Side B,
1.Mshairi na Mwanafasihi Tiban Liyong baadhi ya vitabu vyake- The last Word,Another nigga dead aliwahi kusema kwamba Africa Mashariki ni Jangwa la Usomaji hiyo ikiwa ni Mwaka1969,
Lakini Wanazuoni na Wasomi wa wakati huo walimpinga sana huku akishumbuliwa kwa maneno Makali...
Sasa imepita miongo minne na zaidi,
Swali,
a) Wewe Waonaje hali ya Usomaji wa vitabu nyakati hizi kwa Wanaafrica Mashariki..???
b)Nini Nafasi ya Usomaji vitabu katika kuleta Maendeleo ya Mtu binafsi na Maendeleo ya Taifa kwa Ujumla...?
2. Karume raisi wa kwanza wa Zanzibar aliwahi kusema "Muungano ni kama koti,Waweza kulivua likikubana" Haya yanapatikana katika kitabu cha Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru, kilichoandikwa na Harithi Ghassany.
a)Yapi Mapungufu Makubwa ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ..?
b) Wewe unamtazamo gani na maoni gani kuhusu Muungano,Muungano uvunjwe au Uimarishwe...?
c) Zipi faida na hasara za kuvunja Muungano..?
3.Ushawahi kuandika kitabu chochote kile kiwe cha Siasa,Uchumi,Mahusiano,Sayansi au dini,Michezo/Tamaduni na vinginevyo...?
a)Ipi hasara ya kusoma vitabu..?
b)Nini anakikosa Mtu asiye na utamaduni wa kusoma vitabu...?
4. Mwalimu Nyerere"Mchonga" katika moja ya hotuba zake aliwahi kusema huwa anatembea na biblia na kajitabu ka'azimio la Arusha akadai huwa anakasoma anakurudia hajaona pabovu kabisa.
a)Nini Maoni yako kuhusu Azimio la Arusha...?
b)Nini pungufu/kasoro kubwa ya Azamio la Arusha..?
c)Nini maoni yako Juu ya Oscar kambona Moja ya wapigania uhuru wa Tanganyika...?
4.Awamu ya Kwanza ya uongozi Tanganyika/Tanzania Mambo gani Makubwa ilifanikiwa na kosa gani kubwa ilifanya..?
a)Yapi Mapungufu ya Mwalimu nyerere katika Uongozi..?
b)Wewe unafikiri Mwalimu anapewa sifa anazositahili...?
c) Mambo gani muhimu ya kujifunza katika awamu ya Kwanza...?
5.Mimi Naamini Maendeleo bora huletwa na mawazo bora yaliyofanyiwa kazi,Mawazo bora hupatikana kwa kuwa na Elimu bora.
a)Mfumo Wetu wa Elimu unamapungufu gani Makubwa...?
b)Tume ya Makweta ya Mwaka 1982 Walipendekeza Lugha ya kiswahili itumike kuanzia ngazi ya Awali mpaka c huo kikuu lakini ilishindikana Nadhani ripoti zitakuwa zinakojolewa na Panya kabatini...Nini maoni yako kuhusu lugha ya kufundishia kitumike Kiswahili au kiingereza na kwanini...? au vyote kama ilivyo sasa...?
c)Wewe unadhani Elimu katika Taifa letu inapewa kipaumbele kikubwa au imeachwa nyuma kama mkia wa Mbuzi...?
6.Mwanamama kutoka Zambia Dambisa Moyo Mwandishi wa Dead Aid na How the west was lost huku pia akiwahi kufanya kazi World Bank...Anasema na kutoa maelezo ya kuwa World Bank Na IMF hazina msaada katika kuinua chumi za Africa zaidi zinatuingiza katika mzigo wa madeni.
Unamaoni gani kuhusu World Bank na IMF katika kuinua uchumi wa Nchi Maskini haswa Nchi za Kusini mwa Jangwa la sahara..?
a)Ipi faida na hasara ya Mfumo wa Ujamaa...?
b)Ipi faida na hasara ya mfumo wa Ubepari..?
c)Tanzania yasasa tunafaata mfumo gani..?
d)Je kuna Mfumo bora zaiidi kuliko Ujamaa au Ubepari..?
Sent using
Jamii Forums mobile app