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona unapinga maisha ya kaburi ilhali Qurani imezungumza wazi juu ya kuwepo maisha ya kaburini.

Au hujapinga kuwepo kwa maisha ya kaburi nilikunukuu vibaya mama yangu?
Nnaipinga Qur'an? Mbona swali la kiajabu sana hilo?

Nipinge muongozo wetu kutoka kwa Allah?

Astaghafiru Allah. Naona sasa tunakoseana heshima.

NinI kilichokufanya mpaka uulize swali hilo la ajabu?

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
 
Sijaona kwenye Qur'an hayo maisha ya kaburini. Weka aya.

Ingawa umerukia swali la mtu mwengine, yako yanakungoja juu huko.
Naona unapinga maisha ya kaburi ilhali Qurani imezungumza wazi juu ya kuwepo maisha ya kaburini.

Au hujapinga kuwepo kwa maisha ya kaburi nilikunukuu vibaya mama yangu?

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
Sijapinga pahali bali nimesema siamini kuhusu "maisha" ya kaburini. Ukinipa aya ya Qur'an nitaamini kweli kuna "maisha ya kaburini".

Mpaka dakika hii hujanipa aya. Na ukishindwa kunipa aya ya "maisha ya kaburuni" basi nawe ukiri kuwa hakuna maisha hayo na usiamini hivyo.

Sawa?

Nasubiri.
 
Swali gani ambalo sijajibu la kwako mbona nilishayajibu?

Siwezi kuingia kwenye mada ya maisha ya kaburi na siwezi kutoa aya mpska unijibu swali langu lile la KUKATA MKONO.

Ebu weka ambalo sijajibu
Sijaona kwenye Qur'an hayo maisha ya kaburini. Weka aya.

Ingawa umerukia swali la mtu mwengine, yako yanakungoja juu huko.

Sijapinga pahali bali nimesema siamini kuhusu "maisha" ya kaburini. Ukinipa aya ya Qur'an nitaamini kweli kuna "maisha ya kaburini".

Mpaka dakika hii hujanipa aya. Na ukishindwa kunipa aya ya "maisha ya kaburuni" basi nawe ukiri kuwa hakuna maisha hayo na usiamini hivyo.

Sawa?

Nasubiri.

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
 
Swali gani ambalo sijajibu la kwako mbona nilishayajibu?

Siwezi kuingia kwenye mada ya maisha ya kaburi na siwezi kutoa aya mpska unijibu swali langu lile la KUKATA MKONO.

Ebu weka ambalo sijajibu

ukiacha kuchagua jua umechagua kuacha
Pitia uzi juu kidogo utayakuta. Usiwe na haraka, nenda soma taratibu ujibu.
 
Inabidi, lakini umeshasema vijana, mara nyingi ukiwa kijana unakuwa mtukutu, twende nao hivyo hivyo huku tunawapa darsa. Wakikuwa wataacha.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji45] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] tisha mbaya
 
Back
Top Bottom