Familia inateseka sana. Nisaidieni natafuta Kazi, Kibarua

Asano

Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
53
Reaction score
170
Habari wana JF,

Mie kijana wa kiume, naishi Dodoma! Nina mke na mtoto mchanga wa miezi 4. Kitaalum ni muhitimu wa Bachelor ya Computer Science, na nilikuwa nimeajiriwa sehem lkn tulipunguzwa kipindi kile janga la corona limepamba moto.

Sina kazi maalum kwa muda sasa, naunga unga tu kiukweli, nikibahatisha kupata kazi ya mtu binafsi mfano kutengeneza website au la kidogo imekuwa ikinibeba hasa kulipia kodi, lkn sijapata hizo kazi kitambo sasa! nimejaribu sana na bado naendelea kutuma maombi lkn sijafanikiwa, hali imekuwa ngumu kweli kweli kwetu! Nafanya vibarua sometimes hadi vya kubeba zege japo tu familia ipate mlo hasa mke anaenyonyesha!

Lakini saa nane kasoro hii usiku naandika hapa, tumelala njaa, leo nimejaribu vibarua bila mafanikio, hatuna hata sh. mia hapa ndani, imeniuma sana ndio maana nimekuja kwenu kuomba kazi, kibarua chochote halali hata cha kipato kidogo tu!

Mtoto wa miezi minne imebidi tu aanze kunywa uji maana mlo wetu mmoja kwa siku mama anakosa maziwa ya kutosha!

Mwenye chumba kanivumilia hadi kachoka kaniambia nikabidhi tu chumba, japo hii laptop naitumia kwa kazi zangu, lakn kama kuna mteja wana JF naiuza laki3, au kama kuna mtu anakopesha niiweke bond, atunusuru tafadhalini tunatolewa kwenye hii nyumba!

Nipo tayari kuja popote kufanya kazi/kibarua chochote halali! Naombeni sapoti nateseka sana, hasa huyu mzazi kulala njaa hivi inanipa stress sana!

Kwa mawasiliano, namba zangu 0767 960 255 au 0629 531 358.

Natanguliza Shukrani na Mungu atubariki!
 
Nenda hapo mjini ulizia zinapo patikana ofisi za kampuni ya ulinzi inaitwa GARDAWORLD SECURITY nenda pale hautakosa kazi mshahara wao ni 300,000 kwa mwezi ila utachukua 280,000 baada ya makato.

Nenda wale jamaa kila siku wanaajiri tena kama unaweza nenda Arusha kwenye ofisi zao hutochukua muda utakuwa umesha anza kazi.

Uza hiyo laptop muachie mke hela wewe kapambanie hiyo kazi
 
Nenda hapo mjini ulizia zinapo patikana ofisi za kampuni ya ulinzi inaitwa GARDAWORLD SECURITY nenda pale hautakosa kazi mshahara wao ni 300,000 kwa mwezi ila utachukua 280,000 baada ya makato...
Umeongea kirahisi sana aisee...duh.

Mtu hata ya mlo wa mchana hana we unamuambia nenda Arusha kuna kazi, anaendaje? Atafikia wapi? Akifika siku hiyohiyo anapata kazi? Hata akipata kwani ndio analipwa siku hiyohiyo? Kula kulala hadi mwisho wa mwezi itakuwaje?

Na hata ofisi ya hapa Dar sio kwamba ukifika tu unapata kazi uhakika, tusidanganyane jamani.

Naunga mkono apite hapo lakini tusiongee kama motivational speakers.
 
Nashukuru sana sana wana Jamii Forum kwa sapoti yenu,nadhani si busara kutaja majina yenu hapa na wengine tayari tumeshaongea! Namba yangu ya halotel ipo kwenye modem,kuna wanaopiga wanaona sipatikani,lkn ya voda 0767 960 255 ipo kwenye simu!NASHUKURU SANA,lkn issue mama bado,ya kupata kibarua ili niwe na kipato endelevu hata kama kidogo!kabla mke hajajifungua nilikuwa na ka biashara ka maziwa fresh nilikuwa naenda sehem na baiskeli nalangua lita 1500 then nauza mjini lita 2000,lkn uzazi wake ulikuwa na complications kdogo,akajifungua kwa Operation,nikawa niko karibu zaid naye namuhudumia kiasi biashara ikayumba,mtaji ukakata pia kutokana na gharama za hospital na kumuhudumia pia plus maziwa bei ilikuwa juu!Hapa namaanisha kama siwezi pata kazi kwa sasa,kama kuna mdau anaweza nikopesha au kunishika mkono niendelee na hyo biashara yangu,tena kpind hiki cha mvua malisho yanapatikana hvyo maziwa pia yataanza kuwa mengi na kushuka bei,yalipanda.
 
Habari wana JF,

Mie kijana wa kiume, naishi Dodoma! Nina mke na mtoto mchanga wa miezi 4. Kitaalum ni muhitimu wa Bachelor ya Computer Science, na nilikuwa nimeajiriwa sehem lkn tulipunguzwa kipindi kile janga la corona limepamba moto.

Sina kazi maalum kwa muda sasa, naunga unga tu kiukweli, nikibahatisha kupata kazi ya mtu binafsi mfano kutengeneza website au la kidogo imekuwa ikinibeba hasa kulipia kodi, lkn sijapata hizo kazi kitambo sasa! nimejaribu sana na bado naendelea kutuma maombi lkn sijafanikiwa, hali imekuwa ngumu kweli kweli kwetu! Nafanya vibarua sometimes hadi vya kubeba zege japo tu familia ipate mlo hasa mke anaenyonyesha!

Lakini saa nane kasoro hii usiku naandika hapa, tumelala njaa, leo nimejaribu vibarua bila mafanikio, hatuna hata sh. mia hapa ndani, imeniuma sana ndio maana nimekuja kwenu kuomba kazi, kibarua chochote halali hata cha kipato kidogo tu!

Mtoto wa miezi minne imebidi tu aanze kunywa uji maana mlo wetu mmoja kwa siku mama anakosa maziwa ya kutosha!

Mwenye chumba kanivumilia hadi kachoka kaniambia nikabidhi tu chumba, japo hii laptop naitumia kwa kazi zangu, lakn kama kuna mteja wana JF naiuza laki3, au kama kuna mtu anakopesha niiweke bond, atunusuru tafadhalini tunatolewa kwenye hii nyumba!

Nipo tayari kuja popote kufanya kazi/kibarua chochote halali! Naombeni sapoti nateseka sana, hasa huyu mzazi kulala njaa hivi inanipa stress sana!

Kwa mawasiliano, namba zangu 0767 960 255 au 0629 531 358.

Natanguliza Shukrani na Mungu atubariki!
Pole sana kijana mwenzangu,najua changamoto unazopitia najiona kama mimi vile,Naomba vijana wenzangu kila mtu ajitolee angalau buku mbili mbili ili kuweza kumkimu kipindi iki iki akipitiacho,Allah akufanyie wepesi
 
Asante ndugu,Amin!
 
Nenda hapo mjini ulizia zinapo patikana ofisi za kampuni ya ulinzi inaitwa GARDAWORLD SECURITY nenda pale hautakosa kazi mshahara wao ni 300,000 kwa mwezi ila utachukua 280,000 baada ya makato.

Nenda wale jamaa kila siku wanaajiri tena kama unaweza nenda Arusha kwenye ofisi zao hutochukua muda utakuwa umesha anza kazi.

Uza hiyo laptop muachie mke hela wewe kapambanie hiyo kazi
Wengi vimo vinatuangusha mkuu, mi nimejaribu kwenda pale Mikocheni kila kitu kikawa sawa. But tatizo kimo tu, japo kuna wengine niliwaona nawazidi urefu ila wako pale wanafanya kazi. Nikasema haya bn, kisicho ridhiki hakiliki!
 
Nashukuru sana sana wana Jamii Forum kwa sapoti yenu,nadhani si busara kutaja majina yenu hapa na wengine tayari tumeshaongea! Namba yangu ya halotel ipo kwenye modem,kuna wanaopiga wanaona sipatikani,lkn ya voda 0767 960 255 ipo kwenye simu!NASHUKURU SANA,lkn issue mama bado,ya kupata kibarua ili niwe na kipato endelevu hata kama kidogo!kabla mke hajajifungua nilikuwa na ka biashara ka maziwa fresh nilikuwa naenda sehem na baiskeli nalangua lita 1500 then nauza mjini lita 2000,lkn uzazi wake ulikuwa na complications kdogo,akajifungua kwa Operation,nikawa niko karibu zaid naye namuhudumia kiasi biashara ikayumba,mtaji ukakata pia kutokana na gharama za hospital na kumuhudumia pia plus maziwa bei ilikuwa juu!Hapa namaanisha kama siwezi pata kazi kwa sasa,kama kuna mdau anaweza nikopesha au kunishika mkono niendelee na hyo biashara yangu,tena kpind hiki cha mvua malisho yanapatikana hvyo maziwa pia yataanza kuwa mengi na kushuka bei,yalipanda.
Mtaji ulikuwa wa bei gani mkuu?
 
Back
Top Bottom