Faiza Foxy live interview on DJ sepetu show!!

Faiza Foxy live interview on DJ sepetu show!!

Nimefutilia Uzi huu tangu mwanzo.Nilichokigundua ni wivu uliopitiliza kwa baadhi ya wachangiaji.Kuna vijana wameanza kumchukia kwa kasi Muosha rungu.Wanaona pengine interview anazoziandaa zinazidi kumletea umaarufu.Ndio maana wanajitahidi kuleta mizaha kwenye interview ili zionekane hazina maana!!!Nakuomba uwapuuze mkuu wengi ni utoto tu unawasumbua wakikuwa wataacha.
 
Pamoja na maangalizo yako unayoyaweka, we dogo unasababisha vurugu mwenyewe... Uzi unauanzisha saa kumi na moja kasoro robo wakati usahili unaanza saa 12. Hapa katikati unategemea hawa vijana wasiojua kufuata masharti watafanyeje??

Mtu maarufu kama FaizaFoxy vijana wengi wana shauku ya kumuuliza maswali ili wapate uzoefu wake katika maisha. Sasa muda wote huu unakatika lazima itokee vurugu tu.

Bahati mbaya sana, maswali ambayo walipaswa kumuuliza baada yako, kiherehere chao kimewafanya wayaulize kabla usahili haujaanza na matokeo yake hawajajibiwa na lawama zote wanakuangushia wewe...

Hongera kwa kipindi kizuri lakini jaribu kurekebisha kasoro ndogo ndogo ili uende sawa na vijana wenzako. nakushauri usahili uanze papo kwa papo ili kutowapa nafasi watu kuchakachua...

Baada ya kuandika hayo, mimi babu yenu narejea kitandani kupumzika na bibi yenu.
Chakuongezea hapo pia apange muda wa yeye kuuliza maswali yake kadhaa kisha awape nafasi wengine.

Jamaa anauliza maswali kwa masaa matatu watu siwatakuwa washauchoka uzi?

Maswali yenyewe haulizi ya msingi.

Kinachowafanya watu walete fujo ni yeye mwenyewe kukosa busara.

ilipaswa awe na kikomo cha maswali yake na muda.
 
FaizaFoxy, hebu angalau kwa ufupi, uhuru wa kuabudu dini ya Uislam katika nchi za magharibi ukoje ukilinganisha na Afrika hasa Tanzania?
 
Back
Top Bottom