Familia aliyegongwa na mwendokasi yahaha kumtibia akisubiri kulipwa

Familia aliyegongwa na mwendokasi yahaha kumtibia akisubiri kulipwa

Hakuna wa kumlipa hata aende popote kama hana watu ,
Wanasubiri msiba tu waufadhili.

Karibu Tz
 
Ningekuwa mwanasheria hii case ningeisimamia ili alipwe haki zake, ni uonevu sana kwa watu maskini. Ingekuwa serikali ya Dkt Magufuli hakika angekuwa keshalipwa, lakini kwa huu upigani unaweza kuta hela watu ilishatoka na wakala na mhanga kapewa kidogo. Hakika Tanzania imegeuka ya wachache
Ki Bongo Bongo eti Wanasheria wanasema hairusiwi kufanya hivyo,lazima ulipe fee ya kisheria kwanza ndiyo uhudumiwe kisheria!!
 
Ghafla bin vuu jamaa kawa mlemavu,halafu waliosababisha hawajali....maisha ya mwanadam yamejaa mateso,mahangaiko na shida tupu,ukiwa mzma,mshukuru mno Mungu!
Waswahili wanasema "hujafa hujauumbika"
 
kweli serikali yetu ione aibu sio kutuza Simba na Yanga ilhali tayari zina wafadhili.. huu sio uungwana kwakweli.
Watanzania wenzangu. Hawa watawala wako pale kwa sababu ya matumbo yao. Fedha wanazotoa kwenye timu za mpira zinawapa faida ya kuendeleza kupumbaza wadanganyika waliolala fofofo huku mali zao zikipigwa. Wanajua huko kwenye mpira ndiyo kuna ''nyumbu'' wengi. Sasa wakimpa huyu msaada unadhani watapata faida yoyote? Amkeni!
 
Juzi nimeshuhudia mlango wa Mwendokasi wakati unafungwa ukamkata mtu kidole cha mkono, kikadondokea ndani. Jamaa libidi ashuke.

Dereva aliambiwa lakini akaondoa zake gari. Wafanyakazi kituoni hawajui la kufanya.
Duh! Inasikitisha Sana
 
Watanzania wenzangu. Hawa watawala wako pale kwa sababu ya matumbo yao. Fedha wanazotoa kwenye timu za mpira zinawapa faida ya kuendeleza kupumbaza wadanganyika waliolala fofofo huku mali zao zikipigwa. Wanajua huko kwenye mpira ndiyo kuna ''nyumbu'' wengi. Sasa wakimpa huyu msaada unadhani watapata faida yoyote? Amkeni!
Serekali hapa tunaionea tu,hili swala ni la Bima watende haki tu waache ubabaishaji kisa Watanzania tulio wengi ni Ma layman! Wale wenye information za huyu Jamaa kulipwa naomba wamuongoze hadi apate haki yake anayo stahili Kama majeruhi wa ajali!!
 
Serekali hapa tunaionea tu,hili swala ni la Bima watende haki tu waache ubabaishaji kisa Watanzania tulio wengi ni Ma layman! Wale wenye information za huyu Jamaa kulipwa naomba wamuongoze hadi apate haki yake anayo stahili Kama majeruhi wa ajali!!
Kazi ya serikali ni kuongoza watu, unalijua hili? Kwa hiyo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha hata wale wasiojua taratibu, wanajulishwa wafanye nini.
 
Ki Bongo Bongo eti Wanasheria wanasema hairusiwi kufanya hivyo,lazima ulipe fee ya kisheria kwanza ndiyo uhudumiwe kisheria!!
Inapaswa kuingia makubaliano tu ili hela ikilipwa na wakili analipwa, ni %
 
Unalikumbuka tukio la basi la mwendokasi lililoacha njia na kugonga ukuta wa jengo lililopo Kisutu jijini Dar es Salaam huku likimkosa mwenda kwa miguu aliyekuwa akikatisha mtaani hapo? Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tira) imesema anastahili kulipwa fidia.

Wakati Tira ikisema hivyo, familia ya Osam Milanzi aliyenusurika katika ajali hiyo ya Februari 22, inapitia sintofahamu ya kumtibu ndugu yao.

Hata hivyo, Esha Mohammed, mke wa Osam hafahamu chochote kuhusu fidia hiyo, akidai mawasiliano yao na mabosi wa mwendokasi yalikatika tangu mumewe aliporuhusiwa kutoka hospitalini.

“Tangu ametoka hospitali hatuna msaada wowote, wale waliomsababishia ajali tumeambiwa walipaswa kugharimia malipo ya hospitali tu, aliporuhusiwa kurudi nyumbani hakuna kingine tunachokifahamu kutoka kwao. Aprili 4 anapaswa kurudi kliniki, anahitaji kupata wheelchair, dawa, magongo na hata lishe, maisha yetu tulimtegemea yeye hivyo tunasubiri kudra za Mwenyezi Mungu tu,” alisema Esha.

Anasema mumewe bado ana maumivu ya mkono wa kulia na mguu wa kushoto ambao alifanyiwa upasuaji na kuwekewa vyuma.

“Hata upasuaji ulichelewa baada ya kutakiwa kulipa Sh600,000 ambazo familia hatukuwa nazo na wale waliomsababishia ajali walizitoa kwa kuchelewa,” alisema.

Nyumbani kwa Osam, Manzese Midizini, watu wakiwamo majirani, ndugu, jamaa na marafiki hawakauki kumjulia hali, ingawa mkewe anasema huwa anaangua kilio kumbukumbu zinapomrudia na kuwatambua waliomtembelea.

“Baada ya ajali, amepata tatizo la kupoteza kumbukumbu, unaweza kumuuliza kitu, anapoanza kukujibu anabadilisha na kuzungumza kitu kingine,” anasema Esha na ndicho kilitokea hata alipozungumza na gazeti hili juzi Alhamisi nyumbani kwake, katikati ya mazungumzo yalibadilika na kuanza kuomba radhi akieleza ni kwa sababu hakutekeleza ahadi yake ya jana.

Mkewe alilazimika kumkatisha kwa kumtikisa na kumuita jina lake, ndipo anarudi kwenye mazungumzo ya kawaida.

“Hii ndiyo changamoto yake, ni baada ya kuumia kichwani katika ajali ile japo daktari aliniambia atakuwa sawa na katika vitu ambavyo amesema tusimuulize ni kuhusu ajali, kwani inaweza kumrudisha kwenye kumbukumbu mbaya zaidi na kumsababishia tatizo jingine,” alisema.

Tangu kutokea kwa ajali ile, alisema Osam hafahamu wala hakumbuki kama aligongwa na basi ila anajua kwamba anaumwa.

“Hata tulipokuwa hospitali, kuna muda alikuwa akiniuliza ni kwa nini yuko pale, anachokifahamu ni mgonjwa, ila nini kimesababisha yeye kuwa kitandani hafahamu hadi sasa,” alisema.

Kwa hali aliyonayo mumewe, anasema hawezi kufanya kitu chochote kwa sasa hata kunyanyuka na kufanya mazoezi ni kwa msaada wa magongo ambayo alisaidiwa na jirani yao mmoja japo si ya saizi yake ila wanayatumia hivyohivyo.

“Hawezi kupanda daladala, inapofika siku ya kwenda kliniki, lazima tujue anafikaje. Mguu alifanyiwa upasuaji na kuwekewa vyuma, japo ulichelewa kutokana na pesa iliyohitajika kupatikana kwa kuchelewa, watoto wanahitaji kwenda shuleni, nauli, chakula na mahitaji mengine kama baba alikuwa akiyafanya yeye, sasa hana uwezo huo,” alisema Esha, mama wa watoto watatu.

Esha ambaye ni mama wa nyumbani anasema mwanzoni baadhi ya wasamaria wema waliwasaidia na kupata ahueni ya maisha.

“Kwa sasa hatuna kitu, kula yetu ni ya siku hiyohiyo tunachokipata, kikiisha basi hatufahamu kesho itakuwaje. Osam ndiye alikuwa kila kitu kwetu, sasa ni mgonjwa hawezi kufanya chochote, kila kitu anahitaji kusaidiwa kutokana na hali yake,” alisema Esha.

Kwa hali aliyonayo mumewe, Esha anaomba msaada wa wasamaria. Ili kumsaidia Osam, unaweza kuwasiliana na mkewe kwa namba 0748 152 830 iliyosajiliwa kwa jina la Esha Mohammed Issa.

Esha anayemwelezea mumewe kuwa alikuwa mtu wa kuswali sana, anasema siku ya tukio kama kawaida yake aliamka kuwahi swala ya asubuhi.

“Huwa anapenda kufanya mazoezi, alifanya hapa nyumbani, akajiandaa na akaniaga anakwenda msikitini kisha ataelekea kibaruani.

mwendokasi-pic.png

Mke wa Osam na mumewe​

Swala ilimuokoa Sana. Maana ni mtu anayependwa kuswali.
 
Nchi hii kwenye maswala ya kulipana lazima kuwepo na zengwe

Ova
 
BIMA unawajua unawasikia?

Watasema ni uzembe wa dereva, kamshtaki Dereva
Dereva anashtakiwa ndio, lakini kama ana angalau third party basi kisheria hiyo thirdparty ina wajibika kumlinda mtu wa tatu aliyeumia
 
Serikali ebu mlipeni huyo Jamaa
Na siyo kumlipa tu kumpatia huduma zote za kimsingi ili at least arudi katika hali yake !!!!! vyombo vya habari viendelee kupaza sauti na ikiwezekana na sisi humu tumpe msaada!!!
 
Serikali ebu mlipeni huyo Jamaa
Utashangaa huo mradi wa mwendokasi kila saa kila siku bus zinazunguka barabarani kutwa wanakusanya pesa na nauli zimepandishwa body ya huu mradi inashindwa nini kukaa kikao ikajadili namna ya kumsaidia huyu muhanga?

Nina imani haya ktk sheria zao kuna maelekezo namna ya ku-deal na watu wanaosababishiwa matatizo na magari yao nini kinawafanya wasiharakishe wanaacha victim wao anateseka namna hii?hizo hela wanatoa zao mifukoni?siyo haki kabisa ukichukulia mtu ana familia inamtegemea
 
Back
Top Bottom